Bado hujanionyesha mahali ambapo panaonyesha kwamba Eva au Hawa alimhadaa Adam, hapo panasema tu kwamba alimpa mumewe naye akala, hata hivyo Adama alikuwa na uwezo wa kukataa kula na kumkumbusha eva kwamba tulikatazwa kula huo mti wa katikati. Kumbuka hapa sizungumzii swala la Eva kutangulia kula tunda bali napinga kusingiziwa kumhadaa Adam au kumshawishi kama tulivyoaminishwa.
Lakini pia Mungu alimuumba Adam na ndipo akamuumba Eva kutokana na ubavu wa Adam, kama maandiko ya hizo dini mbili maarufu hapa nchini yanavyosema, na pia maandiko hayo yanasema kuwa huyu Adama ni kichwa cha nyumba, yaani ndiye kiongozi, sasa kwa kuwa kiongozi si alipaswa kumuongoza Hawa au Eva. Sasa ilikuwaje akapewa tunda ambalo waliambiwa wasile yeye akajitwalia na kula bila kukataa na kumkataza Eva au Hawa akiwa kama kiongozi wake?