Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

kwa kosa gani? amewajibika kisiasa kisheria atawabwaga kwa sababu ukipewa ushauri kama ni mbaya siyo lazima uutumie

Anajiuzuru kwa kosa gani? Kwani siasa inaongozwa bila sheria? Akinani wanaotunga sheria? Kwann mnatetea upuzi
 
Hapa kuna mchezo tu unachezwa kulinda wahalifu wengi..Yaana jamaa bado hawajajifunza. Prof anatakiwa kuwa makini kwenye hili coz watu bado tunaconnect dot and finally we will arrive into a conclusion. Ukijaribu kuangalia kwa umakini inawezekana jamaa ameombwa sana mpaka akakubali kuachia ngazi, sasa wale wenye vichwa ngumu kama Muhongo na Maswi dont expect kama watakubali kirahisi.. tusubirie episodi nyingine ya hii movie
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Uaminifu na uadilifu Duh!! Ama kweli Kambale wote (Wakubwa, watoto, Majike, Madume, vilema) wana ndevu!!
 
Upo uwezekano ni maelekezo na mbinu za kisiasa kwa kuwa siku chache zilizopita kuna mtu alitoa taarifa kuwa Werema alistaafu tangu Nove. 30, 2014, huenda ikawa kwa sasa kilichofanyika ni kustaafu na siyo kujiuzulu. Kibaya zaidi ni kuwa tayari amekiri mwenyewe kuwa ushauri wake umeleta madhara/ hasara kubwa kwa Taifa, je tunahitaji kuendelea kufanya uchunguzi badala ya kumuunganisha na akina Yona, Mgonja na wengine ambao wanaendelea na kesi zao kwa makosa kama hayo hayo? bila kufanya hivyo sidhani kama dhambi hii ya ubabe wa madaraka kwa viongozi wetu itaisha, ndiyo mana wamekuwa na viburi badala ya kujenga nchi na kutumikia wananchi.
Hiyo bila shaka atakuwa ametekeleza maelekezo aliyopewa na JK.
 
Kauli hii haiendani na mtu aliyejiuzulu. Kwa maana nyingin Mkuu hajatambua kuwa Werema amejiuzulu bali amefikisha umri wa kustaafu na amestaafu kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.
Uaminifu na uadilifu Duh!! Ama kweli Kambale wote (Wakubwa, watoto, Majike, Madume, vilema) wana ndevu!!
 
Huo ni mchezo wa kuwatakasa wenzake...na alilijua hilo ndo maana bungeni aliwaambia wabunge wahangaike na yeye...hamuoni hapo kuna deal inafanyika la kurescue wengine.

Nami naona hivyo, lakini namhurumia Pinda atatoa feedback gani bungeni mkutano ujao hasa ukizingatia makundi ya urais
 
Mtazamo...!!!! Sina shaka na kujiuzulu kwa mwanasheria mkuu. Shaka langu ni nini kitatokea baada ya kujiuzulu. Na pia kama na wengine watafuata kujiuzulu...!!! Lakini zaidi isijekuwa kama Mhe..!!wa Monduli alivyojiuzulu peke yake..!!!!
 
Jamaa anamshukuru AG kwakulingiza taifa katika wakati mgumu kuna mambo mengine yanaboa sana au anashukuru kwa kufanikisha hazma yao.taifa lipo katika wakati mgumu bado rais anawachekea inaumiza sana wadau lazima hatua zichukuliwe hili awatende haki wanaokufa kwa kukosa madawa hospital na mipesa yao account ya escrow.
 
Huyu si ndo alimwita mwenzake tumbili?? Kweli usitukane mamba kabla hujavuka mto.
 
Kuna kijana wangu nyumbani hivi karibuni amekuja na mkanda wa sinema na kunitazamisha. Ni wa kichina.Kwa Wachina nimezoea kuangalia mikanda ya sinema ya Bruce Lee,Jackie Chan, Donnie Yen, Choo Young Fat na wengineo maarufu. Mkanda aliouleta kijana wangu nyumbani uko tofauti.Simjui hata staa/steringi wa sinema ile.

Unaitwa Shaolin Soccer. Kijana wangu akanishawishi kuuangalia huku akiusifu kuwa uko poa na wa kupigiwa mfano. Alinitabiria kuwa kizungumkuti cha Shaolin Soccer kitatokea kwenye sakata la Escrow.Nikambishia kwa ukali na kumsimanga. Sasa nayaona.

Kwenye sinema hiyo, ingawa simjui steringi, kuna pambano la mpira wa miguu la ajabu sana. Wachezaji huruka huku na kule hewani wakiwa wanalisakata kandanda. Kusakatwa huko kwa kandanda hewani kunachagizwa na wachezaji kupeana mapigo matakatifu ya kung fu hadi kupelekea wachezaji kufa au kujeruhiwa. Kiukweli,pambano hilo la kandanda halieleweki.

Lakinikijana wangu mda wote wa sinema alikuwa akishangilia ingawa kichina na hata kiingereza hakipandi. Kutoeleweka kwa kandanda la Shaolin Soccer ndiyo hasa burudani yake. Akathubutu kulihusisha na hata kulifanaisha kandanda hilo na sakata la Escrow liiloanzia Bungeni na kuendelea hadi sasa uraiani. Shaolin Soccer.

Jana,zilipotolewa aarifaza kuiuzu kwa AG Werema,kijana wangu huyo akanitumia ujumbe mfupi wa maandishi simuni mwangu: "Mzee, Shaolin Soccer imeanza rasmi. Jaji Werema ameianzisha". Nilipomuuliza ajieleze vyema akadai kuwa pambano la Escrow halitaeleweka lakini wapo watakaoathiriwa. Maazimio hayataonekana kufuatwa lakini wananchi watadhia.

Escrow Soccer imeanzishwa na Jaji Werema!


Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom