Habari wandugu?
Kuna dada nilimnasa mahali akilalama kuwa amepata rafiki wa kiume (mume wa mtu) mwezi Mei mwaka huu, huyo mwanamme anataka huyo dada ndie awe anamualika kutoka out na huyo dada ndie awe analipia vinywaji vyote na chakula. Na lingine alilalama kuwa wakiwa sehemu wanakunywa yule bwana akiwaona rafiki zake basi anamwambia mhudumu wapelekee wale kinywaji wanachokunywa na ana clear bill lakini hataki kununua vinywaji kwa ajili yao wawili.
Pia alisema kuwa, hata anapompigia simu, yule bwana anaongea kwa kifupi sana na kudai kuwa hapendi kuongea na simu muda mrefu lakini wakiwa wamekaa pamoja huyo bwana huwa anatumia muda mwingi kuwapigia simu ndugu zake na anaongea nao muda mrefu.
Mbaya kuliko yoyote anasema huyo bwana anataka yeye siku ya kubanjua amri ya sita huyo dada atafute room na kulipia.
Anasema kuna siku alimwambia kuwa yeye anasitisha uhusiano kwa kuwa anateseka sana kumpenda mtu ambaye hayuko wazi kama anampenda au hampendi, yule bwana kusikia hivyo akamtishia kuwa akimuacha atamuonyesha cha mtema kuni.
Mwenye nafasi ya kuchangia hebu tumshauri huyu dada