Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,035
Haya sasa wale wanazuoni wa dodoma watoe tamko la kupinga werema kujiuzulu.
Jaji Frederick Werema kajiuzulu na JK amekuli.
Source. Channel ten na ITV
Haya sasa wale wanazuoni wa dodoma watoe tamko la kupinga werema kujiuzulu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Wahisani wanataka kuona hatua stahiki zinachukuliwa dhidi ya wahusika....sasa mtu kajiuzuru kwa hiari yake hyo sivyo tutakavyo...afikishwe mahakamani akajibu tuhuma za kusababisha upotevu wa mabilion ya pesa za umma...
Hapo ndiyo mujue rais anawaelewa vizuri wezi wa ESCROW, "ulioongozwa na uaminifu na uadilifu" hizi ni porojo, mwizi na tumbili amekuwaje mwadilifu au ni kinyume chake yaani ufisadi,ila ukiwa fisadi ccm wanakukumbatia.Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Ajihudhuru = Ajihuzulu
Ni Aibu kwa serikali hii kukaa na wahujumu uchumi hadi wanapata nafasi ya kujihudhuru!.Kwani mpaka wao wanajibaini kuwa walifanya makosa! na serikali yenye madaraka kamili, inakaa kimya???.
Kweli hii mnatutendea haki wananchi!? Inamaana hamtaki kuwawajibisha kwasababu gani ya msingi?Ukiangalia walio jiudhuru kwa kashifa ya kukwapua mali za umma ni wengi na hakuna yeyote aliye chukuliwa hatua yoyote!. Hila kama kungekuwa na mtu aliyewajibishwa kwa ufujaji wa mali ya umma, nidhahiri watu wangeogopa, ndiyo maana watendaji wa serikali wanaweza kuchukua rushwa kubwa wakijua anaweza akajiudhuru na ikawa poa!. Sasa wabunge pelekeni mswaada bungeni kwa yeyeote atakayepatika na hatia ya kukwapua mali ya Umma akae maabusu kwa miaka 3 then ndiyo kesi yake itajwe na asiwe na dhamana.
Hakuniconvince katika UDPP wake....he is not BOLD