Geita: Baba amchoma mwanaye mikono

Ngasere45

Senior Member
Dec 31, 2022
149
565
Mtoto Elizabeth Mathias Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ziwani Mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita Mkoani Geita ameunguzwa mikono miwili kwa kulowekwa kwenye maji ya moto na Baba yake mzazi (jina halijatajwa) baada ya kumkuta akiwa na shilingi 5000 ambazo alishindwa kueleza alikozitoa.

RPC wa Geita, Safia Jongo amekiri kumkamata Mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo huku akisema Mtoto huyo amekuwa akilelewa na Mama yake wa kambo ambaye pia alishiriki katika kutekeleza tukio hilo.

Kamanda Safia amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutoa rai kwa Wananchi kuacha tibia za kuwaadhibu Watoto kikatili na kusema atakayekaidi atachukuliwa sheria.

Millard Ayo
 
haya matukio ya kuchomana mbona yamashika kasi sana kosa kidogo fire burning, si katika mapenzi tu hata ngazi ya familia wat wanachomana
 
wakusuma kubalini tu hamna akili sawasawa.
mambo ya kijinga yote yanatokea huko
Screenshot_20230407-144226.jpg
 
Roho mbaya huwa mtoto anaingizwa na wazazi wake KWA matendo kama haya
 
Pana mwanamke mpumbavu mmoja alienda kupiga umbea kwa jirani kaacha nyama jikoni, mtoto njaa imebamba akaanza kula nyama jikoni. Mama mtu kurudi nyama imepungua akaanza mpiga mwanae KISHA akamchoma moto mikono ya mwanae. Akiishi nae KWA maumivu ndani siku tatu baba yake alisafiri. Mtoto alizidiwa akapelekwa hospitalini kufika hospital mtoto kawekewa damu na maji.
Manesi wanamwambia mwanamke mpumbavu "angalia gharama ulizotumia kumtibu mwanao kwann ukununua nyama nyingine " maana zinazidi hata thamani ya nyama yenyewe. Mtoto alipata matibabu baada ya wiki mtoto akafariki. SAsa hapa unalia nini wakati mzazi umemkataa mtoto Mungu kaamua kumchukua sababu umeshindwa kumtunza mtoto.
Wazazi wengine ni wachawi kabisa.
 
Unapomfanyia ukatili wowote mtoto shida wataenda pata wengine mfano mke , mme, wanafunzi, ofisini, Jamii nk wakati huo mzazi amekaa miguu juu.
Chochote upandacho mzazi watakaoathirika ni wengine. Mfano kiongozi akiwa ni dikteta akaua watu wake mzazi huwezi kwepa laana ya dhambi ya mtoto uliyemlea kwa ukatili utotoni.
 
Back
Top Bottom