Mwandishi APIGWA risasi na Polisi

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Shaban Matutu amepigwa risasi na Polisi, ambao wanadaiwa walikuwa wanamtafuta mhalifu na kwenda kugonga chumbani kwa Mwandishi huyo.

Baada ya kufunguliwa wakamfyatulia risasi na kisha wamesema suala hilo ni la bahati mbaya.

Hhivi sasa wamemchukua na wanampeleka hospitali ya Mwananyamala


attachment.php


attachment.php
 

gobore

JF-Expert Member
Aug 17, 2009
715
352
Duh! Kama ni kweli aisee wenye hii nchi mmekwisha! Mtu ananyukwa risasi hata kama hayuko armed? Halafu wanasema bahati mbaya kirahisi tu?

Source please mleta mada
 

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,640
6,066
Baadhi yetu tumefika hospitali. Tulikuwa na mmoja wa wana JF senior. Alinikuta pale. Alikuwepo mwandishi mwenzake na Shaban na mfanyakazi mwenzake mwingine. Kisha akaja mwandishi mwenzake mwingine na pia akafika Absalom Kibanda, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa TEF.

It is just another sad story kwa kweli kama wengine walivyokwisha kusema hapa. Waandishi tumeweza kuzungumza na mke wa Shaban, Mama Jay. Kitu ambacho hakiingii akilini eti polisi wa anti crime hawawezi hata ku spot exactly chumba cha mhalifu wanayemtafuta kwa mabunduki na mabastola, wanaanza kupita wanauliza uliza kwa wapangaji wenzake.

Wanaelekezwa mlango au chumba cha mtuhumiwa wanayemtafuta, Mama Jay. Bado wanakosea mlango, wanaenda kugonga kwa Mama Jay mwingine, bila tahadhari wala kujitambulisha wanaingia ndani wote kishari, kisha wanafyatua risasi kumuelekea Mama Jay (mke wa Shaban), ambaye ananusuriwa na kitendo kile cha wao kuingia kwa kasi kwa kupamia mlango kama wahalifu, anadondoka, risasi zinapigwa zinampata mwandishi wa habari, kama unavyoona kwenye picha, almanusura impate kwenye moyo. Fikiria nini yangekuwa matokeo yake. Risasi kupiga moyoni.

Kisha askari hao ambao tulitarajia wawe weledi hasa linapokuja suala la uhai wa mtu, wanaambiwa hapo si kwa Mama Jay mnayemtafuta, mbona tuliwaelekeza mlango ule pale. Kama hiyo haitoshi, askari mmoja akataka kuitoa ile risasi kwa Shaban kwa mikono. Kufuta ushahidi? Bahati nzuri Shaban aligoma, muda huu wangesharuka. Yangekuwa mambo ya kupigwa na vitu vizito. Imeshindikana.

Nane, maana hatujui filamu hii itageuzwa namna gani baadae hata kufikia tisa na kumi, wakati wanaondoka pale nyumbani kwa Shaban, akipelekwa hospitali, wakapishana na Mama Jay mtuhumiwa aliyekuwa anawindwa na hao anti crime police. Maana inasemekana wakati zogo likiendelea alikimbilia kibanda fulani mtaani hapo hapo. Wameoneshwa Mama Jay mliyekuwa mnamtafuta si huyo hapo, wala...hawakuwa na habari naye tena.

No body is safe. This is not an issue of somebody. Nchi inageuzwa pole pole, police state.
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
24,705
21,175
Jk si ameshawakataza kuua!!!?!i? Au bado hajawapa official letter
 

Tai Ngwilizi

JF-Expert Member
Apr 20, 2010
781
210
mwizi anatafutwa nyumbani kwa mwandishi wa habari.... polisi anampiga risasi anayefungua mlango...bahati mbaya...
utata mwingi hapo, maswali mengi kuliko majibu, naomba Mungu hii yote iwe ni uzushi tu kama hadithi za shigongo
 
  • Thanks
Reactions: Ame

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,652
Hata kama ni mwizi kweli,kwa nin apigwe risasi? Hii nchi police wanapaswa kulinda raia na mali zao..nashangaa how could this posibly happen atlist pangekua na majibizano sababu kisheria si sawa polisi kuadhibu,au kujeruhi na hata kuua kama mtu anaetaka kumtia kizuizin hana silaha! Naogopa sana tuombe hii taarifa isiwe ya kweli!
 

sanjo

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
943
271
Kama ni habari hii ni ya 'kweli basi jeshi la polisi halitaki kujifunza juu ya unyama waliomfanya marehemu Mwangosi. Shame on them.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom