Mwanamke usimuulize mwanaume swali hili

Mwanamke usimuulize mwanaume swali hili

Hilo lina ukweli
kabisa,na tabia hiyo inakera sana sana yani. Unachat na mtu vizuri
sawa,anakuomba umtumie picha yako,unamtumia tu kiungwana. Bado anaona
haitoshi anataka tena umtumie na nyeti zako. Mi hua nakosa jibu kwamba
nikisha mtumia hizo ili iweje sasa zitamsaidia nin? Hii mitandao jamani
tuitumie kwa faida

Kumbe kuna mengi huko!!
 
ndo kusema mimi nipo nje ya kujua nini kinaendelea?
yaani mpaka hapa sijajua nini ubaya wa Whatsapp.....
maana naitumia sana kuwasiliana na watu maana sms zimekuwa expensive kwangu, lol! LIKUD naomba unifafanulie nini ubaya wake?

Whatsapp haina shida shida ni msichana unapokutana na mwanaume for the first time na moja kwa moja unamuuliza kama yupo whatsapp or else. Thats my point
 
mie sijui ila me nipo viber, whats app, we chat a lot of thing am benefits of it sina tatizo....
 
Whatsapp haina shida shida ni msichana unapokutana na mwanaume for the first time na moja kwa moja unamuuliza kama yupo whatsapp or else. Thats my point
samahani kwa maswali....
huyo jamaa wanakuwa wamebadilishana namba? au huyo binti anamwomba jamaa namba na kumwuliza kama yupo whatsapp?
 
samahani kwa maswali....
huyo jamaa wanakuwa wamebadilishana namba? au huyo binti anamwomba jamaa namba na kumwuliza kama yupo whatsapp?

umekutana na msichana sehemu mlikuwa hamfahamiani, labda mkafahamishwa kupitia marafiki, badaye mkapena namba halafu all of a sudden she jumps on telling the whatsapp thing
 
umekutana na msichana sehemu mlikuwa hamfahamiani, labda mkafahamishwa kupitia marafiki, badaye mkapena namba halafu all of a sudden she jumps on telling the whatsapp thing

Inakeara kwakweli!!!!!!
 
umekutana na msichana sehemu mlikuwa hamfahamiani, labda mkafahamishwa kupitia marafiki, badaye mkapena namba halafu all of a sudden she jumps on telling the whatsapp thing
ukilaza nao ni mzigo wa miiba....
kwani kama una namba ya mtu si unajua kama yupo whatsapp bila hata kumwuliza?
 
Whatsapp ikitumika vizuri ni app nzuri tu mfano. Mimi nachat na Sister wangu kila siku thru whatsapp kwasababu tuko nchi tofauti, imerahisisha mawasiliano.

Ila "upo whatsapp" ikiwa ni moja ya swali mwanzoni mwa mazungumzo jua akili ya huyo msichana imejaa ukungu.

Acha kubana wewe! Unachat vipi na sister wako kila siku kila mara? Unataka siku ya mwisho akupende wewe badala ya boyfriend wake sio?

Hayo ndio matumizi mabaya, mpe muda wa kuchat na wanaume bana, ebu kwanza nipe namba yake nimkataze kuchat na wewe kila siku, eboo!
 
ukilaza nao ni mzigo wa miiba....
kwani kama una namba ya mtu si unajua kama yupo whatsapp bila hata kumwuliza?

Umeona eeh! Bora ujue hata matumizi yake ila usiitumie, sio kila anayekuuliza una watsapp we unammind, kumbe umepitwa na technologia.

Mi ninayo, mambo ya kutumiana picha za watoto wetu (unajua tena uzazi wa kwanza kwa picha eeh!), inasaidia kweli, sio mpaka mambo ya email.
 
mimi siku hizi nimeshasahau kutuma sms, kama huna whatsapp tutawasiliana kwa call, lol!
 
ooh kumbeee
Whatsapp haina shida shida ni msichana unapokutana na mwanaume for the first time na moja kwa moja unamuuliza kama yupo whatsapp or else. Thats my point
 
huhuhuuu limekupata nn LIKUD .
 
Last edited by a moderator:
mimi siku hizi nimeshasahau kutuma sms, kama huna whatsapp tutawasiliana kwa call, lol!

Whatsapp inahusika bana, kwanza uzuri wake inahusisha phone book yako, ambaye hana namba yako hawezi kuona hata profile yako, picha unazomtumia mtu mmoja mwengine haoni, so ni kama vile kumtumia mtu SMS ya kawaida tu. Sio kama facebook ambapo yeyote anaweza ona mambo yako.

Tatizo ni ushamba na kutotaka kujua nini technolojia imebeba, sasa utakuta huyu mtu akitaka kutuma picha anahangaikaa, mara kuscan, mara kuattach kwenye email, mara kutuma, na MB 4 kwenda mbele haziendi kwa email.
 
Back
Top Bottom