Mwanamme anataka mimi ndio nimjali

Mwanamme anataka mimi ndio nimjali

Habari wandugu?

Kuna dada nilimnasa mahali akilalama kuwa amepata rafiki wa kiume (mume wa mtu) mwezi Mei mwaka huu, huyo mwanamme anataka huyo dada ndie awe anamualika kutoka out na huyo dada ndie awe analipia vinywaji vyote na chakula. Na lingine alilalama kuwa wakiwa sehemu wanakunywa yule bwana akiwaona rafiki zake basi anamwambia mhudumu wapelekee wale kinywaji wanachokunywa na ana clear bill lakini hataki kununua vinywaji kwa ajili yao wawili.

Pia alisema kuwa, hata anapompigia simu, yule bwana anaongea kwa kifupi sana na kudai kuwa hapendi kuongea na simu muda mrefu lakini wakiwa wamekaa pamoja huyo bwana huwa anatumia muda mwingi kuwapigia simu ndugu zake na anaongea nao muda mrefu.

Mbaya kuliko yoyote anasema huyo bwana anataka yeye siku ya kubanjua amri ya sita huyo dada atafute room na kulipia.

Anasema kuna siku alimwambia kuwa yeye anasitisha uhusiano kwa kuwa anateseka sana kumpenda mtu ambaye hayuko wazi kama anampenda au hampendi, yule bwana kusikia hivyo akamtishia kuwa akimuacha atamuonyesha cha mtema kuni.

Mwenye nafasi ya kuchangia hebu tumshauri huyu dada
NAHUJA, wanaume wa kujari bado tupo bhana! Njoo huku usipate tabu.
 
Ttz la wadada wengi wanapenda
Sana uongo hua mkiambiwa
ukweli mna kataaa haya
Mnachokitafta ndo hicho mnakipata
Nasikia eti kwenye mapenzi "uongo" unaleta hamasa kuliko "kweli tupu"😉
 
NAHUJA, wanaume wa kujari bado tupo bhana! Njoo huku usipate tabu.
hahahaha, hayo maswahibu yamemkuta rafiki yangu sio mimi. hahahahaha. ila kama unajali hebu nirushie pesa kidogo, nadhani 900 itapendeza zaidi ukinitumia kwa eatelimane hahaha
 
Nasikia eti kwenye mapenzi "uongo" unaleta hamasa kuliko "kweli tupu"😉
Yaaah 90% maana Sasa ukisema
Ukweli utakataliwa na kuonekana
Muongo mkubwa

Sasa bhas uongo unanafac
kubwa sana kwenye mahusiano
 
Hapo mbona simple 1. uyo Dada anaacha kumpigia simu akimuuliza kwa nini anamjibu hana vocha akituma message hivo hivo labda akurecharge.
2. Akitaka outing unamwambia huna hela labda alipie.
3. Kugegedana uyo mume wa mtu ndio akatafute chumba.
4. Mkienda outing wewe pendekeza sehemu nzuri na za garama ukifika agiza vitu vya garama .
5. Asipotia akili na kutamani kukuwacha mwenyewe Fanya hivi
6. Kila siku wewe mueleze matatizo yako na umwombe pesa. Kila siku. Yani akipiga simu baada ya salamu wewe muombe pesa tuu ya saluni, pango, nguo, kuku, pizza, wine...
7. ASIPOBADILIKA NI PM.
Kwa mbinu hizi lazima mwanaume aingie mitini. Lakini, Hiyo namba 4 huoni kuwa itamgharimu yeye mwenyewe!
 
Umenikumbusha zamani sana kipindi hicho mtu ndo unaanza anza mapenzi !
Basi najisikia ufahari kinoma girlfriend akiniomba hela .......Halafu nikimtumia baadae nikikaa peke yangu roho inauma sana nikikumbuka mkwanja wangu![emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mapenzi haya......
 
Haha..ngoja nicheke kingereza! Mkuki kwa nguruwe, yan huyo mshkaji nikimjua namnunulia bia hd aseme bhaass!
 
Umenikumbusha zamani sana kipindi hicho mtu ndo unaanza anza mapenzi !
Basi najisikia ufahari kinoma girlfriend akiniomba hela .......Halafu nikimtumia baadae nikikaa peke yangu roho inauma sana nikikumbuka mkwanja wangu![emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mapenzi haya......
😛😛😛😛😛😛😛😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Anasema kuna siku alimwambia kuwa yeye anasitisha uhusiano kwa kuwa anateseka sana kumpenda mtu ambaye hayuko wazi kama anampenda au hampendi, yule bwana kusikia hivyo akamtishia kuwa akimuacha atamuonyesha cha mtema kuni.

Mwenye nafasi ya kuchangia hebu tumshauri huyu dada
Kwanza huyo mtema kuni alionaga nini? Baadaye ndo ntachangia
 
Back
Top Bottom