Mwanamke na haki za ndoa

Mwanamke na haki za ndoa

CONCHEY

New Member
Joined
May 9, 2026
Posts
1
Reaction score
1
TAMU YA KESI ILIYO AMULIWA NA ( SUPREME COURT OF INDIA) ANNA SAURABY DUTT VS. LIEUTENANT COLONEL CIVIL APPEALNO.25076 0F 2024

MAJAJI WALIELEZA YAFUATAYO KATIKA MAHAKAMA HIYO...

Mwanamke aliyesoma na mwenye sifa za kitaaluma hawezi kutarajiwa kufungiwa ndani ya mipaka migumu ya majukumu ya ndoa pekee.

Ndoa haifuti utu wake binafsi, wala haiusishi utambulisho wake chini ya ule wa mwenzi wake wa ndoa. Ni wajibu wa mume na mke kwa pamoja kuimarisha mahusiano yao ya ndoa kwa namna inayoheshimu matarajio na ndoto za kila mmoja, na si mmoja wao kutumia mamlaka yake kupanga maisha ya mwenzake kwa upande mmoja tu.

Tupo karne ya 21, lakini bado juhudi za mwanamke mwenye taaluma ya kitaaluma kuendeleza kazi yake na kuhakikisha familia inakuwa na mazingira salama na yenye utulivu kwa ajili ya uchumi wa familia pamoja na malezi ya watoto wake, zimechukuliwa kama kitendo cha ukatili na kutelekeza ndoa.

“Katika kesi hii mlalamikaji alikuwa ameweka juhudi kubwa na gharama nyingi ili kupata shahada ya Udaktari wa Meno. Hivi Katika dunia ya sasa ambapo wanawake wanaendelea kupiga hatua kubwa sana katika nyanja mbalimbali, kwa sababu tu mume alikuwa afisa wa jeshi aliyepangiwa kufanya kazi eneo la mbali, kutegemea kwamba mke hangeweza hata kufikiria kuendelea na taaluma yake ya Udaktari wa Meno, ni ishara ya fikra za kizamani, za kimwinyi na utumwa, zinazorudisha maendeleo nyuma.

Note: Wanaume tubadilike tuwape wenzi wetu Fursa za kuendeleza taaruma zao , biashara Kwani duniani Kote Wanawake wamedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa wa kibiashara na kutengeneza vipato vya familia, hivi tuachane na fikra hasi na tufungue akili zetu kwendana na kasi ya kiuchumi, kwendana na kasi ya jinsi mambo yanavyo kwenda ..✍️
 
Back
Top Bottom