Pamoja na juhudi za air Tanzania kupeleka kuboresha huduma Mwanza; ila vibanda vilivyojengwa mbele ya uwanja ni aibu kwa nchi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
870
4,062
Huduma ya usafiri wa ndege kwenda Mwanza imeimarika sana. Ndege zipo nyingi na zinatoa huduma masaa ishirini na nne kwa kupishana anagani.

Wageni wengi wanaingia Mwanza sasa hivi, baadhi ya wasafiri kutoka nchi jirani wanapandia ndege Mwanza.

Kila ninapopita katika uwanja huu napatwa na msongo wa mawazo! Sijui ni nani alitoa vibali vya ujenzi mbele ya uwanja. Mbele ya uwanja kuna vibanda vya chakula, ofisi, vyoo nk ambavyo vimejengwa bila kuzingatia masharti ya ujenzi wala ubora.

Niombe mtu akipita uwanja wa Mwanza ahesabu makontena madogo madogo yaliyowekwa nje, ahesabu vibanda vidogovidogo vilivyo jengwa like kila ukitaka kujenga unapewa Sehemu yako.

Hali ya uchafu uwanjani inatia aibu na kutatiza juhudi za Mhe. Rais. Viongozi wa uwanja na jiji la Mwanza mnasubiri hadi Mhe Rais aje awaeleze chakufanya? Kwanini msibomoe hivi vibanda kama mnavyowabomolea machinga stendi na mjini?

Mhe. Makala tembelea uwanjani, may be unapita ukiwa ndani ya gari pamoja na viongozi wenzako. Nenda kesho kakague pale naamini utapavunja na kujenga au kubipanga vyema vibanda huku ukisimamia usafi.

Kumbuka hii hoja tuliwahi kuileta kwenu sisi watu wa sekta ya utalii mwaka juzi na mliweka ahadi yakupapanga upya ila bado kimya.
 
Kuna wakati viongozi wanaweza wakadhani wamepunguza matatizo ila kumbe yapo yamejificha.

Tukitumia majukwaa kuwakumbusha inawasaidia kuondoka ofisini na kwenda mtaani kutatua kero.........

Air Tanzania wamepeleka abiria wengi sana Mwanza.....wamiliki wa Uwanja waione hii kama fursa waondoe mazingira duni uwanjani
 
Mwamza bhana sielewagi kabisa shida nini...Hii stand ya Nyegezi haikupaswa kabisa kujengwa upya hapa wangesogeza mbele buhongwa hukoo..Ona sasa daladala zinapata shida kuingia na kutoka mpaka zizunguke nyuma ya Stand..Nyingine zinatokeo pakuingilia
Foleni isiyo na maana
Yaani aisee
 
Uholela umetapakaa Tanzania nzima...

Nenda Dar uone barabara zinajengwa, halafu nusu ya barabara inamegwa na wauza biashara kwa kujenga vibanda au kupanga vitoroli...
 
Hilo sio tatizo ila umekagua chumba cha abilia kusubilia ndege,, kile ni kibanda au padsangers louge? Huduma za mwanza aitport bado ni duni zinatia aibu.
Unasema mwanza. Kuna njombe.hata Stendi ya mabasi ya Abc imeipita ubora. Bado wale wafanyakazi wa mamlaka ya viwanja vya ndege wanafaja jodging na kutusha Matangazo
 
Kuna nini airport ya Mwanza kila Rais anayekuja anautelekeza uwanja huu muhimu kiuchumi,inaumiza sana, Samiah kwa kile kinachojulikana uhodari wako wa miradi hili la uwanja usicheke nao Wizara na TAA walisema wapewe wao watoe kitu kizuri ukawapa na pesa ukatoa sasa wanashindwa nini kama siyo dharau kwa mamlaka za juu
 
Mwamza bhana sielewagi kabisa shida nini...Hii stand ya Nyegezi haikupaswa kabisa kujengwa upya hapa wangesogeza mbele buhongwa hukoo..Ona sasa daladala zinapata shida kuingia na kutoka mpaka zizunguke nyuma ya Stand..Nyingine zinatokeo pakuingilia
Foleni isiyo na maana
Yaani aisee
Blacks
 
Back
Top Bottom