''Mwanangu, babako amekufa''

''Mwanangu, babako amekufa''

Samahani mleta mada,namna uluvyoeleza huyu ni kama mumeo...Lakini sio.Hapo ndipo shida ilipo.Huyu ni hawara yako tu, na inawezekana hakupendi kivileee! Si ajabu tatizo n wewe ,kivipi ....hatujui.Kaza moyo lea mtoto na ujifunze.Kwz wengine pia ....msiwachukulie poa wanaume!
Nikweli ulichosema mimi mwenyewe nilijua ni mumewe. Kitu kingine kwanini mleta mada unasisitiza zaidi matumizi ya mtoto kuliko upendo kati yenu? kwani mlipanga kuzaa na kulea tu basi? Mbona unauwezo wa kulea mtoto mwenyewe kwanini usifikiri jinsi ya kurudisha upendo wenu kwanza. Unawaza juu ya upendo wa baba na mtoto, huyo atampenda tu, na pia anaweza akampenda asikupende wewe. Matumizi ya mtoto hayazihilishi upendo kati yenu anweza akayatoa na usikupende. Jiulize wewe shida yako ni upendo shida yako ni matumizi? kwanini umdanganye mtoto kwamba baba amekufa anahusikaje kwenye ugomvi wenu mpaka umtese kiasi hicho, na kwa faida gani?
 
Usifanye maamuzi ukiwa na hasira,tulia kwanza halafu jiulize jee unaweza kuishi bila yeye uwepo wake? moyo wako umekubali kua its OVER,vyovyote itakavyokua huyo ni mzazi mwenzio sisemi kama huwezi kusonga mbele bila yeye
ila jee unaposema basi unamaanisha au basi ya hasira?
Ikiwa umeamua kua utalea mtoto wako mwenyewe na humuhitaji sio kwa matumizi tuu bali hata kwa ushauri ntasema
sawa endelea mbele na maisha yako na usimtafute na hata akikutafuta mpotezee...
 
Huu ndio ujinga wa baadhi ya wanawake kudhani kumzalia mwanaume mtoto basi anakuwa wako milele. Kama hajakupenda kwa dhati wakati mnadate tu usitegemee akakupenda wala kukujali wewe n huyo mtoto wakati umeshazuru leba. Kumbukeni si kila mwanaume anafaa kuitwa baba.
Kuna watu nawafahamu walizaa hivyohivyo staili hiyohiyo ya mtoa mada wameharibu maisha yao mazima sababu hakuna mwanaume atakubali kuoa mwanamke ambaye keshazaa na mwanaume mwingine labda huyo mwanaume awe amekufa (hayupo kabisa).
Kwanini utengeneze mazingira ya kuharibu maisha yako? Hata useme baba wa mtoto amekufa haisaidii chochote ukweli hubaki palepale baba yupo n mtoto bado atamhitaji tu. Na inawezekana kabisa wewe mwenyewe siku ukamuonyesha mwanao babako yule pale.
 
Samahani mleta mada,namna uluvyoeleza huyu ni kama mumeo...Lakini sio.Hapo ndipo shida ilipo.Huyu ni hawara yako tu, na inawezekana hakupendi kivileee! Si ajabu tatizo n wewe ,kivipi ....hatujui.Kaza moyo lea mtoto na ujifunze.Kwz wengine pia ....msiwachukulie poa wanaume!
Una akili kuliko shule, umenigusa sana, halafu tunamlilia MUNGU uko wapi wakati hatuna hata ndoa, tunataka MUNGU aonekane kwenye Uzinzi wetu? Hahahaha hii ni joke.

Ok, Dada tubu na endelea na maisha yako, maadamu una kazi
 
Huu ndio ujinga wa baadhi ya wanawake kudhani kumzalia mwanaume mtoto basi anakuwa wako milele. Kama hajakupenda kwa dhati wakati mnadate tu usitegemee akakupenda wala kukujali wewe n huyo mtoto wakati umeshazuru leba. Kumbukeni si kila mwanaume anafaa kuitwa baba.
Kuna watu nawafahamu walizaa hivyohivyo staili hiyohiyo ya mtoa mada wameharibu maisha yao mazima sababu hakuna mwanaume atakubali kuoa mwanamke ambaye keshazaa na mwanaume mwingine labda huyo mwanaume awe amekufa (hayupo kabisa).
Kwanini utengeneze mazingira ya kuharibu maisha yako? Hata useme baba wa mtoto amekufa haisaidii chochote ukweli hubaki palepale baba yupo n mtoto bado atamhitaji tu. Na inawezekana kabisa wewe mwenyewe siku ukamuonyesha mwanao babako yule pale.
Nakuunga mkono, ila napingana nawewe sehem ya kua wanawake walio zaa hawaolewi, wanaolewa sana tu mkuu. Mume na mke mwema hutoka kwa Mungu, Kama mtoa mada kakosea kuzaa bila ya ndoa sio kwamba amekosea maisha yake yote yameishia hapo, Kuna mwanaume yupo atamuowa
 
Nakuunga mkono, ila napingana nawewe sehem ya kua wanawake walio zaa hawaolewi, wanaolewa sana tu mkuu. Mume na mke mwema hutoka kwa Mungu, Kama mtoa mada kakosea kuzaa bila ya ndoa sio kwamba amekosea maisha yake yote yameishia hapo, Kuna mwanamke yupo atamuowa
Mkuu inahitaji moyo wa ziada kuoa m'ke aliyezaa. Mara nyingi familia ya mwanaume wanakuwa kikwazo na kubwa ni kujua kwanini huko alikozaa hakuolewa. Unaweza ukawa mwanamke mzuri, mwenye tabia nzuri n sifa zote lakn doa la kuwa na mtoto likakuweka mashakani.
 
Pole dear... This issue is very disturb and hurt kids most of the time.. I think umeuumia because you still love him and expected him to do More , but most of it at least to show a care for you and Baby.. At the end umeaambulia patupu from your expectations.. Dear don't cry or hurt yourself because of Him.. I do understanding unavyojisikia .... Inauma sana.. You probably feel as a failure or why you. Whatever the pain you have never feel regret because that baby came in this earth with reason , God appointed Him.. What I do advice you is : Move on with your life without baby Daddy.. Dont depend on Him 100% because you will get hurt and disapointment again.. Now ushajua who he is then try not to bother for him anymore.. Katika kumove on with your life dont tell your own son that his dad died , while He stills alive somewhere, thats not nice .. Since you go to church and read the Bible, pray for the healing and Erase those words by the Blood of Jesus , muaachie Mungu.. Lea mwanao Mama maana wewe ndio unauujua uchungu zaidi kuliko huyo Baby Daddy.. Focus on God and your son... Kazi yako ni kulea na ku show love to your son .. Akikua , akiuliza baba yake mwambie aliko if you will have information zake .. Kama hautazijua dont bother.. Dear ninachopendea boys , are always Mama's boy itachukua muda mmpaka yeye kukuuliza about his father.. Huyo Baby daddy akimmtaka mwanae mmpange wapi amuone mtoto .. To me I do advice you awe anakutana nae kwa Bibi mzaa Baba is better than kumuacha mwanao na huyo unknown step mother ... ( msichana wake ).. Akimaliza kuspend time nae kammchukue mwenyewe kwa bibi.. Epuka kuwa ukaribu na huyo Baby Daddy... Usiruhusu aje kwako hovyo hovyo , unless kama baby akiwa anaumwa sana .. Na wewe pia acha kwenda kwake, move on with your life and God will give the right man who will be the best husband and Father for your Son.. Good luck.. Thanks..
 
Chuki zipi wakati atajua baba kafa. Sasa akiwa hai nitamwambia hajawahi kukutunza, hakujali wala nn huoni kuwa ni kupandikiza chuki kwa mtoto.

Kina baba wajibikeni kwa watoto wenu!!
Asume umemtambulisha baba kafa zen aje ajuwe kuwa baba yupo hebu nambie mtot atakuelewa kuwa baba ake hakumhudumia? Acha kujitoa ufaham bora umwambie tu ukweli mwanao,yy mwenyewe atajua cha kufanya sio chuku yako na mmeo uweke kwa mtot hapo ndo mnakoseaga pakubwa sana,ujuwe na huyo baba nae anajua kujitetea ikibid nae atamwambia hata uongo je itakuwaje ?wanawake jigunzeni kusema ukweli kw wtt mzaz n mzaz tu, mbona kuna wanawake wanazaa watt halafu wanawakimbia wakiwa wdogo mda mwingine wanawatupa hata chooni wanaokotwa na baba tunawakuza mbona wga hatuwa fundishi ujinga huu, kuweni wakweli bwana.
 
kila mtu anaish kwake mmh, atakuwa Hana uhakika Kama Ni wake anangoja akue then achek sura Ni yake au laaa.
 
Lea mwanao dada wala huyo pimbi asikutishe. Hesabu alishadead..mzike kabisa! Huwezi kushindwa kumlea mtoto...trust me. Hata kama una kipato kidogo kiasi gani wewe mlee mwanao hivyo hivyo na utashangaa maisha yanasonga na mtoto anakuwa.
Acha kulia..na nakwambia tena usipoteze machozi yako kwa mwanaume asiyekuthamini hata siku moja. Furahia maisha kadri uwezavyo...furahi na mwanao. Hushindwi kitu nakuambia. Tena pimbi mwenyewe hata hajakuoa. Achana na huyo Shwain...mxiuuuuu
 
Ila wanaume bwana, wakati mwingine tunajitafutia malaana bila sababu. Sawa, humpendi mama watoto na hutaki kuwa na mahusiano nae, basi hata mtoto wako kweli? Hivi ulifikiri mwisho wa kustarehe na mwanamke ni nini kama sio mtoto?
 
Huyo mtoto mleee mwenyewe ila chonde chonde usiweke chuki za kumchafua baba yake we kaa kimya yeye mwenyewe akikua ataelewa who was right and who was guilty na atachukua maamuzi sahihi
 
Wahenga walisema wastara hasumbuki,wambili havai moja.Nisiwachose,ni kuwa nimevumilia mengi kwa mwanaume huyu.

Tuna mtoto mmoja wa kiume ana miezi mi5 sasa.mwanaume amekuwa hashikiki,hashauriki na wala hatoi chochote cha matumizi si yangu wala ya mtoto.

Hakuwahi hudumia mimba na hata siku nazaa kwa uchungu alikuwa busy na anaowajua wakila maraha ya mjini.Toka mtoto kazaliwa amenunua pampas set mbili tu za sleepy ,mkungu mmoja wa ndizi na nyama kilo mbili nilipojifungua.nayo ni baada ya kusema sana.

Ana fanya kazi private company,anapata pesa nzuri tu.Ila kumhudumia mwanaye imekuwa majanga.na yote hii anafanya kisa nami nina kazi.Nilikaa nyumbani siku 84 kulea mtoto hilo hakujali,akisema nawe una kazi.Nikasema its ok mtoto ni

For some reasons hatuishi,pamoja.amepanga kwake nami naishi kwangu na mtoto.kilichonisukuma kuleta uzi huu mida hii,ni kuwa jana alikuja kumwona mtoto,akiwa mikono mitupu as usual.

Nikamwuliza hata kuchukua kilo ya nyama kwa mangi umeshindwa?akasema,amekuta nyama imeisha.akambeba mtoto kidogo then akamweka sofani akafungua hotpot akakata ugali na samaki akala.

Imefika saa 8 nikawa na safari ya kwenda kanisani,nikamweleza .nikaingia chumbani kwangu kubadili,akaja mbiombio akaniaga na kutoka.

Robo saa nami nikawa tayari nikamwaga msichana wangu wa kazi,nikamwachia na mtoto nikawasha gari nikatoka.

Wakati niko barabarani sauti ikanambia hebu pita hapo kwa baba nanihii kabla ya kwenda kanisani.Basi nikapaki gari jirani then nikatembea,kufika pale nikabisha kama dakika 5 ndo akafungua.

Nikaingia nikakuta kumbe anaishi na binti,nikamwuliza ndo huyu anayesababisha usitoe hata hela ya pampas za mwanao?nikamwambia mpigie simu mama yako tuongee akagoma.Basi nikatoka zangu nikarudi kwenye gari na kuendelea na safari yangu ya kanisani njiani nikidrive huku nalia kwa uchungu.

Nimefika nimechelewa kiasi,nikakaa kiti cha nyuma kabisa nikajiinamia nikilia,huku moyoni nikisema uko wapi Mungu wangu?mawimbi yananipiga,uko wapi unitet(,ni wimbo,niupendao).

Ibada imeisha saa 12 jioni nikarudi nyumbani kichwani nikiwa na mawazo tele.Nikakuta mwanagu analia nikamnyonyesha akalala.

Nimestuka muda huu nikamtazama mwanangu alivyolala kama malaika,ila kichwani nimeamka na resolution moja tu,kwamba from today mwanagu hana baba,mimi ndo baba na ndo mama yake.Nilitaka mpigia mamake ila nikaona yatakuwa yaleyale.Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu nitamlea mwanangu,naasume amekufa,and yes nimemwambia asifike kwangu tena.Kama ni mwanaye asubiri akifikisha 18 years atamtafuta.

Kama ni wewe mwanamke mwenzangu utafanyaje?kwanini mwanaume ukatae hudumia mwanao kisa starehe?
Wanawake wengine sijui akili mnaziweka wapi? We huna uwezo Wa kumlea mtoto mwenyewe paka uanze kumfundisha mtoto tabia mbaya?
Lea mwanao kwa amaani tuu, acha kujiumiza kichwa kutaka matumiz kutoka kwa baba yake.
Labda unataka mengine.
Unaenda kanisani kusali alafu unadanganya kiasi hicho? Kwamba baba kafa...subiri akue mtoto mueleze ukweli wake.

Kamuulize pasta wako juu ya Huo uwamuzi wako kama ni sahihi
 
Usifanye maamuzi ukiwa na hasira,tulia kwanza halafu jiulize jee unaweza kuishi bila yeye uwepo wake? moyo wako umekubali kua its OVER,vyovyote itakavyokua huyo ni mzazi mwenzio sisemi kama huwezi kusonga mbele bila yeye
ila jee unaposema basi unamaanisha au basi ya hasira?
Ikiwa umeamua kua utalea mtoto wako mwenyewe na humuhitaji sio kwa matumizi tuu bali hata kwa ushauri ntasema
sawa endelea mbele na maisha yako na usimtafute na hata akikutafuta mpotezee...

Nimeamua kwa dhati ya moyo wangu kabisa,nitamlea mwanagu,naomba Mungu anipe umri mrefu na aniwezeshe katika hilo.Sitokaa nikamtafuta tena iwe mvua iwe jua.
 
Lea mwanao dada wala huyo pimbi asikutishe. Hesabu alishadead..mzike kabisa! Huwezi kushindwa kumlea mtoto...trust me. Hata kama una kipato kidogo kiasi gani wewe mlee mwanao hivyo hivyo na utashangaa maisha yanasonga na mtoto anakuwa.
Acha kulia..na nakwambia tena usipoteze machozi yako kwa mwanaume asiyekuthamini hata siku moja. Furahia maisha kadri uwezavyo...furahi na mwanao. Hushindwi kitu nakuambia. Tena pimbi mwenyewe hata hajakuoa. Achana na huyo Shwain...mxiuuuuu

Ndio kwangu amekufa kabisa na nimemzika rasmi.Sifanyi haya kwa hasira,hapana ila natambua napaswa kuwa mwenye furaha niweze mlea huyu mtoto,na ili nifanikishe hilo sinabudi kumwondoa maishani mwangu.He is dead and buried.
 
Pole dear... This issue is very disturb and hurt kids most of the time.. I think umeuumia because you still love him and expected him to do More , but most of it at least to show a care for you and Baby.. At the end umeaambulia patupu from your expectations.. Dear don't cry or hurt yourself because of Him.. I do understanding unavyojisikia .... Inauma sana.. You probably feel as a failure or why you. Whatever the pain you have never feel regret because that baby came in this earth with reason , God appointed Him.. What I do advice you is : Move on with your life without baby Daddy.. Dont depend on Him 100% because you will get hurt and disapointment again.. Now ushajua who he is then try not to bother for him anymore.. Katika kumove on with your life dont tell your own son that his dad died , while He stills alive somewhere, thats not nice .. Since you go to church and read the Bible, pray for the healing and Erase those words by the Blood of Jesus , muaachie Mungu.. Lea mwanao Mama maana wewe ndio unauujua uchungu zaidi kuliko huyo Baby Daddy.. Focus on God and your son... Kazi yako ni kulea na ku show love to your son .. Akikua , akiuliza baba yake mwambie aliko if you will have information zake .. Kama hautazijua dont bother.. Dear ninachopendea boys , are always Mama's boy itachukua muda mmpaka yeye kukuuliza about his father.. Huyo Baby daddy akimmtaka mwanae mmpange wapi amuone mtoto .. To me I do advice you awe anakutana nae kwa Bibi mzaa Baba is better than kumuacha mwanao na huyo unknown step mother ... ( msichana wake ).. Akimaliza kuspend time nae kammchukue mwenyewe kwa bibi.. Epuka kuwa ukaribu na huyo Baby Daddy... Usiruhusu aje kwako hovyo hovyo , unless kama baby akiwa anaumwa sana .. Na wewe pia acha kwenda kwake, move on with your life and God will give the right man who will be the best husband and Father for your Son.. Good luck.. Thanks..

Asante sana dear,maneno yako yamenifariji sana.Nimekata mawasiliano naye,na kumzika rasmi.sitopanndikiza chuki yoyote kwa mtoto,ila akikuwa na kumuulizia daddy yake,jibu ni hilo kuwa,he dead a long time ago.
 
Ndio kwangu amekufa kabisa na nimemzika rasmi.Sifanyi haya kwa hasira,hapana ila natambua napaswa kuwa mwenye furaha niweze mlea huyu mtoto,na ili nifanikishe hilo sinabudi kumwondoa maishani mwangu.He is dead and buried.
Safi. Futa machozi na unyanyuke. Hushindwi kumlisha mwanao na kumsomesha pia unaweza. Utashangaa tu amefika chuo kwa jitihada zako tu mwenyewe. Hakuna unachoshindwa nakwambia.
wanawake muda wa kulia umeisha. You are strong than you think!
 
Back
Top Bottom