Mwanamke wa namna hii hakufai asilani na wala Usipoteze muda wako juu yake

Ahlan wa sahlan

Kuna wanawake wa aina nyingi hapa duniani.Kuna baadhi ya tabia zao zikianza kujionesha katika mahusiano yenu jua kuwa taa nyekundu imeshawaka na yakupasa ushtuke na usepe mapema.

Mwanamke ambae hakusalimii wala kukujulia hali wala kukutakia usiku mwema mpaka umuanze wewe jua kabisa kuwa haupo kwenye moyo wake. Hapa ndugu unatakiwa ushtuke mapema na ikiwezekana temana nae.

Mwanamke ambae ukimtumia sms zako anazisoma halafu hakujibu ontime kwa kisingizio kuwa yupo busy na kazi , na anajibu anavyojisikia yeye labda baada ya siku moja su hata wiki baada ya kuzisoma jua kuwa huna umuhimu kwake ,hivyo inakupasa ujiongeze.

Mwisho ni mwanamke ambae ukiona anakutafuta au kukujulia hali yako ni pale tu anapokuwa amekwama kiuchumi.Huyu temana nae na umfungie vioo kabisa maana hakufai ,umuhimu wake kwako ni katika masuala ya pesa tu.
Ukitaka uhuru na mambo mengine yaende nenda kanunue na usepe zako kwa nyakati hizi hali ni mbaya
 
Kwahiyo mkuu unamaanisha hizo tabia ni kwa mwanamke tu? Mwanaume kwake ni sawa kuwa hivo?kiukweli kabisa ukimpenda mtu yaani unatamani kila saa muongee, mimi napenda kuongea, text kujuliana hali nk . Ila kama humpendi mtu hata ukiona text yake hushtuki kabisa. Hii ni kwa wote lkn si wanawake pekee
Mada yangu imelenga katika mrengo huo ila yes nakubaliana na ww pia kuwa inaweza kuwa vice versa
 
Kuna ukweli hapa kumbe Mimi huyu wangu hapa hatutoboi

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
Stuka mapema kabla hujawa mtumwa juu yake! Binadamu huwa tuna hulka ya kuhangaika vile vitu adimu. Kama hakupi attention yake kwako,wala usijihangaishe kumfanya atambue uwepo wako, we mkaushie halafu anza maisha mengine. Btw , wapo wazuri wengi zaidi yake
 
Ok but why ulenge upande mmoja tu wakati wote wanahusika ? Umeeleweka mkuu.
Unapotaka kutoa hoja pendelea kujielezea ww km ww na sio kuanza kuulzia upande wa pili, Mada imeelezea tabia za wanawake unaanza kusema et hata wanaume wako hvyo...stick kwenye topic husika ......

Jifunze kujenga hoja pasipo kutafuta upande wa kuegemea
 
Unapotaka kutoa hoja pendelea kujielezea ww km ww na sio kuanza kuulzia upande wa pili, Mada imeelezea tabia za wanawake unaanza kusema et hata wanaume wako hvyo...stick kwenye topic husika ......

Jifunze kujenga hoja pasipo kutafuta upande wa kuegemea
Mkuu acha kudandia gari kwa mbele wewe, umeona comment yangu ya hapo juu nyingine? nimeelezea ndiyo nikaulizia kwamba wanaume wao ni sawa? kosa langu ni lipi hadi unifundishe kustick kwenye topic? bila hata kuwaza kwa mapana yake?.

jifunze pia kudadavua mambo kwa mapana siyo kustick kwenye topic tu, kwani topic ni msaafu huo hautakiwi kuchambuliwa,kukosolewa nk?
 
Back
Top Bottom