Mwanza: Amchoma mkono Mwanaye kisa kudokoa Chainizi

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
208
462
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia, Maneno Thomas (35) mkazi wa Chamagati, wilayani Sengerema kwa tuhuma za kumchoma mikono mtoto wake kwa maji ya moto baada ya kumtuhumu kudokoa mboga ya majani aina ya chainizi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa, ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 30, 2023, baada ya kutoka katika shughuli zake.

Mtafungwa ameeleza kuwa mtuhumiwa alipofika nyumbani kwake alimwambia binti yake aitwaye Prisca Maneno (11), apike chakula cha usiku ndipo alipoelezwa kuwa hakuna mboga, kwani ililiwa na mdogo wake Daniel Maneno (9), ambaye anasoma darasa la pili Shule ya Msingi Mtakuja.

"Maneno Thomas alishatengana na mkewe kutokana na vitendo vyake vya kipigo cha mara kwa mara na mwanamke aliamua kuondoka," amesema Mtafungwa.

Amesema mtuhumiwa aliwasha moto kisha kuchemsha maji yalipochemka, alimuita mwanae Daniel Maneno na kumwagia maji hayo katika mikono yake yote miwili na kumsababishia maumivu makali.

Anasema baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa aliamua kumfungia mtoto huyo chumbani kwake na wananchi wa eneo hilo walishtuka kutomuona mtoto Daniel siku mbili mfululizo, ndipo walipoanza kufatilia na kugundua amefanyiwa ukatili huo.

Imeandaliwa na Cyprian Magupa, Mwanza .

Sources Via Habari Leo
 
Madhara ya kuwa mwanachama wa ccm kupindukia ukishidwa kupata pesa za wizi ni utaenda magereza kwa kesi za kijinga..
 
Kuna wakati binadamu huwa nyang'au sijui Mungu katuumba namna gani
Mwanao unamuunguza kisa chakula miaka 9 mpaka anakula chines manaake Baba hujui majukumu yako yaani watoto hawashibi na unacholeta
NB:Huyo sio baba bora Sheria ifuate mkondo wake


Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
umasikini ni laana.
Ni lana kweli,kijana wangu jana tu katafuna nusu kilo nzima ya kitimoto,
Kazuga kufichaficha ila mi najua kala kiasi gani.
Sasa utampiga?
Ni mwanao nikacheka tu kula kilichobaki basi hata sijauliza.
Mwanangu kala kitu changu hasa chakula.
Si chake nayeye pia.
 
Back
Top Bottom