''Mwanangu, babako amekufa''

''Mwanangu, babako amekufa''

Mwanao mwambienukweli kuwa baba yake hasaidii, hatoi matumizi (aka zigo la misumari) ila mwambienin such a way usije muumiza hisia zake.

Ushauri mbaya sana huu, kama una mtoto usidhubutu kumuelezea mabaya ya baba yake au mama yake.

Hakuna namna utayaremba hayo maneno, eti asiumie.
 
ok, some times hawa jamaa ni pasua kichwa
Anakuwa na mchepuko wake wee akisha nasa mimba anajifanya kuleta mahaba ya kihindi...!

Sometimes wanaume wanatumia mwanya huo kulipa kisasi kwa wadada wasumbufu...!
 
dah wengine wanatafta mtoto usiku na mchana wengine hawana habari na wanao
 
Tafadhal mama kama hyo mimba uliweka ww ndio utafanya hvyo.
Kuna sheria.mpe mda wa kuona kiumbe chake ni haki yake hata kama hatoi ela.
Kutoa pesa ya mtoto n muhim but syo kigezo cha kukatazwa kuona mtoto.
 
hapo kwenye asije mtambulisha sidhan kama upo sahihi akina mama wengi hayo ndo makosa ambayo huwa mnayafanya tena wengine huthubutu hata waambia watoto baba yao amekufa wakati yupo hai tabia hii si rafiki kwa afya ya ubongo wa watoto wasije pandikiza mbegu ya chuki baina ya mtoto na mzazi ayo mengine yaacheni nature itake control sio kuanza mjaza mtoto mambo ya ajabu kisa baba yake ameleta usumbufu mi sikubaliani na hii tabia kabisa
Unataka upandiwe mbegu nzuri we umepanda?hujui kama muosha huoshwa?huoni ananyonyesha mtoto akiwa na uchungu?dada endelea mbele mlee mtoto na usisahau kumwambia uovu wa baba yake kila ukipata muda
 
Samahani mleta mada,namna uluvyoeleza huyu ni kama mumeo...Lakini sio.Hapo ndipo shida ilipo.Huyu ni hawara yako tu, na inawezekana hakupendi kivileee! Si ajabu tatizo n wewe ,kivipi ....hatujui.Kaza moyo lea mtoto na ujifunze.Kwz wengine pia ....msiwachukulie poa wanaume!
Nami wazo langu lilikua ni hilo, mwanamke anaweza kuwa ni tatizo mimi yamenitokea na hadi sasa naishi na mtoto ingawa ilikua ni kwa mbinde sana kumchukua, wanawake ni kama tabia yao unaweza kuwa nae kama wapenzi na mkapanga mambo mengi kumbe yeye ni looter. Anakufanya kama mmoja ya vutega uchumi vyake, unaweza kuta alikua na mwanamme zaidi ya huyo, sasa baada ya jamaa kukata tamaa na yule mwingine hana time nae ndo kulalamika kuwa ameachiwa mtoto, wakati mwingine wanawake we acha tu.
 
kaushia mdada move forward, mlipokua kwenye dating ungekua unaenda church ivo ungeepusha mengi, be care sio kila relationship ina destiny ya maisha yako jifunze kumfaham mtu kabla ya mambo ya kuzaa, sema wanawake wengi hua mnawaza kwa mihemko. unaeza ukamblock kuongea nae totally.
 
w
Wahenga walisema wastara hasumbuki,wambili havai moja.Nisiwachose,ni kuwa nimevumilia mengi kwa mwanaume huyu.

Tuna mtoto mmoja wa kiume ana miezi mi5 sasa.mwanaume amekuwa hashikiki,hashauriki na wala hatoi chochote cha matumizi si yangu wala ya mtoto.

Hakuwahi hudumia mimba na hata siku nazaa kwa uchungu alikuwa busy na anaowajua wakila maraha ya mjini.Toka mtoto kazaliwa amenunua pampas set mbili tu za sleepy,mkungu mmoja wa ndizi na nyama kilo mbili nilipojifungua nayo ni baada ya kusema sana.

Ana fanya kazi private company,anapata pesa nzuri tu.Ila kumhudumia mwanaye imekuwa majanga na yote hii anafanya kisa nami nina kazi.Nilikaa nyumbani siku 84 kulea mtoto hilo hakujali,akisema nawe una kazi.Nikasema its ok mtoto ni for some reasons hatuishi pamoja amepanga kwake nami naishi kwangu na mtoto.

Kilichonisukuma kuleta uzi huu mida hii ni kuwa jana alikuja kumwona mtoto,akiwa mikono mitupu as usual.Nikamwuliza hata kuchukua kilo ya nyama kwa mangi umeshindwa?akasema,amekuta nyama imeisha akambeba mtoto kidogo then akamweka sofani akafungua hotpot akakata ugali na samaki akala.

Imefika saa 8 nikawa na safari ya kwenda kanisani,nikamweleza nikaingia chumbani kwangu kubadili, akaja mbiombio akaniaga na kutoka.Robo saa nami nikawa tayari nikamwaga msichana wangu wa kazi,nikamwachia na mtoto nikawasha gari nikatoka.

Wakati niko barabarani sauti ikanambia hebu pita hapo kwa baba nanihii kabla ya kwenda kanisani.Basi nikapaki gari jirani then nikatembea,kufika pale nikabisha kama dakika 5 ndo akafungua.

Nikaingia nikakuta kumbe anaishi na binti,nikamwuliza ndo huyu anayesababisha usitoe hata hela ya pampas za mwanao? Nikamwambia mpigie simu mama yako tuongee akagoma.Basi nikatoka zangu nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari yangu ya kanisani njiani nikidrive huku nalia kwa uchungu.

Nimefika nimechelewa kiasi,nikakaa kiti cha nyuma kabisa nikajiinamia nikilia,huku moyoni nikisema uko wapi Mungu wangu? Mawimbi yananipiga,uko wapi unitet(ni wimbo,niupendao).

Ibada imeisha saa 12 jioni nikarudi nyumbani kichwani nikiwa na mawazo tele.Nikakuta mwanagu analia nikamnyonyesha akalala.Nimestuka muda huu nikamtazama mwanangu alivyolala kama malaika,ila kichwani nimeamka na resolution moja tu,kwamba from today mwanagu hana baba,mimi ndo baba na ndo mama yake.

Nilitaka mpigia mamake ila nikaona yatakuwa yaleyale.Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu nitamlea mwanangu,naasume amekufa,and yes nimemwambia asifike kwangu tena.Kama ni mwanaye asubiri akifikisha 18 years atamtafuta.

Kama ni wewe mwanamke mwenzangu utafanyaje? Kwanini mwanaume ukatae kuhudumia mwanao kisa starehe?
wanaume wa hivi wa ovyo sana....tunatakiwa kuhudumia hata kama mapenzi kwa mama aumpenzi hayapo...mtoto ni issue nyingine support mzazi mwenzio...huyu anatuaibisha wanaume na nimpumbavu kabisa
 
Hapa yawezekana hata wewe mwanamke kuna mabaya uliyomfanyia huyu jamaa japokuwa sijui, pengine tungemsikiliza mwanaume angekuwa na ya kukulaumu wewe maana wanawake nao sometimes ndiyo kikwazo tena kikwazo hasa japo si vizuri kutomhudumia mwana wa damu yako. Kama Mungu amekujaalia kipato mhudumie tu mwanao Ila usimwambie Baba yako kafa mwambie tu yupo utamjenga vizuri kisaikolojia. Ila umenishangaza alipokuja kwako ukamwambia hukupita kwa Mangi angalau uchukuwe nyama, najiuliza kwanini nyama na kwanini isiwe zawadi yoyote kwa mtoto? Kabla ya kumlaumu jamaa jiangalie na wewe mwenyewe pengine wewe ndiye kikwazo
 
Acha kuuliza upuuzi,nanyonyesha,au wadhan bila kula supu na mtori maziwa yatapatikanaje?unaona nyama ni ishu sana eeh
 
Sina
kaushia mdada move forward, mlipokua kwenye dating ungekua unaenda church ivo ungeepusha mengi, be care sio kila relationship ina destiny ya maisha yako jifunze kumfaham mtu kabla ya mambo ya kuzaa, sema wanawake wengi hua mnawaza kwa mihemko. unaeza ukamblock kuongea nae totally.

Sina time naye,nilitaka ahudumie mwanae,ila ndo hivo mtoto huyu amsahau.
 
Unajua mwenyewe kwa kuwa tunasikia upande mmoja unajifanya kumlaum jamaa ila nahakika km akijitokeza hapa tutajua mengi sana!

Unajua siyo rahisi kwa mwanaume kumsusa mwanae kilichopo ni mazingira fulami ambayo utakuwa unataka kunufaika kupitia mgongo wa mtoto au kuna kitu kibaya ulimfanyia anakulipiza au mwenendo wako haukua mzuri na bahati mbaya ukapata mimba!
 
Nyie mnaomlaumu huyu mleta maada mnanishangaza sana. Mtu ana kazi nzuri tuu inamlipa kwanini hasimuhudumie mtoto? hata kama aligombana na mamaake ugomvi wake na mamaake haumuhusu mtoto. yeye angekuwa ni baba bora angemtunza tu huyo mtoto sabab huwezo anao. Halafu bado anafika kwa mwanamke akuta kuna msosi anakula bila hata ya aibu alafu mnamtetea. Kweli kuwa mwanamke ni kaziii.
 
Unajua mwenyewe kwa kuwa tunasikia upande mmoja unajifanya kumlaum jamaa ila nahakika km akijitokeza hapa tutajua mengi sana!

Unajua siyo rahisi kwa mwanaume kumsusa mwanae kilichopo ni mazingira fulami ambayo utakuwa unataka kunufaika kupitia mgongo wa mtoto au kuna kitu kibaya ulimfanyia anakulipiza au mwenendo wako haukua mzuri na bahati mbaya ukapata mimba!
Kwanini amlipize mama kwa mtoto? ugomvi wake na mama wa mtoto unamuhusu nini. Kuna njia nyingi tu za kumtunza mtoto hata kama hutaki kuonana na mamaake kama kweli hutaki kumtelekeza. Mnaendekeza ujinga tu kutelekeza watoto wasio na hatia.
 
Wahenga walisema wastara hasumbuki,wambili havai moja.Nisiwachose,ni kuwa nimevumilia mengi kwa mwanaume huyu.

Tuna mtoto mmoja wa kiume ana miezi mi5 sasa.mwanaume amekuwa hashikiki,hashauriki na wala hatoi chochote cha matumizi si yangu wala ya mtoto.

Hakuwahi hudumia mimba na hata siku nazaa kwa uchungu alikuwa busy na anaowajua wakila maraha ya mjini.Toka mtoto kazaliwa amenunua pampas set mbili tu za sleepy,mkungu mmoja wa ndizi na nyama kilo mbili nilipojifungua nayo ni baada ya kusema sana.

Ana fanya kazi private company,anapata pesa nzuri tu.Ila kumhudumia mwanaye imekuwa majanga na yote hii anafanya kisa nami nina kazi.Nilikaa nyumbani siku 84 kulea mtoto hilo hakujali,akisema nawe una kazi.Nikasema its ok mtoto ni for some reasons hatuishi pamoja amepanga kwake nami naishi kwangu na mtoto.

Kilichonisukuma kuleta uzi huu mida hii ni kuwa jana alikuja kumwona mtoto,akiwa mikono mitupu as usual.Nikamwuliza hata kuchukua kilo ya nyama kwa mangi umeshindwa?akasema,amekuta nyama imeisha akambeba mtoto kidogo then akamweka sofani akafungua hotpot akakata ugali na samaki akala.

Imefika saa 8 nikawa na safari ya kwenda kanisani,nikamweleza nikaingia chumbani kwangu kubadili, akaja mbiombio akaniaga na kutoka.Robo saa nami nikawa tayari nikamwaga msichana wangu wa kazi,nikamwachia na mtoto nikawasha gari nikatoka.

Wakati niko barabarani sauti ikanambia hebu pita hapo kwa baba nanihii kabla ya kwenda kanisani.Basi nikapaki gari jirani then nikatembea,kufika pale nikabisha kama dakika 5 ndo akafungua.

Nikaingia nikakuta kumbe anaishi na binti,nikamwuliza ndo huyu anayesababisha usitoe hata hela ya pampas za mwanao? Nikamwambia mpigie simu mama yako tuongee akagoma.Basi nikatoka zangu nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari yangu ya kanisani njiani nikidrive huku nalia kwa uchungu.

Nimefika nimechelewa kiasi,nikakaa kiti cha nyuma kabisa nikajiinamia nikilia,huku moyoni nikisema uko wapi Mungu wangu? Mawimbi yananipiga,uko wapi unitet(ni wimbo,niupendao).

Ibada imeisha saa 12 jioni nikarudi nyumbani kichwani nikiwa na mawazo tele.Nikakuta mwanagu analia nikamnyonyesha akalala.Nimestuka muda huu nikamtazama mwanangu alivyolala kama malaika,ila kichwani nimeamka na resolution moja tu,kwamba from today mwanagu hana baba,mimi ndo baba na ndo mama yake.

Nilitaka mpigia mamake ila nikaona yatakuwa yaleyale.Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu nitamlea mwanangu,naasume amekufa,and yes nimemwambia asifike kwangu tena.Kama ni mwanaye asubiri akifikisha 18 years atamtafuta.

Kama ni wewe mwanamke mwenzangu utafanyaje? Kwanini mwanaume ukatae kuhudumia mwanao kisa starehe?
Pole sana dada.fanya kama ulivyoamua
 
Back
Top Bottom