Mwandosya anatutia hasara ya mamilioni kwa mwezi

Mwandosya anatutia hasara ya mamilioni kwa mwezi

pesa anayolipwa na pesa inayoibwa na mafisadi ipi nyingi au mwandosya alikufanyia kitu mbaya maana umeonesha chuki yako wazwaz! pole bana samahani unalotaka HALIWEZEKANI
 
Pamoja na kumshambulia mleta mada, mimi nina maoni kiasi tofauti na yeye na wengine lakini yanaendana kimaudhui!
NI BUSARA PROF. MWANDOSYA AKAACHISHWA KAZI KWANI KI UKWELI HAMNA TIJA KATIKA KAZI ALIYONAYO SASA. LAKINI SERIKALI IEDELEE KUGHARAMIA MATIBABU YAKE, KAMA AMBAVYO INAFANYA KWA WATU WENGI WATANZANIA AMBAO NI MASKINI NA WANATIBIWA KWA MUDA MREFU SANA NA SERIKALI.

Na huo ndo ukweli!
 
ugojwa kapatia kazini we mkeo akipata ugojwa ukiwa naye utamuacha ukatafute kipotabo eti kwa sababu ni dhaifu na ukimuacha aende wapi_?
 
Naona jamaa mnamshambulia kweli kweli kana kwamba katenda dhambi kubwa kutoa maoni yake. Maoni yake naona yana msingi sana ingawa watu hamtaki kuona hasa alichokusudia kusema, au amekisema kwa namna ambayo hamjapendezwa nayo.

Nadhani cha msingi si kuondoa taratibu za tiba yake, lakini ni ukweli kwamba katika hali aliyo nayo pamoja na uwezo mkubwa alionao hayuko katika nafasi nzuri ya kutimiza wajibu wake kama waziri. Haiwezi kuwa dhambi kama atapunguziwa majukumu ya uwaziri kwa sasa, akapata tiba kwanza hadi apone kabisa then mteuzi anaweza kumpa nafasi ya kutumika huenda hata kwenye nafasi nyeti zaidi kuliko aliyo nayo sasa.

Kama ambavyo pilot akipoteza uwezo wa kuona hawezi endelea kuendesha ndege katika hali hiyo kwa kuwa tu ni pilot mahiri, atatibiwa kwanza akipona kisha ndo anarejea kwenye U-pilot wake.
 
Watanzania tuna chuki mbaya sana na hii itatumaliza wenyewe kwa wenyewe,

Yaani Binadamu mwenzako anaumwa but wewe inakuuma kuona anagharamiwa Matibabu, ndiyo serikali ya ccm inatutesa sana lakini kwenye wagonjwa tuache uadui as haujafa haujaumbika
 
Tatizo lako unaonekana ni mvivu wa kufikiri, upende usipende Prof. Mwandosya ni muhimu sana kwenye nchi hii kuliko unavyofikiri wewe na hivyo vimilioni unavyovisema ni vidogo sana kuliko anavyolipwa huko Marekani kwa utaalamu wake tu.

Ndugu yangu nchi hii haiendeshwi kama unavyofikiri wewe, kuna watu wenye akili na hekima zao wanaotoa ushauri kipi kifanyike. Kama hujui umuhimu wa Prof. Mwandosya subiri Mwezi Mei, 2015 utajua.

Edward Lowasa alimpa sumu ili kumuua au kumpunguza kasi ya 2015 sasa ataona mwenyewe. Mtu mwenye hekima huwa halipizi kisasi kwa maovu anayotendewa.

Acheni unafki na ukabila Mtu mgonjwa akae hospital au Nyumbani ,utaratibu wa serikal ni kuwapa watu wenye afya na akili nafasi si walio hoi ktandani ,gari bovu kwao ni garage au juu ya mawe si njiani...............Mwandosya anapaswa kujipima ,kujitazama na kujifikiria kama kweli anastahili kulala na kula jasho letu kama waziri;ona wananchi wanavyoteseka ...........kikwete kampa cheo ili Wanyakyusa wampende na wasimpige mawe tena;ila Uraisi hapati
 
Mtoa mada ni mnafiki wa kutupwa , hajatoa tathmini ya mchango wake yeye kwa taifa ili tumwelewe , ndiyo maana nimemtakia kifo yeye na nduguze ili atoe mchango wake kulipunguzia taifa matatizo.

Hajajibu, nafikiri anajiweka yeye mbele zaidi kuliko wengine katika mustakabali wa nji hii.

Mtoa mada when will you die?
 
prof ana leukemia,gharama iliyotumika kumtibu appolo ilibidi JK aidhinishe ilikua kubwa mno!BOMBO hosp hakuna shuka
 
Kama raia wengine wa nchiin hii wasio na kipato wanakufaa kwa magonjwa kutokana na huduma mbovu za afya hapa nchini.Kwanini nao kama viongozi tena wenye kipato wasijitegemee kwa matibabu?

Tatizo letu tunaona uhai wa kiongozi una thamani kuliko wa mlala hoi.

Bila uwepo wa wananchi wa kawaida hawa vingozi wangekuwepo kwa ajili ya nani?

unfortunately natumia kimchina ningekugongea like kaka!kama raia na watawala kwa ujumla hatujajua ni kwa nini tu masikini, tembelea mahospitalini,kwenye zahanati,vituo vya afya,shule za kata hali ni mbaya so tukiendelea ku entertain mambo kama haya ni kujimaliza wenyewe,atafutwe mtu mwingine wa kushika nafasi yake huku yeye akiendelea kupata matibabu
 
Acha mbwembwe wewe! Hela anazotumia kwaajili ya matibabu zinafanana na zile za EPA? Deep Green, Rich Monduli, Rizi? Mbona unakuwa na roho mbaya? Fuatilia kwaza hizi pesa za waliokula acha kabisa kumshutumu Mzee Mwandosya.
 
arigold Muheshimiwa Mwandosya alimuomba MKUU ampuzishe kwasababu ya afya yake lakini mkuu alikataa na kumpa post hiyo kwahyo siyo kosa lake ni kosa MKUU
 
Last edited by a moderator:
Mpumbavu ni aliyejua anaumwa harafu anamwomba awe waziri, kwa uwezo wa mwandosya kiakili aliona akubali ili kumkejeli maana alimwonesha kejeli.

Hivi kweli hiyo ni mali na rasilimali za taifa au za mtu na familia yake??? CCM ingekuwa na viongozi wangeliona hiyo na kumwambia huyo dereva wao apige kona. Sasa CCM ni kina Nape, unategemea nini?, CCM ni Kina Kibonde na d 2 za kureseat, unafikiria nini kitafanyika???

Tuwakataeni kwa nguvu mwaka 2015.
 
Kuto kupitia PG na Masters kunakusaida nini? Lete hoja za msingi tukuelewe, mwandosya kutibiwa na serikali ni hali yake ya msingi. na wala hela anayotumia ni sehemu ndogo tu ya uchumi wetu watanzania. Kikubwa watu wawajibike na ufisadi usiwepo uone kama kuna mtu atafuatilia nani katibiwa wapi na kwa hela ya nani?
 
wwww ...Umuhimu wake kama kiongozi sio tu akili, but ana-deliver? Akili yake kama haina tija inatufaa nini? Acheni hizo sifa za kijinga banaa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom