Mwanza City: The Photo Gallery

Mwanza City: The Photo Gallery

Nimeona watu mnalalamika . mwanza tunaonewa kwenye miundombinu..vipi hii miradi mikubwa ni gharama ghani imetumika .
daraja la busisi bilion 700
meli bilioni 70
......nje ya dar hamna jiji jingine lilipewa fedha za maendeleo kuzidi mwanza ..

Kwa hyo tulitakiwa tuchague ,, billion 700 zisijenge daraja zijenge vifuatavyo na hela ingetosha fresh
njia nne Usagara to town -billion 40
njia nne kisesa town -billion 35
Interchange buzuruga -billion 90
feeder roads nyamagana km 70-bilion 100
Feeder roads ilemela km 70-bilion 100
Njia nne kisesa Usagara -billion 25
Njia nne pasiansi buzuruga bilion 15
Uwanja wa Mpira Watu 30000 bilion 50
Apartment za kisasa milima ya mbugani, mabatini na pamba -billion 150
mzee upo vizuriiii Kama ingekuwa hivi lingekuwa Jambo la maana mno o
 
njia nne Usagara to town-billion 40
njia nne kisesa town -billion 35
Interchange buzuruga -billion 90
feeder roads nyamagana km 70-bilion 100
Feeder roads ilemela km 70-bilion 100
Njia nne kisesa Usagara -billion 25
Njia nne pasiansi buzuruga bilion 15
Uwanja wa Mpira Watu 30000 bilion 50
Apartment za kisasa milima ya mbugani, mabatini na pamba -billion 150

Daraja la busisi lisingejengwa ...pesa zake zingetosha kujenga hyo miradi
Hivi capripoint hamna kiwanja? Nimechoka vumbii
 
Bwana intelligent Mimi kwa kweli hamna kitu kinaniuma kama kushadadia tu vitu Kama tu stand kwe limji likubwa hivi, stand zinamaana gani Kama mji uliopakana na ziwa eti wananchi wake hawana access ya maji, mibarabara yote ni vumbi tu mingi umechoka, kwa Karne hii ile barabara ya kutoka buhongwa kwenda kishiri ni ya kukosa lami kweli!

Ifike muda tukubali tu huu bado ni mji wa kishamba mno, ni maeneo machache tu ya kueleweka we mwenyewe hili unalijua na ndo ukweli
Mimi pia huwa nashangaa sana badala tutoe mawazo namna ya kuboresha mji uliopo tunashadadia Lodge, vituo vya mafuta, stand za daladala, frame za maduka, huwa nachoka.
As if Tuko sawa na njombe au misungwi nk
 
Nchi hii sijui ina matatizo gani.

Kwenye Masterplan mpya ya Jiji inaonesha Usagara, Fela na Kisesa kuwa sehemu ya Jiji lakini mpaka sasa kiuwekezaji Ilemela na Nyamagana wanayakwepa hayo maeneo kwasababu haziwanufaishi kwa sasa.
Hii mambo ya Nyamagana na Ilemela inatakiwa kuvunjwa iwe kitu kimoja tu,
Kama kuna umuhimu za kuwepo basi zisisimamie miradi bali iundwe halmashauri ya jiji la mwanza itakayohusika na mapato na miradi kwa jiji zima.
Hii inaweza rahisisha hata upatikanaji wa wilaya mpya maana mapato na matumizi ya wilaya zote zitakazounda jiji yatasimamiwa na chombo kimoja, hivyo hawatagombania maeneo.
 
Mimi pia huwa nashangaa sana badala tutoe mawazo namna ya kuboresha mji uliopo tunashadadia Lodge, vituo vya mafuta, stand za daladala, frame za maduka, huwa nachoka.
As if Tuko sawa na njombe au misungwi nk
Mimi kwa upande wangu kutanuka kwa mji sio deal tena, Mwanza tayari ni jiji kubwa mpaka limeanza kuingia kwenye Halmashauri nyingine, yaani kutanuka kwa jiji la Mwanza sio kwa kulazimisha kama wanavyofanya Dom. Muhimu waboreshe miundo mbinu yote ndani ya metropole, na ikiwezekana wazuie uendelezaji wa maeneo ya pembezoni.
 
Hii mambo ya Nyamagana na Ilemela inatakiwa kuvunjwa iwe kitu kimoja tu,
Kama kuna umuhimu za kuwepo basi zisisimamie miradi bali iundwe halmashauri ya jiji la mwanza itakayohusika na mapato na miradi kwa jiji zima.
Hii inaweza rahisisha hata upatikanaji wa wilaya mpya maana mapato na matumizi ya wilaya zote zitakazounda jiji yatasimamiwa na chombo kimoja, hivyo hawatagombania maeneo.
Uko sahihi, ila naomba tujadili, mnapowanyan'ganya misungwi eneo la usagara mnakuwa na maana gani? Au kisesa kutoka Magu yani what is the point? Kwa hiyo hizo misungwi na Magu zibaki vipi? Me naona mkoa wa Mwanza na wilaya zake kunatakiwa kuwe kumebalance, siyo ilemela na nyamagana tu ndo pawe mjini, hata sengerema, Magu, misungwi ziwe na hali flani ya kuwa urban areas, hata mkoa wote wilaya zake zikipata hadhi ya kuwa manispaa inakuwa vizuri zaidi, kuliko kuwachukulia urban centers zao na kuziingiza ndani ya jiji, kwangu haina maana
 
Hii concept tayari ilikuwepo kabla ya mwaka 2012 . ilemela na nyamagana zilikuw chini ya chombo kimoja .MCC Hadi zilipovunjwa ,Kwa mujibu wa taratibu za ugatuzi wa madaraka Kila wilaya inatakiwa isimamie shughuli zake za maendeleo yenyewe chini ya Chombo chake ..na ndio maana halmashauri ikavunjwa ,hata hvyo bado Kuna mgogoro wa namna ya kuita nyamagana.either iwe manispaa au ibakj na kuwa jiji la mwanza.....
Cha muhimu hapa nashauri kuwepo na miradi ya ubia kati ya halmashauri mbili ili kutengeneza win to win situation.otherwise migogoro katika miradi ya maendeleo haiwezi kuisha hapa Tanzania
 
Uko sahihi, ila naomba tujadili, mnapowanyan'ganya misungwi eneo la usagara mnakuwa na maana gani? Au kisesa kutoka Magu yani what is the point? Kwa hiyo hizo misungwi na Magu zibaki vipi? Me naona mkoa wa Mwanza na wilaya zake kunatakiwa kuwe kumebalance, siyo ilemela na nyamagana tu ndo pawe mjini, hata sengerema, Magu, misungwi ziwe na hali flani ya kuwa urban areas, hata mkoa wote wilaya zake zikipata hadhi ya kuwa manispaa inakuwa vizuri zaidi, kuliko kuwachukulia urban centers zao na kuziingiza ndani ya jiji, kwangu haina maana
Kinachosababisha ni upatikanaji wa huduma kwa uraisi kwa wananchi wa Usagara na Kisesa. Kwao ni rahisi kupata huduma Mwanza CC na Ilemela MC kuliko kwenda kwenye DC zao.
 
Mimi kwa upande wangu kutanuka kwa mji sio deal tena, Mwanza tayari ni jiji kubwa mpaka limeanza kuingia kwenye Halmashauri nyingine, yaani kutanuka kwa jiji la Mwanza sio kwa kulazimisha kama wanavyofanya Dom. Muhimu waboreshe miundo mbinu yote ndani ya metropole, na ikiwezekana wazuie uendelezaji wa maeneo ya pembezoni.
Kwan metro pole inaishia wapi ..na hapa inabidi tuzungumzie maendeleo ya mkoa mzima Kwa sababu bila wilaya za pembeni kuendelea tukubali tukatae Mwanza itabaki stagnant haiwezi kuendelea.
 
ila benki ya dunia wanajenga barabara aisee sio mchezo cheki ya sabasaba buswelu halafu hii ya igoma to buhongwa ilitakiwa njia nne
Imekula panga baada ya mzee kufa, kuna sehemu huwa natafuta mabula akisema ni njia nne.
Toka mzee afe imekuwa njia 2.

Tuvumilie tu si mnaona hata DIT mza imekuwa 19b badala ya 37b.
 
Uko sahihi, ila naomba tujadili, mnapowanyan'ganya misungwi eneo la usagara mnakuwa na maana gani? Au kisesa kutoka Magu yani what is the point? Kwa hiyo hizo misungwi na Magu zibaki vipi? Me naona mkoa wa Mwanza na wilaya zake kunatakiwa kuwe kumebalance, siyo ilemela na nyamagana tu ndo pawe mjini, hata sengerema, Magu, misungwi ziwe na hali flani ya kuwa urban areas, hata mkoa wote wilaya zake zikipata hadhi ya kuwa manispaa inakuwa vizuri zaidi, kuliko kuwachukulia urban centers zao na kuziingiza ndani ya jiji, kwangu haina maana
Naunga mkono hoja ..inabidi maendeleo yaende beyond.sio ilemela na nyamagana tu ..
 
Kwan metro pole inaishia wapi ..na hapa inabidi tuzungumzie maendeleo ya mkoa mzima Kwa sababu bila wilaya za pembeni kuendelea tukubali tukatae Mwanza itabaki stagnant haiwezi kuendelea.
Metropole ni Nyamagana yote. Ila hata Ilemela in the near future inaweza kuwa metropole
 
Mimi kwa upande wangu kutanuka kwa mji sio deal tena, Mwanza tayari ni jiji kubwa mpaka limeanza kuingia kwenye Halmashauri nyingine, yaani kutanuka kwa jiji la Mwanza sio kwa kulazimisha kama wanavyofanya Dom. Muhimu waboreshe miundo mbinu yote ndani ya metropole, na ikiwezekana wazuie uendelezaji wa maeneo ya pembezoni.
Kukua Kwa mji hakuzuiliki kaka ,.....Hilo linawezekana tu Kwa kuboresha miji ya pembeni au wilaya .Ili watu wasivutiwe sana kuhamia miji mikubwa wabaki kwenye miji midogo ... other wise watu wataendelea kuhamia kwenye majiji...... marekani wameweza kutengeneza miji mingi ya siZe ya kati ,,,,hivyo watu hawaoni haja ya kukimbilia new York au Los Angeles
 
Maendeleo ni kama Mwanga Boss, Jiji haliwezi ng'arishwa Ilemela ikabaki imepauka. Nimegusa Metropole kwa sababu ndio taswira ya JIJI.
Khaaa... nyamagana ndio jiji tangu Lin ... nyamagana haina sifa za kuwa jiji ...
 
Yes kuna mji kuwa mkubwa halafu Kuna mji kuwa na bora
Ndio maana napinga mji kupanuka, bora tuuboreshe, tunashabikia frame, huko dodoma sehemu mpya zinazojengwa unaona frame za maduka hovyohovyo kama mza?

Hivi kusimamia watu kwamba eneo hili ukinunua kiwanja jenga hivi na ezeka vigae au bati jekundu, huwezi acha nenda kajenge Sengerema.
Je hii nayo ni kazi ngumu kwa viongozi halafu mnakuwa mnapita kila baada ya mwezi kuona maendeleo ya ujenzi, aliyekiuka piga faini na kuvunjiwa, tutashika adabu ila rushwa imetujaa sana kuliko kusimamia haki
 
Back
Top Bottom