Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,035
Ukiona hivi ujue kuna wambea wamemtonya werema kuwa soon kikwete amepanga kutangaza kuwafuta nafasi zao
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Na rais amekubali na amesema. Werema amechafua hali ya hewa.........
wanazuoni si wataandamana ili atengue uamuzi!!!
Mimi nimeshasema. Kikwete anazidi kuunda matatizo makubwa zaidi kwa taifa. Eti anamsifia kwamb utumishi wake uliongozwa na uaminifu sijui na uadilifu. Inahitaji ujasiri wa kifisadi kutamka maneno haya hadharani bila hay akwa mhusika wa kashifa iliyo dhahiri.
Asije kumpa kazi nyingine ama kumfanya balozi kwa sababu anazidi kuhatarisha usalama wa nchi. Hawezi kuimarisha mtandao wa majizi kana kwamba nchi hii ni yake. Ninaamini maneno yaliyozagaa kwamba Accounts za escrow, zilizokuwa Stanbic, ni za kikwete, mkewe na familia yao ndiyo maana anaishia kujiuma uma na kufanya unafiki ili kuwapoza mafisadi wenzake, wasimuumbue. They are team mates!.
Tunahitaji watu wote waliohusika kwa kashifa ya escrow wawajibishwa kisheria na warudishe fedha zote. Hadith za kijinga n kuwafaya watanzania wote ni wajinga hazikubaliki.
Tulijua nia ya kikwete na lowasa kwenda ikulu haikuwa kuwatumikia wananchi. Ilikuwa ni kukidhi tamaa zao za anasa na mtamanio binafsi lakini hatukujua zitakuwa na syndicate ya wizi mkubwa kiasi hiki. Kikwete ni mwizi na ni kiongozi mkuu wa mafisadi. Anastahili kuwajibishwa kwa kushindwa kazi na kuhujumu uchumi wa nchi huku akijenga misingi ya machafuko nchini.
Pesa zilikuwa BOT aliyesema zitoke zilipwe ni Werema na sasa kaachia ngazi, Mhongo akitoka lazima Gavana,Waziri wa Fedha,Waziri wa Viwanda na Biashara nao wang'oke kwani walifanya kazi sambamba iweje Mhongo ashinikizwe peke yake? Kisa ana Ugonvi na Mengi juu ya Udalali wa Vitalu vya Gesi, huku Mkono akiwa na Uchungu wa kunyang'anywa kazi zote za kisheria Wizara ya Nishati, Mhongo ni Shinikizo Binafsi la Mengi na Mkono kwa Manufaa yao, Tunaomba Kafulila na Zito nao wajiuzulu kwa kuwa walipewa pesa na Mengi ili wapaze sauti kwa Manufaa ya kuwafurahisha kisha kuwaaminisha wananchi ili wawaonee huruma mengi na mkono ambao pia si walipaji kodi ipasavyo, wao pia wakichunguzwa na FBI wana Madhambi lukuki, Nchi hii hakuna aliye Msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole, Watumishi wengi wa Umma wanaishi Kinyume na Vipato vyao Harisi, wakiletwa FBI hapa wawachunguze wote wenye Mali hakuna ambaye atapona.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
ITV hii hii ya Tanzania au? Utakua umeangalia ITV ya Uingereza lakini hii ya Mengi hii habari ndiyo ilikua ya kwanza.Hivi karibu kumekuwa na watu wanazusha taarifa za uwongo. Neangalia ITV mwanzo mpaka
Mwisho sijasikia taarifa ya TATAA MURA kujiuzuru. Naomba ufafanuzi wadau!
Ajihudhuru = Ajihuzulu