Adaiwa kumuua mwanaye mchanga na kumzika shambani

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Maurine Anyango ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Oyugis katika kaunti ndogo ya Rachuonyo Kusini nchini Kenya kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mchanga na kumzika katika shamba moja katika kijiji cha Kawiti.

Maurine alikamatwa Jumamosi usiku baada ya majirani zake kuwa na mashaka baada ya kutomuona mtoto huyo wa siku moja, na kutoa taarifa polisi ambapo walikwenda moja kwa moja kuwahoji watoto wa mwanamke huyo ambao walifichua kilichotokea.

Watoto wake wameeleza kuwa walimuona mama yao akimzamisha mtoto huyo katika maji baridi siku ya Ijumaa, na waliporejea nyumbani kutoka shuleni baadaye siku hiyo walimuona mtoto huyo kitandani, akiwa amefungwa kitambaa cheupe.

Imeelezwa kuwa baadaye usiku mwanamke huyo alimuomba binti yake wa darasa la sita amsindikize hadi shambani katika kitongoji hicho, ambapo aliuzika mwili huo
Muda mfupi baada ya tukio hilo kuripotiwa, mtuhumiwa aliwaongoza polisi hadi eneo ambalo alimzika mtoto huyo na kuwaonesha
 
Back
Top Bottom