maagizo yanatoka kwa wakuu wao wa kazi umesahau ya kamanda baro alivyomuambia yule afisa uhamiaji kuwa ana bahati, ukiingia kwenye anga zao wao ni risasi tu hawana Mswalie mtume !Nachelea kusema hili tatizo liko CCP, sipati jibu kuwa askari anaamriwa na boss wake kuwa nenda kwa fulani ukikutana naye piga risasi. Mathalani angefungua mlango mtu tofauti bado wangetwanga au wangeingia kupekua?
Pole sana mwandishi!
DSN,umeeleza vizuri kupoza hasira za Pasco na wengine,Lakini umeharibu kuleta siasa ktk suala la maisha mwanadamu.Unaposema wana ujuzi wa kufanya Investigation za kifisadi"wafanye na Journal Investigation una maana lifanyiwe kazi kisiasa?je mwandishi huyo angekuwa wa gazeti la uhuru ungesema hivyo?!!au kwa sababu ni mwandishi wa Tz daima?!!!.Think Twice"
This is getting serious guys...!!
JK nchi imemshinda for sure.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Shaban Matutu amepigwa risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu na kwenda kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo.
Baada ya kufunguliwa wakamfyatulia risasi na kisha wamesema suala hilo ni la bahati mbaya.
Hhivi sasa wamemchukua na wanampeleka hospitali ya Mwananyamala
Wanasema kirahisi kuwa walikuwa wanasaka majambazi, walitonywa kuna majambazi wakavamia nyumba ya Mwandishi eti katika kusukumana ndio bastola ikafyatuka risasi ikampata Mwandishi, polisi hawasemi majambazi yapo wapi waliyokuwa wanayasaka, hawakupita kwa mwenyekiti wa mtaa, walivamia nyumbani kwa mwandishi. wanasema Mwandishi alijilinda kwa panga akamjeruhi Askari, hawaonyeshi Askari huyo yuko wapi? amejeruhiwa vipi? Jamani Maswali kibao mimi nimechoshwa na Ujinga wa Polisi na Ujambazi wanaofanya.