Ukatili dhidi ya watoto: Baba amchoma mikono mwanaye kisa kudokoa mboga aina ya dagaa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Screenshot 2023-11-28 103324.png

MTOTO Grace Mwita mwenye umri wa miaka mitano, mkazi wa mtaa wa Starehe wilayani Tarime mkoani Mara amechomwa mikono kwa moto na baba yake mzazi Mwita Abdala na kumsababishia majeraha na maumivu makali akimtuhumu kudokoa mboga aina ya dagaa iliyokuwa imepikwa na baba huyo kwa ajili ya chakula cha mchana.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, Novemba 28, 2023 ambapo baba wa mtoto huyo, amekiri kufanya tukio hilo la kumchoma moto mikono mtoto wake kisa alidokoa mboga.

Chanzo: Nipashe
 
Huyo mzee fara sana. Mpaka mtoto anafikia hatua ya kudokoa maana yake hali akashiba.

Badala huyo fara ajiongeze apambane watoto wale washibe yeye anachoma mikono.

Peleka gerezani hiyo takataka.
 
Umasikini mbaya sana
Mtoto mpaka anadokoa means ana njaa mpakulie .na tabia hazirekebishwi Kwa kuwa katili
 
Huyo mzee fara sana. Mpaka mtoto anafikia hatua ya kudokoa maana yake hali akashiba.

Badala huyo fara ajiongeze apambane watoto wale washibe yeye anachoma mikono.

Peleka gerezani hiyo takataka.

Kabisa kiongozi,imeniuma sana!huyo mzee apelekwe gerezani moja kwa moja kwa kuwa tayari amekiri kosa!huyo mtoto kama hakuna wa kumchukua wanipe nimlee tafadhali
 
MTOTO Grace Mwita mwenye umri wa miaka mitano, mkazi wa mtaa wa Starehe wilayani Tarime mkoani Mara amechomwa mikono kwa moto na baba yake mzazi Mwita Abdala na kumsababishia majeraha na maumivu makali akimtuhumu kudokoa mboga aina ya dagaa iliyokuwa imepikwa na baba huyo kwa ajili ya chakula cha mchana.
Jana kulikuwa na uzi wa kumlaani Paulina kwa kumfanyia ukatili Hashimu sijui hii ya Grace na Abdala itazungumziwaje!!
 
Kabisa kiongozi,imeniuma sana!huyo mzee apelekwe gerezani moja kwa moja kwa kuwa tayari amekiri kosa!huyo mtoto kama hakuna wa kumchukua wanipe nimlee tafadhali
Akudokolee mboga nawe umfukuze awe choko? Ebu wacha watoto wakunjwe na wazazi kabla walimwengu hawajashika mipira ya moto.
 
Tegemeeni ukatili kutamalaki Zaid kadri ya muda unavyokwenda.
Binadamu walipo Sasa hawapendani Kama ilivyokuwa awali.
 
Mwita ameyatimba. Wachonga vinyago original wanamsubiri wamshep hiyo tabia akitoka atakuwa amenyooka hivi....
pic-magereza.gif
 
MTOTO Grace Mwita mwenye umri wa miaka mitano, mkazi wa mtaa wa Starehe wilayani Tarime mkoani Mara amechomwa mikono kwa moto na baba yake mzazi Mwita Abdala na kumsababishia majeraha na maumivu makali akimtuhumu kudokoa mboga aina ya dagaa iliyokuwa imepikwa na baba huyo kwa ajili ya chakula cha mchana.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, Novemba 28, 2023 ambapo baba wa mtoto huyo, amekiri kufanya tukio hilo la kumchoma moto mikono mtoto wake kisa alidokoa mboga.

Chanzo: Nipashe
Umasikini ni aghali.
 
Kabisa kiongozi,imeniuma sana!huyo mzee apelekwe gerezani moja kwa moja kwa kuwa tayari amekiri kosa!huyo mtoto kama hakuna wa kumchukua wanipe nimlee tafadhali
Adhabu ya gerezani inaadhibu wote baba na mtoto. Nani atamhudumia mtoto baba akifungwa?
Huyu ahukumiwe viboko 12 kila siku hadi mtoto apone. Na alipe nauli za mgambo wa kwenda kumchapa kila siku na ma mwita wengine wajifunze.
 
Inaweza kuhatarisha maisha ya mtoto akiendelea kukaa nae
 
Back
Top Bottom