Mwanamke anapobebeshwa yasiyomuhusu!

Mwanamke anapobebeshwa yasiyomuhusu!

Hivi Adam hakuumbwa na ubongo na hakuwa na uwezo wa kufikiri

Zinduna hivi unajua ni tunda gani linazungumziwa hapo? Nini Adam hakwenda shule, maprofesa na wanazuoni hawana ujanja wanapopewa ofa ya hilo tunda. Kiukweli Hawa ndo alimpa Adam tunda vinginevyo, angejitetea kuwa alibakwa na Adam.
 
Zinduna ukiendelea kusoma kifungu cha 9 na kuendelea bado utaona kuwa mwanamke ndiye aliyeleta kadhia yote...

Soma kwa makini maelezo yaliyo katika rangi nyekundu...

9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?

10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.

11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.

13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Umeona hata huo utetezi wa Adam ulikuwa ni wa kuepuka lawama na hivyo ndiyo wanaume wengi walivyo haa leo hii jambo lolote likineda hovyo lawama zinaelekezwa kwa mwanamke.
 
Quran imewataja wanawake hivi;- "hakika hii ni miongoni mwa vitimbi vyenu wanawake kwani vitimbi vyenu ni vikubwa mno" (surat yusuf). Sio Adam tu alieshawishiwa na mwanamke, umemsahau Yusuf? Mke wa mfamle alimfanyia mengi mpaka akafungwa yusuf bila kosa lolote, wanawake ni viumbe waajabu sana
Huu nao ni uongo mwingine

CC: FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Kimsingi wanyama wote wana lugha na kwa namna Mungu alivyomuumba mtu wa kwanza ambaye ni Adamu, alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na kila mnyama hivyo suala la nyoka kuongea na Adamu wala lisikushangaze.

Pili, shetani ni roho yaani hana mwili.
Ili kutimiza lengo lake la kupotosha uumbaji wa Mungu, alitumia mwili wa nyoka "vessel" ili apate kuongea na mtu (Hawa).

Hivyo kwa jinsi ya mwili ni nyoka aliyekuwa akiongea lakini kwa jinsi ya roho ni shetani aliyekuwa akionge.

kwa hiyo unataka kutuambia kwamba zamani nyoka alikuwa anaongea?

we huoni kwamba kuna lugha ya picha hapo?
 
Hivi hilo tunda ni lipi?ni kitu gani?
Zinduna soma kwa makini maandishi mekundu...pia elewa maongezi yalianza baina ya nani na nani?

Mwanzo 3

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.

4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
 
Last edited by a moderator:
Quran imewataja wanawake hivi;- "hakika hii ni miongoni mwa vitimbi vyenu wanawake kwani vitimbi vyenu ni vikubwa mno" (surat yusuf). Sio Adam tu alieshawishiwa na mwanamke, umemsahau Yusuf? Mke wa mfamle alimfanyia mengi mpaka akafungwa yusuf bila kosa lolote, wanawake ni viumbe waajabu sana

Na kwenye bible kuna kidemu kinaitwa Delila. kilimseduce Samson mpaka akachemka. Zinduna hajawahi ona mahausigelo wanavyowapelekesha mabosi wao tena wasomi tu, anashangaa Adam kushawishiwa na Eva.

Lile tunda halina mwanamme mjanja dhidi yake.
 
Last edited by a moderator:
Nmecheka sana lugha ya picha hahaa lol...nyoka nyoka nyoka nyoka.
kwa hiyo unataka kutuambia kwamba zamani nyoka alikuwa anaongea?

we huoni kwamba kuna lugha ya picha hapo?
 
Kimsingi wanyama wote wana lugha na kwa namna Mungu alivyomuumba mtu wa kwanza ambaye ni Adamu, alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na kila mnyama hivyo suala la nyoka kuongea na Adamu wala lisikushangaze.

Pili, shetani ni roho yaani hana mwili.
Ili kutimiza lengo lake la kupotosha uumbaji wa Mungu, alitumia mwili wa nyoka "vessel" ili apate kuongea na mtu (Hawa).

Hivyo kwa jinsi ya mwili ni nyoka aliyekuwa akiongea lakini kwa jinsi ya roho ni shetani aliyekuwa akionge.

ahsante mkuu kwa maelezo mazuri!

swala ambalo linaniwia vigumu sasa ni hili.

kama malaika anaweza kujidhihirisha na kuonekana kwa wanadamu, kwanini shetani yeye hajidhirishi? kwanini aje kwa maumbo ya vitu vingine kama mizimu na viumbe vingine kama nyoka?
 
Na kwenye bible kuna kidemu kinaitwa Delila. kilimseduce Samson mpaka akachemka. Zinduna hajawahi ona mahausigelo wanavyowapelekesha mabosi wao tena wasomi tu, anashangaa Adam kushawishiwa na Eva.

Lile tunda halina mwanamme mjanja dhidi yake.
Kwa hiyo unathibitisha hapa kwamba wanaume ni dhaifu.
Au?
 
Last edited by a moderator:
Umeona hata huo utetezi wa Adam ulikuwa ni wa kuepuka lawama na hivyo ndiyo wanaume wengi walivyo haa leo hii jambo lolote likineda hovyo lawama zinaelekezwa kwa mwanamke.

Labda mwenzangu Kiswahili kinakupiga chenga, nilifanya makusudi kuweka mtiririko wa maongezi ya kisa kizima.

Adamu na Hawa tunaambiwa walikuwa ni mwili mmoja, kwa mantiki kuwa mmojawapo akiona jambo ni zuri na lapendeza basi mwingine hana sababu ya kukinzana.

Ukisoma vizuri aya ya sita inathibitisha hilo ndio maana hata Adamu hakuwa na upinzani wowote alipopewa tunda na mkewe.

Sidhani kama kilichotokea wakati huo kinapaswa kulinganishwa na hali ya sasa, udhaifu wa Hawa au Adamu hauendani na udhaifu wa sasa.
 
Umeona hata huo utetezi wa Adam ulikuwa ni wa kuepuka lawama na hivyo ndiyo wanaume wengi walivyo haa leo hii jambo lolote likineda hovyo lawama zinaelekezwa kwa mwanamke.

Bisha kwa kuweka point zenye ujazo wa kutetea hoja zako haya maswala ni mapana yanataka maelezo yaliyo shiba bi dada.
 
Zinduna soma kwa makini maandishi mekundu...pia elewa maongezi yalianza baina ya nani na nani?

Mwanzo 3

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.

4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Hapo mwisho kwenye red: Kwamba Eva alikula kwanza, then akampa Adam nae akala:

My take: Eva alifanywa kwanza, then baada ya kuexperience Ile ladha ndio akampa na adam. Hii ina manisha Eva alifanya kwanza na mtu mwingine sio Adam. Na Huyo mwingine ni Huyo nyoka, which is Lucifer. Kwa hiyo mwanamke ni msaliti wa enzi. Na ndivyo walivyo hata leo. No matter what
 
Last edited by a moderator:
Kumbukeni na Ile stori ya samsoni na Delilah. Wanawake wana matatizo sana. Kwa waliosoma Bible vizuri mtaweka hapa ule mstari unaowasihi wanaume kuishi na wanawake kwa umakini sana.
 
Back
Top Bottom