- Thread starter
- #201
Huyu mwandishi alikuwa akifanya nini mpaka akapigwa risasi.tatizo la waandishi wetu ni limbukeni.panapokuwa na vurugu wao hukaa upande wa wanaofanya vurugu.hivi risasi ikipigwa ataachwa.haya ndio yaliyomkuta yule mwandishi iringa.na wengi wao wanashabikia vurugu.habu kuweni na utaratibu wa kukaa nyuma ya polisi ndipo ufanye coverage yako.ni waandishi wa bongo tuu ndio wanaopigwa risasi na polisi ukiona hivyo ujue tatizo si polisi bali ni waandishi wenyewe.
Swahiba huujui uandishi na hata tukio la kuuawa kwa Daudi Mwangosi, ndiyo maana unasema wanakuwa upande wa vurugu kwa kukusaidia tafuta gazeti la Tanzania Daima la septemba 9 utajua namna mwangosi alivyouawa na utajua kama alikuwa katika watu waliokuwa wanashambuliwa na polisi.
kuhusu huyu aliyepigwa risasi na Polisi huko Kunduchi ni kwamba alikuwa Chumbani kwake na mkewe na kwa ufupi ni kwamba askari walielekezwa kwa mtu aliyekuwa akihisiwa kuwauzia madawa ya kulevya vijana, walienda pale kwa lengo la kuchukua fedha na siyo kukamata. mitakupa sababu moja ya msingi kwamba waipewa taarifa mapema juu ya mtu huyo, wakajiandaa kwenda kuonana nae siyo kumkamata kwa kuwa hawakutoa taarifa kituoni kama wataenda kufanya kazi hiyo, na kwa kuwa mlengwa ni mwanamke kama wangetoa taarifa wangepewa askari mwanamke wa kwenda kufanya upekuzi kwa mtuhumiwa ili waweze kumfikisha mahakamani kwa ushahidi watakaoupata, hakuna utetezi hapo taarifa hazikuwa za ghafla juu ya yule wanayemhitaji hawakumshirikisha hata mwenyekiti wa mtaa wajumbe wa mtaa au hata shahidi mwqingine kwa sababu ya kutaka kulinda uhalifu wao usijulikane bahati mbaya kwao wakaingia katika chumba cha mwandishi aliyekuwa amelala na mkewe