Wahenga walisema wastara hasumbuki,wambili havai moja.Nisiwachose,ni kuwa nimevumilia mengi kwa mwanaume huyu.
Tuna mtoto mmoja wa kiume ana miezi mi5 sasa.mwanaume amekuwa hashikiki,hashauriki na wala hatoi chochote cha matumizi si yangu wala ya mtoto.
Hakuwahi hudumia mimba na hata siku nazaa kwa uchungu alikuwa busy na anaowajua wakila maraha ya mjini.Toka mtoto kazaliwa amenunua pampas set mbili tu za sleepy,mkungu mmoja wa ndizi na nyama kilo mbili nilipojifungua nayo ni baada ya kusema sana.
Ana fanya kazi private company,anapata pesa nzuri tu.Ila kumhudumia mwanaye imekuwa majanga na yote hii anafanya kisa nami nina kazi.Nilikaa nyumbani siku 84 kulea mtoto hilo hakujali,akisema nawe una kazi.Nikasema its ok mtoto ni for some reasons hatuishi pamoja amepanga kwake nami naishi kwangu na mtoto.
Kilichonisukuma kuleta uzi huu mida hii ni kuwa jana alikuja kumwona mtoto,akiwa mikono mitupu as usual.Nikamwuliza hata kuchukua kilo ya nyama kwa mangi umeshindwa?akasema,amekuta nyama imeisha akambeba mtoto kidogo then akamweka sofani akafungua hotpot akakata ugali na samaki akala.
Imefika saa 8 nikawa na safari ya kwenda kanisani,nikamweleza nikaingia chumbani kwangu kubadili, akaja mbiombio akaniaga na kutoka.Robo saa nami nikawa tayari nikamwaga msichana wangu wa kazi,nikamwachia na mtoto nikawasha gari nikatoka.
Wakati niko barabarani sauti ikanambia hebu pita hapo kwa baba nanihii kabla ya kwenda kanisani.Basi nikapaki gari jirani then nikatembea,kufika pale nikabisha kama dakika 5 ndo akafungua.
Nikaingia nikakuta kumbe anaishi na binti,nikamwuliza ndo huyu anayesababisha usitoe hata hela ya pampas za mwanao? Nikamwambia mpigie simu mama yako tuongee akagoma.Basi nikatoka zangu nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari yangu ya kanisani njiani nikidrive huku nalia kwa uchungu.
Nimefika nimechelewa kiasi,nikakaa kiti cha nyuma kabisa nikajiinamia nikilia,huku moyoni nikisema uko wapi Mungu wangu? Mawimbi yananipiga,uko wapi unitet(ni wimbo,niupendao).
Ibada imeisha saa 12 jioni nikarudi nyumbani kichwani nikiwa na mawazo tele.Nikakuta mwanagu analia nikamnyonyesha akalala.Nimestuka muda huu nikamtazama mwanangu alivyolala kama malaika,ila kichwani nimeamka na resolution moja tu,kwamba from today mwanagu hana baba,mimi ndo baba na ndo mama yake.
Nilitaka mpigia mamake ila nikaona yatakuwa yaleyale.Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu nitamlea mwanangu,naasume amekufa,and yes nimemwambia asifike kwangu tena.Kama ni mwanaye asubiri akifikisha 18 years atamtafuta.
Kama ni wewe mwanamke mwenzangu utafanyaje? Kwanini mwanaume ukatae kuhudumia mwanao kisa starehe?