Mwanamke usimuulize mwanaume swali hili

Mwanamke usimuulize mwanaume swali hili

Mm nafanya biashara natumia watsapp kuwatumia wateja picha za bidhaaa mpya na inaongeza wateja, we kaa hapo ukijua kila kitu matumizi yake ni uvunguni mwa miguu tu.
 
hii namba ya charminglady imentesa kweli kuipata. Asante mleta mada umenirahsishia kazi... Mamaaaa charminglady ntakutumia kipenseli changu kwenye wozapu eee.
 
Last edited by a moderator:
Isiwe tabu bwanaaa...acha na mie niungane nao haooo wafuata upepo wa teknolojia...na nimeingia kwa kishindo nipo maeneo yafuatayo:-
1- yahoo messenger
2-face book
3- twitter
4- badoo
5- topface
6-tango
7-viber
8-whatsup-ma-niggaa
9-instagram
10-jamiiformums

kwani wee mleta uzi unasemaje?..enheee?..sema sasaaa...unasemajeee?

Na kwa taarifa yako nimeingia huku baada ya kuchoshwa na yafuatayo
1- p.o. Box barua hazifiki kwa wakati
2- fax mara network hakuna
3- telegram ndio zoote zishakufaga
4- simu hasa tigo network hazisomi full kuambiwa namba unayopiga kwa sasa haipatikani wakati unayo na ipo hewani
5- ku-scan ma-picha kisha kuwatumia watu kwa mail usumbufu kisa mgawo wa umeme
6- hakuna jinsi ya kumpigia mtu simu na kumuona live zaidi ya tango
7- kupata matukio yaliyojiri moja kwa moja mpaka itv na tbc wajiunge nayo ni kwenye taarifa ya habari ya usiku

na mengineyo meeeengiiiiii yenye kukera zaidi.

karibu ulimwengu wa kina steve jobs..upate dunia kwenye viganja vyako.
 
Of couse sioni haja ya kumuuliza mtu kama nna namba yake si naiangalia tu kama upo or not.
BTW alietengeneza hizi app alikua na maana nzuri tu ila watu wanazi spoil
 
Hilo lina ukweli kabisa,na tabia hiyo inakera sana sana yani. Unachat na mtu vizuri sawa,anakuomba umtumie picha yako,unamtumia tu kiungwana. Bado anaona haitoshi anataka tena umtumie na nyeti zako. Mi hua nakosa jibu kwamba nikisha mtumia hizo ili iweje sasa zitamsaidia nin? Hii mitandao jamani tuitumie kwa faida
Kwenye misafara ya mamba hata kenge wamo. Ni bora kutofautisha kenge na mamba. Karibu njinjo
 
Kwa upande wangu Whaatsap Application haina tofauti na text msg...Kwa sababu gani nasema hivyo...Ili uweze kuwasiliana na mtu/raia via Whaatsap lazima uwe umesave contact ya huyo mtu kwenye phonebook yako.Kwa hiyo hakuna sababu ya kulalamika kwamba unajitoa whaatsap kama kwenye phonebook yako umesave watu makini.
 
Binafsi natumia watsaap na sioni ubaya wake...ni rahisi kutuma na kupokea picha...
Kama una biashara watsaap ni nzuri pia unaweza tuma picha za bidhaa ulizo nazo kwa wateja kiurahisi..
Watuma vipenseli vyao wapo kila kona.
Akituma nakiangali kisha nakitupia kapuni....
 
miss chaga upo whatsup? ashadii je? teh teh wenye vimeo najua hamuipendi coz huwezi kutoa update za uongo mtashikwa.
 
Umeona eeh! Bora ujue hata matumizi yake ila usiitumie, sio kila anayekuuliza una watsapp we unammind, kumbe umepitwa na technologia.

Mi ninayo, mambo ya kutumiana picha za watoto wetu (unajua tena uzazi wa kwanza kwa picha eeh!), inasaidia kweli, sio mpaka mambo ya email.

Ni pm namba yako,tehe tehe
 
Hapo ndo utaona kumbe unayemuheshimu hafai kuheshimiwa, yan unakuta jitu unaliheshimu sana af linakutumia "kipenseli chake" bila hata chembe ya aibu

What??????? kipenseli is what?
 
Mwisho wa siku tatizo sio watsAap...
Tatizo ni wewe utakavyoipokea na utakavyoitumia.
Na ukiniuliza kama natumia wala simaindi na namba nakupa...na ukiniuliza nakujibu bila kinyongo.
Ukianza kunitumia kibamia chako nakublock tu...case closed.
Wanayoyafanya wengine watsAap hayanihusu ninachofanya mimi ndio kinanihusu...
 
Back
Top Bottom