''Mwanangu, babako amekufa''

''Mwanangu, babako amekufa''

Kwanini amlipize mama kwa mtoto? ugomvi wake na mama wa mtoto unamuhusu nini. Kuna njia nyingi tu za kumtunza mtoto hata kama hutaki kuonana na mamaake kama kweli hutaki kumtelekeza. Mnaendekeza ujinga tu kutelekeza watoto wasio na hatia.
Wanawake akili yenu inawatosha wenyewe uwezi kuniletea jeuri na kiburi cha kishenge eti kisa una mtoto wangu unajua nitakuhudumia tu.

Binafsi nitakupa optional ya kunipa mtoto wangu nilee mwenyewe...!

Mwanamke akili zake km mtoto ukute jamaa kafanyiwa visa weeh baada ya mimba mnajifanya kunyenyekea mkome tamaa zenu badala ya kukomaa kutafuta pesa mnaendekeza tamaa kupenda mtelemko.
 
Kimtokacho mtu kimeujaza moyo wake,pole ndio ulivyolelewa.wapi niliposema nitamjaza mtoto chuki?please onyesha kwenye bandiko langu niliposema hayo.
Achana na huyo mropokaji umesema unaenda kanisa mungu atakupa amani rohoni na nguvu
 
Wanawake akili yenu inawatosha wenyewe uwezi kuniletea jeuri na kiburi cha kishenge eti kisa una mtoto wangu unajua nitakuhudumia tu.

Binafsi nitakupa optional ya kunipa mtoto wangu nilee mwenyewe...!

Mwanamke akili zake km mtoto ukute jamaa kafanyiwa visa weeh baada ya mimba mnajifanya kunyenyekea mkome tamaa zenu badala ya kukomaa kutafuta pesa mnaendekeza tamaa kupenda mtelemko.
Anaetakiwa kuhudumiwa hapa sio mama ni mtoto. na ndomaana nikasema kuna njia kibao za kumpelekea huduma huyo mtoto bila hata kuonana na huyo mamaake. Hata kama mlifanyiana visa na huyo mamaake havimuhusu mtoto. inaelekea na wewe ni walewale umemtelekeza mtoto kwa kisingizio cha kugombana na mamaake. Tunza mtoto wewe acha visingizo alafu mtoto akikua ndo ujilete.
 
Pole sana mamy kwa mie nakuelewa sana kwani nimepitia hayo
Jipe moyo mkuu
 
Anaetakiwa kuhudumiwa hapa sio mama ni mtoto. na ndomaana nikasema kuna njia kibao za kumpelekea huduma huyo mtoto bila hata kuonana na huyo mamaake. Hata kama mlifanyiana visa na huyo mamaake havimuhusu mtoto. inaelekea na wewe ni walewale umemtelekeza mtoto kwa kisingizio cha kugombana na mamaake. Tunza mtoto wewe acha visingizo alafu mtoto akikua ndo ujilete.
Mtoto tu ndiyo uniendeshe kama gari bovu mimi kwangu akikushinda niletee sitaki kuchunwa kizembe!
 
Kumzalia boyfriend, mmh...hilo jambo lisitokee kwenye maisha yangu..
Pole dada lea mwanao,siku hazigandi utamsamehe mzazi mwenzio na mtoto atamjua tu baba,usihofu kuhusu mambo ya baadae hangaika na ya sasa....
 
Hua kuna mtindo wa wadada wanatamani kuzalishwa wanasema watatunza wenyewe ingawaje mambo yakiwashinda wanaanza kulalama sijasema nawe upo hapana. Ila wanaume tuwe makini na wadada pia sio kila uhusiano ni wa kuzaa mtoto ingawaje akipatikana mtoto inabidi ubinadamu utumike si vinginevyo.
Wazazi wetu angefanya haya yanayoendelea ss sijui tungekua wapi, tuchukue majukumu yetu tusiyakimbie.
 
Thread closed,nshafanya maamuz and that's it!
 
Noma sana,hata siku mojamoja kutupia hela kidogo anashindwa!mwanaume suruali huyo
 
Mwanaume kama hakupendi hawezi kulea mtoto ....ndio maana kuna wanawake wanawatoto anapata mwanaume anamlelea watoto vizuri kabisa..hapa kama si mumeo move on dear msamehe jisamehe fanya toba ya kweli lea mtoto wako Mungu atakubariki ...Usithubutu kumwambia mtoto kuwa babake amefariki wakati yu hai ...itamsumbua mtoto ..itakusumbua hata wewe UKWELI UTAKUWEKA HURU UWE NA AMANI NI MAPITO TU NALO HILO LITAPITA
 
Endelea tu Kumcha Mungu,,,,baada dhiki faraja in mtihani tuu na majaribu ya nafsi
 
Ukiona Hivo ujue baba hampendi mama hata kidogo,angekuwa anakupenda unge hudumiwa bila ubishi.
swala si kumpenda mama, mahusiano yanapoanza kuisha pia n kitu mtu unategemea..ila kama mahusiano yalitengeneza mtoto hata kama yatisha si sawa kwa baba kutelekeza mtoto kwa kiburi cha kuwa utatafutwa tu vile we ni baba. msikimbie majukumu baba n kitu kikubwa sana sio mkojo tu
 
Uliomba mtt?
Aliomba mtt?
Ilkua ni accident
Ullazmisha
Au ilkuaje??
 
Back
Top Bottom