Mwanamme anataka mimi ndio nimjali

Mwanamme anataka mimi ndio nimjali

Habari wandugu?

Kuna dada nilimnasa mahali akilalama kuwa amepata rafiki wa kiume (mume wa mtu) mwezi Mei mwaka huu, huyo mwanamme anataka huyo dada ndie awe anamualika kutoka out na huyo dada ndie awe analipia vinywaji vyote na chakula. Na lingine alilalama kuwa wakiwa sehemu wanakunywa yule bwana akiwaona rafiki zake basi anamwambia mhudumu wapelekee wale kinywaji wanachokunywa na ana clear bill lakini hataki kununua vinywaji kwa ajili yao wawili.

Pia alisema kuwa, hata anapompigia simu, yule bwana anaongea kwa kifupi sana na kudai kuwa hapendi kuongea na simu muda mrefu lakini wakiwa wamekaa pamoja huyo bwana huwa anatumia muda mwingi kuwapigia simu ndugu zake na anaongea nao muda mrefu.

Mbaya kuliko yoyote anasema huyo bwana anataka yeye siku ya kubanjua amri ya sita huyo dada atafute room na kulipia.

Anasema kuna siku alimwambia kuwa yeye anasitisha uhusiano kwa kuwa anateseka sana kumpenda mtu ambaye hayuko wazi kama anampenda au hampendi, yule bwana kusikia hivyo akamtishia kuwa akimuacha atamuonyesha cha mtema kuni.

Mwenye nafasi ya kuchangia hebu tumshauri huyu dada
Dah...ningemshauri....lakini naogopa dhambi[emoji87]
 
amejaribu kumchunguza nyeti zake?unaweza kukuta ni mwanamke mwenzie sema ana sura ya kiume,tabia zote alizoainisha ni za kike ila bado kutuambia hiyo sehemu moja tu ya nyeti zaye ili tumalize mjadala
hahahahahahah hakika umeuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kama anajua ni mume wa mtu, anataka amuweke wazi nini hapo sasa. Yeye aangalie ustarabu wake huyo baba wala hana mpango nae sana anafurahia hizo huduma tu za bure, kwa serikali hii ya Magu upate mtu wa kukulea unafikiri mchezo
yaani hii itafungua akili wengi, ukishajua una date na mume wa mtu ujue tu kwamba hapa unajipunguzia tu genye na hakuna faida yeyote. huwa nashangaa wanaojisifia kuwa na waume za watu, kiukweli HAILIPI
 
Dahhhh..... Haya mahusiano siku hizi ni full stress...... Kwa nini lakini? Pole sana kaka maana naona yamekukuta ya aina yake..... Pole sana sana.....!!!!!
Naomba unitoe tongo tongo, ina maana huu uzi ulishaletwa humu na mtu anaitwa Chikira halafu tena Nahuja? au ni mutu moja hapo sielewi

tehteh okoa tu jahazi usinicheke
 
itafika siku huyo manzi ndio atakuwa anatoa pesa za matumizi nyumbani kwa mshikaji, ila jamaa kauzu sana...
 
Naomba unitoe tongo tongo, ina maana huu uzi ulishaletwa humu na mtu anaitwa Chikira halafu tena Nahuja? au ni mutu moja hapo sielewi

tehteh okoa tu jahazi usinicheke
Nikipata muda nita-compare between the two. Thanks
 
yaani hii itafungua akili wengi, ukishajua una date na mume wa mtu ujue tu kwamba hapa unajipunguzia tu genye na hakuna faida yeyote. huwa nashangaa wanaojisifia kuwa na waume za watu, kiukweli HAILIPI
Sijui huwa wanawaza nini kwa kweli!!!
 
Anatoka na mume wa mtu anategemea nini...tena yalipaswa yamkute kuliko hayo!






Mungu anisamehe tu kwa kweli..
 
yaani hii itafungua akili wengi, ukishajua una date na mume wa mtu ujue tu kwamba hapa unajipunguzia tu genye na hakuna faida yeyote. huwa nashangaa wanaojisifia kuwa na waume za watu, kiukweli HAILIPI
kweli kabisa jje's
 
Naomba unitoe tongo tongo, ina maana huu uzi ulishaletwa humu na mtu anaitwa Chikira halafu tena Nahuja? au ni mutu moja hapo sielewi

tehteh okoa tu jahazi usinicheke
Nilibadili jina kutoka CHIKIRA sasa najiita NAHUJA
 
Back
Top Bottom