Uchaguzi 2020 Mwanza Huduma adaiwa kumwaga pesa kama Njugu Bunda Mjini akisindikizwa na Viongozi wa CCM Wilaya

ataishia hapo wazichuke tu ten waombe na zaidi lakini hakatizi kamati kuu!
 
Kwa mwana ccm wa kawaida akishapewa kushika uchumba lazima amchague huyo gabachori

In God we Trust
Huyo ni asili yake hata asingepewa angemchagua,muhimu wamwage hela tu tugawane halafu saa ya kura ndo watajua kuwa kura ni siri.
 
Nipo hapa madras india kwa mwezi wa tatu sijawahi kumuona mwafrika akiongoza hata kitongoji. Nashangaa huko kwetu wahindi ndiyo wameshika hatamu

In God we Trust
Acha ubaguzi usio kuwa na mantiki. Hawa ni watanzania wenye asili ya India babu zao waliletwa na wakoloni kujenga reli. Sasa unataka kuwabagua bila sababu.
 
Pascal Mayalla,
Tatizo Ni Sheria ya uchaguzi khs suala la bajeti na matumizi ya kampeni kutoainishwa vizuri... Hiyo Ni fursa kwa watia nia, wapambe na wapigika kura.

Sidhani Kama mtu akiamua kugawa fedha zake kwa hiari Ni kutoa rushwa.. Takukuru wangeusika endapo kingekuwa Ni kipindi Cha kampen za uchaguzi.

Kwa kuzingatia muda wa kampeni bado ktk vyama na ktk uchaguzi mkuu..
 
Mimi sioni ubaya wowote Kama kaamua kugawa hela zake bill kunishikizwa na yeyote,,,
Agawe tu
 
Watafuneni tu lkn hapa India hata kwa dawa huwezi kumkuta eti msukuma ni mbunge au mkurya ni mbunge au mdengereko ni mbunge au diwani hapa India
Acha ubaguzi usio kuwa na mantiki. Hawa ni watanzania wenye asili ya India babu zao waliletwa na wakoloni kujenga reli. Sasa unataka kuwabagua bila sababu.

In God we Trust
 
Watafuneni tu lkn hapa India hata kwa dawa huwezi kumkuta eti msukuma ni mbunge au mkurya ni mbunge au mdengereko ni mbunge au diwani hapa India

In God we Trust
Ni kwa sababu hawakupelekwa huko na wakoloni na kuacha masalia ya vizazi vyao.
 
Acha ubaguzi usio kuwa na mantiki. Hawa ni watanzania wenye asili ya India babu zao waliletwa na wakoloni kujenga reli. Sasa unataka kuwabagua bila sababu.
Kwanza huko Madras india ulienda lini? India imezuia ndege zote kuingia na wewe unasema una siku tatu. Ndio maana mnatuwekea X ray picture za mikono ya wanaume ambazo mmezidownload kwenye mitandao ili mpate kick. Mbona mnafeli sana nyie vijana wa Ex Dj. Tumieni akili kuliko nguvu. Mmekuwa na propaganda za kishamba na za kizamani.
 
Ungekuwa na akili usinge ji quote

Katika hali ya kushangaza Zury Nanji maarufu kama Mwanza Huduma Mfanyabiashara wa Jijini Mwanza ameonekana Bunda Mjini akigawa pesa hadharani.

Huku akiwa na mabaunsa, wapambe na wanakwaya wakimsindikiza Mwanza Huduma amepita Vijiwe vya Kahawa na Maegesho ya Magari na kugawa kati ya shilingi Elfu 50 na laki moja kwa watu hadharani, Pia amepita kwa baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na kumwaga laki mbili na laki tatu.

Akionekana kujiamini amekusanya baadhi ya wazee katika nyumba moja ya Balozi Semeni Kasuku na kutoa Laki NNE.

Wapambe wa karibu nae wamekabidhiwa shilingi Milioni Moja na kuanza kugawa Elfu kumi Au Elfu kumi na tano kwa Vijana wa Bodaboda na Wanakwaya maalum kwaajili ya kumpamba 'mgombea' huyo.

Kabla tukio hilo la kujitokeza hadharani, Baadhi ya Viongozi akiwemo Mwenezi wa CCM Wilaya Ndugu Bonavencha Makanga akiwa na wasaidizi wake walipita kwa Makatibu wa Kata na kuwapatia posho (rushwa) na baadhi ya Wenyeviti kama sehemu ya salam za Mhindi huyo ambae ameanza kampeni mapema kabla ya muda.

Leo walipoulizwa kwanini wanafanya mambo hayo hadharani bila kuogopa Mpambe wa karibu ajulikanae kama Masalu na Mwingine Selemani Nasoro walisema wamepata kibali kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya hivyo hawatishwi na mtu.

Hali hii isipodhibitiwa Bunda Mjini wagombea watatoana Taya maana Rushwa kwa viongozi wengi inatisha kama Corona.
Kura ni ya siri! HUna sababu ya kuacha pesa ya bwege. Pesa chukuwa ukipiga kura soma akili yako. Kama munaona hiyo ni akili ya kuwa kiongozi basi endeleeni lakini kwa maelezo machache uliyotoa yaonesha hana kitu kichwani kitakachoisaidia Bunda.
 
Back
Top Bottom