Mwanangu Kim Jong Un

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,484
12,097
Nchi yako imewekewa vikwazo vizito tangu enzi lakini bado mnazidi kupiga hatua katika technology ya silaha na mitambo ya kivita, hali inayowafanya kuzidi kuwa mashujaa na kuonyesha ulimwengu kuwa hamyumbishwi.

US anatengeneza nuclear lakini hataki mwengine afanye hivyo, mwanangu umeamua kutengeneza na kujaribu zana zako mpya na sasa unakaribia kushambuliwa
09199863556a3c131425df0a8711105e.jpg
Tayari chombo cha US kipo karibu na nchi yako kikiwa na wanajeshi na zana za kisasa wakisubiri amri ya Rais wao tu kushambulia
3af74b6375ae1bbcf751bf3a1e83d302.jpg
Hii imekupa hasira na ukasema mkianzwa mtatumia kila silaha yenu kushambulia, ni wazi jambo hili limekuudhi
329878849e808781c9bd44ad802b1128.jpg
Umeshaanza kuwaondoa wananchi mji mkuu ili kuwapa nafasi makomando kufanya vitu vyao pale mambo yakianza.

Najua mwanangu upo vizuri ki vita
0abf37f4d31373269786dc478af99171.jpg
3393193b44f355083f4e4cb86ac14884.jpg
lakini nakukumbusha kumbuka ya Gaddafi
b3e8feea60bad51ea204baf4e488d83f.jpg
na usisahau ya Saddam
d68601faf6e00ea217b4d5088b181937.jpg
America ni taifa kubwa duniani lakini usife moyo huenda ukawa imara kama ilivyokuwa kwa Vietnam.

Najua wewe ni imara maana unatengeneza mwenyewe silaha tofauti na Saddam na Gaddafi, wewe ni imara pamoja na kutengwa, lakini pia wewe si damu ya kiarabu kama wao.

Pigania mipaka yako mwanangu...wewe ni tishio sana kwa Dunia ya sasa kote unaogopeka hivyo usirudi nyuma kwani itakuteteresha jumla...mwanangu nipo pamoja nawe
1d18f660f51014d5d45bddb96d0ff224.jpg
 
Unakosea sana kumfananisha Kim na kina Saddam na Gadaffi hao wote walikuwa wananunua silaha kutoka kwa watengenezaji. N. Korea anajitegemea kwa kila kitu na hana cha kupoteza kumbuka alishatengwa na dunia zaidi ya nusu karne halafu hao na wakorea siyo wanafiki kama waarabu
 
Unafanya kosa kubwa kumlinganisha Gadafi, Sadamu Huseini &Co. na Mkorea, hao akina Sadamu ni Waarabu kama sisi Waafrika ingawaje wametuzidi kidogo ambao wana low intelligence, Wakorea ni kundi moja na Wachina, Wajapani, &Co. ni mbegu nyingine kabisa na Mzungu analijua hilo, Wakorea wanaongoza kwa high IQ Duniani hivyo kuwa mwangalifu kidogo hapo kwenye ulinganisho, kumbuka Sadamu Huseini alikutwa na chocolate za mars pmj na hollywood movies made in USA kwenye handaki lake, hata Gadafi pia alikua kutwa nzima yuko na Wazungu mpka walivyo mchenjia, lkn Mkorea (Kaskazini) mpaka operating system ya computer ni ya kwao yaani na siyo ya Mzungu hiyo ni tofauti kubwa sana!

Vifaa vyote vya akina Sadamu Huseini, Gadafi &Co. vilikuwa vinatoka kwa Mzungu hata Ikulu ya Gadafi Mzungu alijenga lkn Korea hakuna kitu kama hicho, is the most secretive country in the world unaambiwa yaani hakuna anayejua kinachoendelea Korea, hivyo usisahau hilo na ninakuhakikishia kamwe Mzungu hawezi kuipiga Bomu Korea hilo halitatokea kwa maana Mkorea ana high IQ!
Baba yake alipokufa ilichukua siku Tatu duniani kujua tena baada ya wao kutoa taarifa
 
Vita siku zote huwa na pande mbili na majibu sahihi huja mara baada ya vita kuisha.....najua Kim ataisumbua US ila mwisho wake atapigwa tu.....SHABIKIENI KIDUKU ILA ISIJE BAADAE MKAMLAUM MMAREKANI KUWA AMEKOSEA KULIANGAMIZA TAIFA HILO.
 
Unafanya kosa kubwa kumlinganisha Gadafi, Sadamu Huseini &Co. na Mkorea, hao akina Sadamu ni Waarabu kama sisi Waafrika ingawaje wametuzidi kidogo ambao wana low intelligence, Wakorea ni kundi moja na Wachina, Wajapani, &Co. ni mbegu nyingine kabisa na Mzungu analijua hilo, Wakorea wanaongoza kwa high IQ Duniani hivyo kuwa mwangalifu kidogo hapo kwenye ulinganisho, kumbuka Sadamu Huseini alikutwa na chocolate za mars pmj na hollywood movies made in USA kwenye handaki lake, hata Gadafi pia alikua kutwa nzima yuko na Wazungu mpka walivyo mchenjia, lkn Mkorea (Kaskazini) mpaka operating system ya computer ni ya kwao yaani hatumii microsoft windows au sijui linux bali wana ya kwao wao wenyewe wameunda na siyo ya Mzungu hiyo ni tofauti kubwa sana!

Vifaa vyote vya akina Sadamu Huseini, Gadafi &Co. vilikuwa vinatoka kwa Mzungu hata Ikulu ya Gadafi Mzungu alijenga lkn Korea hakuna kitu kama hicho, Korea is the most secretive country in the world unaambiwa yaani hakuna anayejua kinachoendelea Korea, na isitoshe fikiria tu hakuna nchi inayoruhusiwa kufanya Biashara na Korea lkn angalia mambo wanayoyafanya, linganisha na Zimbabwe, hivyo usisahau hilo na ninakuhakikishia kamwe Mzungu hawezi kuipiga Bomu Korea hilo halitatokea, kwa maana Mkorea ana high IQ!
Wasaidie, maana humu wajinga ni wengi!
Wanalinganisha vita ya tumia akili na vita za kutumia nguvu na fedha kama za akina Gaddafi, Saddam nk
Very stupid!
 
Tukiwa bado tunaendelea na uchambuzi wa kitisho au kinachoendelea eneo la Asia Pacific kwa US kuivamia kijeshi Korea kaskazini tulisha zungumzia kitisho cha kiuchumi ambapo eneo la Pacific kwa mwaka kuna GDP ya$ 17.1566 Tillion na purchasing power ya 16 ambapo ndio number one ktk wanunuzi wakubwa wa bidhaa kutoka Ulaya na America na kuwa eneo muhimu kibiashara na Uchumi dunia

Leo tutakijita kwenye maswala ya kijeshi baada ya kuona kiuchumi katika uwanja wa mapambano kuna vitengo vitatu ambayo ndio engine ya kushinda vita au kushindwa vitu hvyo ni
1 Intelligence ( ujasusi wa kupata taarifa za kijeshi na Usalama wa adui wako
2Comminication (Mawasilino ndani ya uwanja wa mapambano)
3 Supplying ( Usambazaji wa vifaa,silaha au huduma ndani ya uwanja wa mapambano)

Hivyo ndivyo vitengo vitatu muhimu ndani ya uwanja wa mapambano lakini leo tutakijita kwenye kitengo cha mawasilino duniani kuna aina 5 za mawasilino
1. Optical Communication System
ambayo inabeba mitandao ya kijamii kama JF ,whats app,Facebook,snapchat
2. Radio Communication System
ambayo inabeba mawasiliano ya radio (simu za upepo) na simu za Satellite Phones
3. Duplex communications system
ambayo inabeba mawasiliano ya Telephone,
Mobile, Telegraph ,Fax mfumo huu unakuwa na kitu kinachoitwa Defense Communications System (DCS)
4. Half Duplex Communication System
mfumo huu unadeal na data , na video communication mara nying unatumiwa na watumiaji wa simu za mikononi
5. Tactical Communication System
mfumo huu mara nying unatumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwani unakitu kinachoitwa Voice Communication Control System (VCCS) ambayo unafanya mawasiliano yanakuwa guided

Sasa leo tujikite kwenye Tactical communication systems ambayo vyombo vya Ulinzi na kijeshi wanatumia kutokana na technology ilivyokuwa inaongezeka vifaa vingi sana vya kijeshi vinatumia software au OS (Operating system)
na Duniani kuna OS 3 ambazo ndizo zinarun mfumo mzima wa mawasilino ya computer japo si 100% mifumo hyo ni
1Microsoft windows 83.3%
2MacOS 11.2%
3Linux 1.55%
So ukimpiga jumla unakuta ni 96.05% ndio maana ni kasema si 100%

Uwanja wa mapambano unategemea sana mawasiliano ktk Ops za kushambulia target na vifaa vingi sana vya kijeshi vinatumia software yani kitengo cha mawasilino kipo busy kuliko vitengo vingine vyote threat pekee ni hackers kwa taarifa zilizopo jeshi la korea kaskazini wana kikosi cha kijeshi ambacho ni cyber special force ambacho kazi yao ni kuhack system mbalimbali za kijeshi na mawasiliano ya kijeshi na Usalama pia duniani korea kaskazini ndio nchi pekee yenye Operating system yake yenyewe kule hakuna Microsoft Windows ,MacOS au Linux so kwenye upende wa wao kuwa hacked ni ngumu sana

USA kuna tatizo sana kwenye upande wa NSA ambao kazi yao ni kuhakikisha na kudeal na Cyber threat kwani kumekuwa na matukio ya mashambulizi ya system zaa au mifumo yao na mahackers kutoka Russia , China na Korea kaskazini mifano ni

1 Mwaka 2015 Russian hackers walivamia State Department email system kwa kile kilichojulikana kama “worst ever” cyberattack against a federal agency.
2 Mwaka 2015 Ofisi ya menejimenti ya utumishi wa umma walireport kwa NSA kupotea kwa Americans’ fingerprints milion 5.6 za watumishi wa umma katika kile kilichojulikana kama ilikuwa ni cyberattack.
3 Government Accountability Office (GAO) wamereport kwa NSA kuwa kuanzia mwaka 2015 namba ya mashambulizi ya kimtandao yalipanda kwa 64% kutoka mashambulizi kutoka 5,500 mpaka zaidi ya 77,000 kwa mwaka ni 24 federal agences zilivamiwa
4 Machi mwaka jana hackers wa kutoka China waliendelea kufanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya serikali ya Marekani na mitandao binafsi, kwa mujibu wa U.S.mkuu wa Cyber Command Mike Rogers. China imekuwa ina husishwa na mashirika ya upelelezi ya U.S. kwa kufanya mashambulizi kwa lengo la kuiba taarifa na kuchora ramani katika mitandao muhimu ya kompyuta kwa ajili ya mashambulizi ya baadaye katika mgogoro au vita.

Yapo mengi ya kujadili lakini naomba niishie hapo lakini hii ni moja ya changamoto ktk vita hii ambayo Trump anataka kuanzisha je US wamejiandaa kupigana na jeshi hili la ofisini na silaha zao ni computer tu lakini silaha hizo zenye uwezo wa kulipua mabomu na mifumo yenu palepale Washington DC commands zikitoka Pyongyang kumbuka US anazo silaha za nuclear ambazo nying zinaongozwa kwa mifumo ya computer pia umeme na nishati ya kuendesha mitambo ni computerised je jeshi hili ambalo ni hatari kwa kuhack system mbalimbali za kijeshi na Usalama awawezi kugeuza DC na US kuwa gizani nishati hakuna na je Trump anao watu wa kufanya na kujilinda yakitokea mashambulizi hayo ya mifumo ya kiulinzi na mitambo maana naona National Security Agency (NSA) kama bado kuna tatizo kwani kama uchaguzi tu wahuni wamehack je itakuwa mitandao power systems zinazorun system za nuclear?

Tukipata muda tutakuja kuangalia kitengo cha intelligence kitengo number moja ktk uwanja wa mapambano
 
Back
Top Bottom