''Mwanangu, babako amekufa''

''Mwanangu, babako amekufa''

Lakini hata kama wewe ni mama hukupaswa kuyasema hayo. Nadhani ungeweza kuwa mwalimu bora kwake kwa kumuonyesha njia ambazo zingemsaidia kuliko kunena kitu kama kile. Wataka unambie hujawahi kukumbwa na suala kama hili na ukaomba msaada? Je ulijibiwa kama ulivyojibu hapa? huyu ni mgeni katika uzazi anahitaji kutiwa moyo na wazoefu kama nyie... ''""ULIBEBA MIMBA UKITEGEMEA UTACHUMA MALI sio kaulo nzuri kwa mtu unayejinasibu kuwepo katika ndoa kwa miongo miwili
wewe nadhan ni miongoni mwa watu wagen wa kauliz angu haapa jf
narudia tena kauli ya mleta mada kwamba " ALIZAA AKIDHANI NDO CHANCE YA KUPATA FEDHA KWA HUYU MZAZI MWENZIE" imenikera sana.
abadili mtazamo kama nilivyo mwambia hapo awali.
muda mwingine unapotumika kuwa ubao usiogope wino wa chaki
 
mimi kama mwanamke ningempa mtoto ubini wa baba yangu mzazi ili hata mtoto akimtafuta kuna fine za kutosha tu atalipa.... pili nisingemfikira tena huyo mwanaume suruali kwa kweli.. pole focus kumlea mwanao unamwanaume jinga jinga
Tatizo na ninyi mnazinguaaga hamjui kuomba.....mimi nina mwanamke nimezaa nae mtoto akati nikiwa form four 2008....ndo nilimtia mimba kajifungua 2009......Sasa kuna mwanamke naishi nae kwa kweli mzazi mwenzangu sio mstaarabu nishampga marufuku kunitafuta ....ye kama anataka pesa nitatuma kupitia kwa mama angu ndo zimfikie yeye
 
Tatizo na ninyi mnazinguaaga hamjui kuomba.....mimi nina mwanamke nimezaa nae mtoto akati nikiwa form four 2008....ndo nilimtia mimba kajifungua 2009......Sasa kuna mwanamke naishi nae kwa kweli mzazi mwenzangu sio mstaarabu nishampga marufuku kunitafuta ....ye kama anataka pesa nitatuma kupitia kwa mama angu ndo zimfikie yeye
sasa kwa nini umempiga marufuku we ni mgomvi
 
Mlee mwanao, ila usimdanganye... lakini kaa mbali na jamaa na umwambie mwanao ukweli kuhusu baba yake

In life things change, and time is the best and the wisest counselor...

Ila cha maana, kaa mbali na huyo jamaa... atakuharibia maisha tu
 
sasa kwa nini umempiga marufuku we ni mgomvi
mimi nimelala na mke wangu bila kufikiria anapiga cm saa tano usiku....hana cha maana anachozungumza anatuma sms.....zisizomamaana kama .....nakupenda sana n.k.....je ni akili niliona kuendelea kuwa na mazoea nae ni mwanzo mpya wa kuyumbisha ndoa yangu...



Je tutafakari waliooa wake wenye watoto....mzazi mwenzake anampigia simu usiku saa tano...na kumtumia text mbali mbali za mapenzi ni sahihi...

Niliona kuruhusu ukaribu nae ni tatizo jingine....ni bora kama anashida ampigie bibi wa mtoto alafu kama litakuwa nje ya uwezo wake nitamtekelezea......


Kwanza kajiaribia mengi sana nilikuwa na mipango mizur juu yake sasa yote niliivunja mwaka 2015 mwanzoni..
 
Ushauri mzuri wote ushasemwa hapo juu. Me nina langu moja tu "Likuepukalo lina heri nawe". Bond ya mama na mtoto ni natural, ila ya baba na mtoto, baba anaitengeneza. Muache tu arukeruke leo, kesho ndo wa kwanza kulalamiaka kwneye vyombo vya habari mtoto hanitunzi. Uzuri wa watoto ni viumbe ambao wapo very sensitive. Huna haja ya kumwambia fulani ni mzuri au mbaya, Mungu amewapa ufahamu huo

Kitu alichokiongelea BADILI TABIA na mimi kimenigusa haswaa. Hivi seriously wakati bado mna mahusiano mlikuwa mnaishije na huyo mwanaume? Kama hawezi kumuhudumia mtoto wake, sijui wakati upo naye aliwahi kukuletea hata chupi. Jinsi ulivyomuelezea tangu umejifungua hadi sasa hivi ni kama mtu ambaye hana msaada kwkao. Mtu anakuja kwa mwanae hata pipi hajabeba, afu anafikia kwenye hotpot bila soni anabugia chakula ambacho hakuwekewa yeye. Aisee me ningempikia na kingine ale hadi avimbiwe. Huyo ni mwanaume asiyejali, mchoyo na bahili first class, unless awe karogwa. Ungeolewa naye kwenye ndoa kila siku ungekuwa busy kanisani kutoa sadaka za ukombozi kwa ajili yake. Majukumu ya familia yote angekuachia na wakati uwezo anao, na yeye akirudi job ndo wa kwanza kuuliza "ubwabwa" tayari pyeee, ndo kuna wale wanawake "married singles", una sura tu ya mume home ila hana habari na watoto wake. Dada shukuru zigo limekuepuka, ungekuwa Unacheka kitalebani mbona. Una mwanao na uzuri una uwezo wa kumtunza, shukuru kwa baraka hiyo. Haina haja ya wewe kuwa na hela afu umhudumie mwanao kwa manung'uniko. Mlee mwanao kwa upendo wote na Mungu atakusimamia.

Afu ingawa mmeshaachana ana uhuru wa kuja kumuona mwanae, ila please awe anamuona sehemu nyingine apart from kuja directly home kwako. Ni kama haileti picha nzuri hivi. Utapata mwanaume mwingine sijui kama atakuelewa siku akimkuta baby daddy wako hapo home ati anakuja tu kumuona mwanae. It shall be well with you sis
 
Chuki zipi wakati atajua baba kafa. Sasa akiwa hai nitamwambia hajawahi kukutunza, hakujali wala nn huoni kuwa ni kupandikiza chuki kwa mtoto.

Kina baba wajibikeni kwa watoto wenu!!
husije kumwambia mtoto mzazi amekufa wakati yuko hai hata kama hamuelewani baba wa mtoto atabaki kuwa baba wa mtoto na ana damu yake kwa huyo mwanao kama mmekwaruzana hujue huyo akuwa ridhiki yako ila mtoto mweleze kuwa baba yake yupo na wala usimshirikishe kwenye huo ugomvi wenu
 
Lea mtoto wako,mshukuru Mungu kwa kukupa mtoto. Mtoto hajui chochote,ni malaika huyo usije ukampandikizia chuki akaanza kuchukia wanaume wote,dhambi hiyo utaijibia wew
 
Pole sana ila mshukuru Mungu kwa kila jambo na mwombee pia.. It is too soon to accuse the man.
 
Ingawa dada zetu mnatendwa sana, lakini mara nyingine mnaviburi mno, trough out your atricle hujaacha kumention material things, kama gari, kwangu, nitalea mwenyewe, mara nyingine how we behave tells how we should be treated as well, mwanamke ukiwa humble na msikivu sidhani kama kuna mwanaume kichaa atakayekutenda huyo atakua kichaa ukitaka kua safe kwa mwanaume kua humble supportive, loving and caring, kina dada punguzeni midomo, ujuaji na viburi...
 
Samahani mleta mada,namna uluvyoeleza huyu ni kama mumeo...Lakini sio.Hapo ndipo shida ilipo.Huyu ni hawara yako tu, na inawezekana hakupendi kivileee! Si ajabu tatizo n wewe ,kivipi ....hatujui.Kaza moyo lea mtoto na ujifunze.Kwz wengine pia ....msiwachukulie poa wanaume!
I like the term kyalosangi
 
Polee sana. Ila nitafute private ili tuweze kumlea mtoto wetu
 
Yani wkati mwingine binadamu mwenzako anaweza kukupitisha ktk magumu hadi ukajilaumu why ulikutana nae....ila jipe moyo,msamehe na yote umwachie Mungu,songa mbele tu and never expect his return.




Well,hongera kwa mtoto mamii,Mwenyezi Mungu Ndiyo Baba wa wote hata kama baba mzazi kasusa,Baba Muumbaji Wake anampenda na kumuwazia mema,ubarikiwe
 
Wahenga walisema wastara hasumbuki,wambili havai moja.Nisiwachose,ni kuwa nimevumilia mengi kwa mwanaume huyu.

Tuna mtoto mmoja wa kiume ana miezi mi5 sasa.mwanaume amekuwa hashikiki,hashauriki na wala hatoi chochote cha matumizi si yangu wala ya mtoto.

Hakuwahi hudumia mimba na hata siku nazaa kwa uchungu alikuwa busy na anaowajua wakila maraha ya mjini.Toka mtoto kazaliwa amenunua pampas set mbili tu za sleepy,mkungu mmoja wa ndizi na nyama kilo mbili nilipojifungua nayo ni baada ya kusema sana.

Ana fanya kazi private company,anapata pesa nzuri tu.Ila kumhudumia mwanaye imekuwa majanga na yote hii anafanya kisa nami nina kazi.Nilikaa nyumbani siku 84 kulea mtoto hilo hakujali,akisema nawe una kazi.Nikasema its ok mtoto ni for some reasons hatuishi pamoja amepanga kwake nami naishi kwangu na mtoto.

Kilichonisukuma kuleta uzi huu mida hii ni kuwa jana alikuja kumwona mtoto,akiwa mikono mitupu as usual.Nikamwuliza hata kuchukua kilo ya nyama kwa mangi umeshindwa?akasema,amekuta nyama imeisha akambeba mtoto kidogo then akamweka sofani akafungua hotpot akakata ugali na samaki akala.

Imefika saa 8 nikawa na safari ya kwenda kanisani,nikamweleza nikaingia chumbani kwangu kubadili, akaja mbiombio akaniaga na kutoka.Robo saa nami nikawa tayari nikamwaga msichana wangu wa kazi,nikamwachia na mtoto nikawasha gari nikatoka.

Wakati niko barabarani sauti ikanambia hebu pita hapo kwa baba nanihii kabla ya kwenda kanisani.Basi nikapaki gari jirani then nikatembea,kufika pale nikabisha kama dakika 5 ndo akafungua.

Nikaingia nikakuta kumbe anaishi na binti,nikamwuliza ndo huyu anayesababisha usitoe hata hela ya pampas za mwanao? Nikamwambia mpigie simu mama yako tuongee akagoma.Basi nikatoka zangu nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari yangu ya kanisani njiani nikidrive huku nalia kwa uchungu.

Nimefika nimechelewa kiasi,nikakaa kiti cha nyuma kabisa nikajiinamia nikilia,huku moyoni nikisema uko wapi Mungu wangu? Mawimbi yananipiga,uko wapi unitet(ni wimbo,niupendao).

Ibada imeisha saa 12 jioni nikarudi nyumbani kichwani nikiwa na mawazo tele.Nikakuta mwanagu analia nikamnyonyesha akalala.Nimestuka muda huu nikamtazama mwanangu alivyolala kama malaika,ila kichwani nimeamka na resolution moja tu,kwamba from today mwanagu hana baba,mimi ndo baba na ndo mama yake.

Nilitaka mpigia mamake ila nikaona yatakuwa yaleyale.Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu nitamlea mwanangu,naasume amekufa,and yes nimemwambia asifike kwangu tena.Kama ni mwanaye asubiri akifikisha 18 years atamtafuta.

Kama ni wewe mwanamke mwenzangu utafanyaje? Kwanini mwanaume ukatae kuhudumia mwanao kisa starehe?[/QUOTE]
Mbona unaomba ushauri kwa akina mama tu, wapo wanaume wenye ushauri mzuri tu!!
 
Hasira hasara. Wewe endeleza mawasiliano na mzazi mwenzako, muwe na mahusiano ya kawaida tu. kugegedana naye hapana, muachane kwa amani kwa faida ya mtoto wenu
 
Pole sana dada.kaza moyo songa mbele mtakutana ipo siku atatamani kuwa karibu yako lakini itakuwa too late.
 
Tatizo na ninyi mnazinguaaga hamjui kuomba.....mimi nina mwanamke nimezaa nae mtoto akati nikiwa form four 2008....ndo nilimtia mimba kajifungua 2009......Sasa kuna mwanamke naishi nae kwa kweli mzazi mwenzangu sio mstaarabu nishampga marufuku kunitafuta ....ye kama anataka pesa nitatuma kupitia kwa mama angu ndo zimfikie yeye
wewe kweli Wakuacha kama lilivyo jina lako.
yaani pesa ipite kwa mama yako ndo ifike kwa mzazi mwenzio?
hivi siku ulipokuwa unam-mimba huyu dada mama yako alikuwepo ama alijua?
kwann usitafute njia nyingine nzuri zaid na ili asimlee mwanao kwa jeuri na kiburi kuliko hii?
ukweli nakufungulia uzi aisee
 
Mapenzi ya kulazimishana mwisho wake siku zote ni mbaya... Pole sana...
 
Back
Top Bottom