Mwanangu Kim Jong Un

Mwanangu Kim Jong Un

Tukiwa bado tunaendelea na uchambuzi wa kitisho au kinachoendelea eneo la Asia Pacific kwa US kuivamia kijeshi Korea kaskazini tulisha zungumzia kitisho cha kiuchumi ambapo eneo la Pacific kwa mwaka kuna GDP ya$ 17.1566 Tillion na purchasing power ya 16 ambapo ndio number one ktk wanunuzi wakubwa wa bidhaa kutoka Ulaya na America na kuwa eneo muhimu kibiashara na Uchumi dunia

Leo tutakijita kwenye maswala ya kijeshi baada ya kuona kiuchumi katika uwanja wa mapambano kuna vitengo vitatu ambayo ndio engine ya kushinda vita au kushindwa vitu hvyo ni
1 Intelligence ( ujasusi wa kupata taarifa za kijeshi na Usalama wa adui wako
2Comminication (Mawasilino ndani ya uwanja wa mapambano)
3 Supplying ( Usambazaji wa vifaa,silaha au huduma ndani ya uwanja wa mapambano)

Hivyo ndivyo vitengo vitatu muhimu ndani ya uwanja wa mapambano lakini leo tutakijita kwenye kitengo cha mawasilino duniani kuna aina 5 za mawasilino
1. Optical Communication System
ambayo inabeba mitandao ya kijamii kama JF ,whats app,Facebook,snapchat
2. Radio Communication System
ambayo inabeba mawasiliano ya radio (simu za upepo) na simu za Satellite Phones
3. Duplex communications system
ambayo inabeba mawasiliano ya Telephone,
Mobile, Telegraph ,Fax mfumo huu unakuwa na kitu kinachoitwa Defense Communications System (DCS)
4. Half Duplex Communication System
mfumo huu unadeal na data , na video communication mara nying unatumiwa na watumiaji wa simu za mikononi
5. Tactical Communication System
mfumo huu mara nying unatumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwani unakitu kinachoitwa Voice Communication Control System (VCCS) ambayo unafanya mawasiliano yanakuwa guided

Sasa leo tujikite kwenye Tactical communication systems ambayo vyombo vya Ulinzi na kijeshi wanatumia kutokana na technology ilivyokuwa inaongezeka vifaa vingi sana vya kijeshi vinatumia software au OS (Operating system)
na Duniani kuna OS 3 ambazo ndizo zinarun mfumo mzima wa mawasilino ya computer japo si 100% mifumo hyo ni
1Microsoft windows 83.3%
2MacOS 11.2%
3Linux 1.55%
So ukimpiga jumla unakuta ni 96.05% ndio maana ni kasema si 100%

Uwanja wa mapambano unategemea sana mawasiliano ktk Ops za kushambulia target na vifaa vingi sana vya kijeshi vinatumia software yani kitengo cha mawasilino kipo busy kuliko vitengo vingine vyote threat pekee ni hackers kwa taarifa zilizopo jeshi la korea kaskazini wana kikosi cha kijeshi ambacho ni cyber special force ambacho kazi yao ni kuhack system mbalimbali za kijeshi na mawasiliano ya kijeshi na Usalama pia duniani korea kaskazini ndio nchi pekee yenye Operating system yake yenyewe kule hakuna Microsoft Windows ,MacOS au Linux so kwenye upende wa wao kuwa hacked ni ngumu sana

USA kuna tatizo sana kwenye upande wa NSA ambao kazi yao ni kuhakikisha na kudeal na Cyber threat kwani kumekuwa na matukio ya mashambulizi ya system zaa au mifumo yao na mahackers kutoka Russia , China na Korea kaskazini mifano ni

1 Mwaka 2015 Russian hackers walivamia State Department email system kwa kile kilichojulikana kama “worst ever” cyberattack against a federal agency.
2 Mwaka 2015 Ofisi ya menejimenti ya utumishi wa umma walireport kwa NSA kupotea kwa Americans’ fingerprints milion 5.6 za watumishi wa umma katika kile kilichojulikana kama ilikuwa ni cyberattack.
3 Government Accountability Office (GAO) wamereport kwa NSA kuwa kuanzia mwaka 2015 namba ya mashambulizi ya kimtandao yalipanda kwa 64% kutoka mashambulizi kutoka 5,500 mpaka zaidi ya 77,000 kwa mwaka ni 24 federal agences zilivamiwa
4 Machi mwaka jana hackers wa kutoka China waliendelea kufanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya serikali ya Marekani na mitandao binafsi, kwa mujibu wa U.S.mkuu wa Cyber Command Mike Rogers. China imekuwa ina husishwa na mashirika ya upelelezi ya U.S. kwa kufanya mashambulizi kwa lengo la kuiba taarifa na kuchora ramani katika mitandao muhimu ya kompyuta kwa ajili ya mashambulizi ya baadaye katika mgogoro au vita.

Yapo mengi ya kujadili lakini naomba niishie hapo lakini hii ni moja ya changamoto ktk vita hii ambayo Trump anataka kuanzisha je US wamejiandaa kupigana na jeshi hili la ofisini na silaha zao ni computer tu lakini silaha hizo zenye uwezo wa kulipua mabomu na mifumo yenu palepale US yani silaha zenu zikatumika kuwapiga nyinyi.
Umenifungua sana mkuu
 
Hafanani na Gadafi wala Saddam sababu hao wawili walikuwa na plenty internal enemies and snitches walioshirikiana na mercenaries.

North Korea wapo pamoja zaidi
 
Huyo dogo kinachombeba wanaona bado mdogo akili zake bado hazijakua anachukulia mambo kitoto toto....wanamngoja afike angalao aged 45 akiishajua madhara ya vita ndio wamsugue kweli, kwa akili zake anadhani kutumia nuclear bomb ni rahisi huku hajiulizi kitakachoipata nchi yake kutoka kwa mataifa shirika ya taifa atakaloshambulia maana hawatokaa kimya lazima watamshambulia.
 
Pigeni porojo, lakini hakuna taifa lingine lenye nguvu litalokuja zaidi ya marekani.
Dogo atachapwa tu. Haijalishi atachapwaje.
Tusiende mbali nenda Somalia kaulize ilikuaje USA akakimbia utajua palivomtoa jasho halafu nenda Vietnam kaangalie alivoshindwa then rudi kwa jirani yake Cuba angalia anavoitafuta amani baada ya kushindwa then utajua USA sio kila kitu anaweza!..
 
Mimi sina fact maana sipo pentagon wala piyong yang, sipendi kufanya hisia zangu ziwe fact.
Achana nao Hao wanadownload na kupost mladi hisia zao ziaminike hakuna anae jua hata Obama saiv hajuw Trump anawaza Nin kuhusu NK lakn miwatu inajaza factless thread JF
 
Mimi sina fact maana sipo pentagon wala piyong yang, sipendi kufanya hisia zangu ziwe fact.
Hahahaha hujui kwamba hata hisia vilevile huweza zikatengeneza facts na zikawa za ukweli tu na pia zisiwe za ukweli
 
Nchi yako imewekewa vikwazo vizito tangu enzi lakini bado mnazidi kupiga hatua katika technology ya silaha na mitambo ya kivita, hali inayowafanya kuzidi kuwa mashujaa na kuonyesha ulimwengu kuwa hamyumbishwi.

US anatengeneza nuclear lakini hataki mwengine afanye hivyo, mwanangu umeamua kutengeneza na kujaribu zana zako mpya na sasa unakaribia kushambuliwaTayari chombo cha US kipo karibu na nchi yako kikiwa na wanajeshi na zana za kisasa wakisubiri amri ya Rais wao tu kushambuliaHii imekupa hasira na ukasema mkianzwa mtatumia kila silaha yenu kushambulia, ni wazi jambo hili limekuudhiumeshaanza kuwaondoa wananchi mji mkuu ili kuwapa nafasi makomando kufanya vitu vyao pale mambo yakianza.

Najua mwanangu upo vizuri ki vitalakini nakukumbusha kumbuka ya Gaddafca ni taifa kubwa duniani lakini usife moyo huenda ukawa imara kama ilivyokuwa kwa Vietnam.

Najua wewe ni imara maana unatengeneza mwenyewe silaha tofauti na Saddam na Gaddafi, wewe ni imara pamoja na kutengwa.

Pigania mipaka yako mwanangu nipo pamoja

Mkumbushe pia US alivyotandikwa Vietnam, usisahau kumkumbusha US alivyoaibishwa Somalia mpaka Askari wake wakaliwa maini live na kuburuzwa mitaani mpaka wakakimbia na kuondoa majeshi yao Somalia.

Mkumbushe pia kichapo wanachokula miaka zaidi kumi huko Afghanistan mpaka wameamua juzi kupiga kombora kubwa sana ambalo halijawahi kutumiwa popote kushambulia majabali.

Wamechanganyikiwa wanapigana na hewa.
 
Hahahaha hujui kwamba hata hisia vilevile huweza zikatengeneza facts na zikawa za ukweli tu na pia zisiwe za ukweli
Hapana hizo hazitaiwa fact, il mitizamo tu.shart la fact iwe ni ukweli wenyewe kwa kuona ama kushika kabisa.
 
Mkumbushe pia US alivyotandikwa Vietnam, usisahau kumkumbusha US alivyoaibishwa Somalia mpaka Askari wake wakaliwa maini live na kuburuzwa mitaani mpaka wakakimbia na kuondoa majeshi Yao Somalia.
Maandiko na habari njema kama hizi kuna watu hawataki kuziona au kuzisikia. Naamini safari hii watalazimishwa kuelewa. Acha waendeleze chokochoko maana NK haijaficha azma yake ya kujibu kwa nguvu kubwa.
 
Back
Top Bottom