Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,883
Anaandika Robert Heriel.
Haijalishi atakuambia nini, haijalishi atakupa nini. Mwanaume hawezi kukupenda Kama anavyompenda mkewe.
Hilo wala sio siri, wanaume wote duniani tupo hivyo.
Asije akakudanganya mtu kuwa ati anakupenda kuliko mkewe huo ni uongo na amekuona hamnazo kichwa maji.
Ndio maana wanawake wote wenye akili ndoa kwao ni moja ya kipimo kikubwa cha upendo kwa mwanaume.
Elewa kuwa mpaka mwanaume anakuacha wewe anaoa mwanamke mwingine mbele ya macho yako jua hakupendi.
Hii ni tofauti na wanawake, mwanamke anaweza kuolewa na mwanaume asiyempenda. Lakini kwa mwanaume hilo haliwezekaniki na kama litawezekanika labda kwa masharti ya mganga.
Ukitaka ujue kuwa hupendwi zaidi ya mkewe, ukitaka kuhatarisha ndoa ya mwanaume yeyote hapo ndipo utaonja joto ya jiwe. Na ndio mwanzo wa kupigwa chini.
Ili mwanaume akujali sana kuliko anavyomjali mkewe basi itampasa mkewe awe hafanyi wajibu wake kama mke, awe na kisirani, hajui mahaba, hajui kutumia mdomo wake vizuri, hana manjonjo n.k. Lakini kama anatimiza wajibu wake nakuhakikishia atakuweka katika wakati mgumu kupasua ngome yake.
Kamwe usijilinganishe na mke aliyeolewa, hiyo ni dalili haujitambui. Ni sawa na mgeni kutoka nchi za ughaibuni kujilinganisha na raia wa nchi.
Ndio maana wanawake washenzi wanapoingilia ndoa za watu, huenda kwa waganga wa kienyeji au walozi kisha humloga mke ili apandishe kisirani cha ndoa ili asimpe mumewe utulivu. Hilo likifanikiwa basi mwanamke wa nje hupata nafasi ya kujivinjari na mwanaume.
Wengine huwatupia majini ya ugomvi, maradhi, uvivu, uchafu basi ilimradi kudhoofisha ngome.
Pamoja na yote hayo mke ni mke na hawara ni hawara.
Wanawake wengi wanalijua hilo ndio maana hufanya juu chini kuachanisha ndoa za watu alafu wao ndio waingie washike hatamu ndoani ili kujimilikisha Kabisa.
Wanajua mapenzi bila ndoa hayana guarantee. Muda wowote unapigwa chini na hauna haki yoyote.
Wanawake kiasili hawapendi ukiwa naye kwenye mahusiano mfanye Kwa kujifichaficha, wanaona kuwa huo sio upendo.
Ndio maana ukitoka na mwanamke hapo mtaani sio ajabu huyo mwanamke akawa anajipitisha kwa mkeo na kumfanyia visa mpaka ajue kuwa ni mke mwenza.
Wanawake hawawezagi mapenzi ya siri.
Na kamwe mwanamke asije akakuambia kuwa mapenzi yenu yatakuwa ya siri. Hakunaga kitu Kama hicho kwa hawa dada zetu. Siku zote wanaendeshwa na hisia.
Usiku mwema!
Robert Heriel,
Taikon wa fasihi,
Kwa sasa Kibaha.