Mwanamke aliniharibia kabisa maisha yangu, hawa viumbe hatari sana

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Aug 9, 2022
1,811
4,920
Wakuu mu hali gani? Nashukuru mie mzima wa afya.

Kuna kisa nimekuwa nacho kwa muda mrefu, sikuwahi kushare humu. Niliandika kiufupi tu ila naona ni vizuri nikashare kwa ukubwa ili tupate kujifunza na wengine.

Sikuwahi kujua kama mwanamke anaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa maisha ya mtu, inawezekana ni sababu ya mapenzi anayokupa kabla mambo hayajaharibika, unaona kwa upendo anaokuonyesha hawezi akawa mbaya kwako.

Ni miaka kadhaa imepita, baada ya kumaliza kusoma nilibahatika kupata mkataba kufanya kazi kampuni X. Baada ya maisha kuanza kuwa kwenye mstari niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja mrembo sana, mkarimu na mwenye kujali.

Familia aliyotokea ilikuwa ni ya kawaida tu, ilipambana kumsomesha lakini haikumfikisha kwenye level ya ndoto zake kulingana na hali ya kipato. Kwakuwa nilimpenda sana, nilifanya taratibu za kutaka kumuoa. Nilienda kwao nikatoa kiasi fulani cha pesa ili niishi na mtoto wao. Walinikubalia, tena kwa furaha kubwa sana. Kiasi cha mahari sikutoa chote, niliahidi nitamalizia baada ya muda fulani. Hilo likafanikiwa.

Nilimpenda sana binti, nae alirespond the same. In short niliona nimepata furaha ya moyo, tukapata mtoto wa kiume na kweli nilienjoy.

Siku zote Binti alikuwa akinieleza kwa uchungu namna alivyotamani kusoma ila uwezo wa kifedha haukuruhusu, huku akisisitiza bado anatamani kufikia lengo. Sikuona vibaya, kwakuwa tayari ni mke kwangu nikampeleka Chuo husika cha fani husika nikalipa ada na akaanza rasmi kusoma.

Siku hazikukawia alimaliza. Baada ya kumaliza tu, akawa amepata kazi pia kwenye shirika moja lisilo la kiserikali hapahapa mjini. Tuliendelea kuishi kwa furaha kama kawaida.

Kuna changamoto ilikuja kutokea pale kazini kwangu ambayo sitoitaja hapa, ilipelekea mimi na wafanyakazi wengine Watatu kupoteza kazi. Hapa ndipo mambo yalipoanza kuzua utofauti. Nilipambana sana kufix hilo jambo sababu limekuja ghafla sana pasipo mategemeo, ilikuwa ni case kubwa iliyopelekea kuyumba kuanzia uchumi hadi mahusiano. Nilipoteza sana fedha kwenye kufix hilo ila hakukuwa na mafanikio.

Rasmi nikaanza kuonekana mzigo kwa familia yangu. Sikuweza tena kutoa huduma kama ilivyokuwa mwanzo, nikashindwa kuyamudu majukumu yangu kama awali. Ilibidi mwanamke aanze kufukia baadhi ya mapungufu sasa sababu hakukuwa na namna.

Msiombe kufikia hatua hii wakuu, ni fedheha sana. Nilianza kudharaulika na mwanamke. Maneno yakawa mengi, ikafikia hatua akawaambia hadi kwao kuwa amechoka kuwa na mwanaume asiye na mchango wowote. Wazazi nao wakasahau kabisa hata mazuri yangu, wakaanza kumshinikiza aondoke kwangu. Akawa mjeuri na kunitishia kuondoka aone ntaishije, ina maana ninaishi sababu yake, bila yeye ntateseka sana.

Kuna pesa nilikuwa nikiihifadhi sehemu sikutaka kuigusa kwa hali yoyote ile sababu nilikuwa na lengo la kuja kufungua biashara. Pesa hiyo ilikuwa ni nje na akiba ambayo niliitumia kufix mambo ya kazini. Nilipoona nimeshindwa kuvumilia fedheha na maneno ndani, ikabidi nianze kuitumia kutafuta kazi nyingine kwa kuhonga sehemu tofauti tofauti ili niingizwe kwenye kazi kivyovyote, nadhani hapa nilifanya kosa kubwa.

Ni kwakuwa akili haikuwaza kwa utulivu, nilitaka solution ya haraka kumbe ndio naharibu. Nilijikuta napoteza hela zaidi na zaidi pasipo mafanikio. Nikaanza kuchanganyikiwa baada ya kuona hela ya mwisho ndio naiharibu vile bila mafanikio. Nilianza kukonda sasa. Mke hakunizingatia tena kama mumewe, nikawa rough sababu hanijali.

Kilipobaki kiasi kidogo nikaona sio kesi, ngoja nijilipue kwenda mikoani huko kupambana upya sababu kwa pale ingekuwa ngumu kwangu. Nikaacha kiasi kadhaa kwa wife nikamwambia naenda kupambana, nitarudi. Nikatembea.

Hazikupita hata siku tano tangu niondoke, nikaanza kupokea simu za majirani kuuliza mbona ninahama kimyakimya? Ikawa taarifa ya kushangaza sana kwangu, sababu sitambui hilo. Nikampigia simu wife, akadai anaondoka zake. Hawezi kukaa na mtu asiyeeleweka, eti hata akiugua serious mtoto au yeye au changamoto yoyote kubwa nitawasaidia vipi.

Aisee nililia, sikujua hata wapi anaelekea. Nikapiga simu kwao ila ni kama hakuna aliejali, ni kama walikuwa sehemu ya mpango huo. Nikapiga simu Nyumbani kumueleza mama na baba, kwakuwa walikuwa wanajua fukuto lililokuwepo kwangu tangu nipoteze kazi waliishia kunipa pole na kuniambia nikaze moyo, wala nisihangaike nae huyo mwanamke. Nipotezee tu. Ilikuwa ngumu. Hata nilipoenda sikufanya kilichonipeleka. Niliishia kurudi tena kwangu, nikakuta kimesombwa kila kitu. Hii isikie tu kwa mwenzako, hapo sina hata mia.

Hapo ndipo nikaamini ukipoteza kazi hakuna wa kuhangaika na wewe. Utapoteza kila kitu. Nilipoteza kuanzia mke, mali zangu na hata wale marafiki niliowahi kuwa nao sio nyumbani wala kazini. Niliishia kusemwa tu na hakuna aliyejaribu kunisaidia.

Naweza sema nilikuwa kama nimewehuka, nilikuwa mchafu, mzururaji, full kulia tu. Nilijuta kumjua yule mwanamke, sababu sidhani kama kupoteza kazi ndio alitakiwa kunifanyia vile. Alipaswa awe faraja yangu, atulize akili yangu ili niwaze kwa utulivu namna ya kupata tena kazi ila ndio akanivuruga nikarudi hadi zero tena.

Nilikaa almost 7 Months kwenye hali ile. Watu walijua nimeshachanganyikiwa japo mimi nilijua niko sawa kabisa. Hawakunizingatia isipokuwa wazazi wangu, nawashukuru sana. Sikukata tamaa.

Nilikuja kupata kazi kampuni nyingine kwenye Mradi wa Bwawa la Rufiji. Nilijiapiza kupiga kazi kwa uchungu sana. Nimefanya kwa takribani mwaka na nusu hadi kufikia mwezi wa nane mwaka huu nikamaliza. Nimerudisha maisha yangu kwenye mstari kabisa. Nina furaha na nguvu nyingi.

Muda wa kumaliza kule ulipokaribia, ni kama mwezi wa tano nilituma CV zangu jijini Mwanza kwenye kampuni moja ya ujenzi ambayo majibu yake yametoka almost 3 weeks ago na sasa nipo huku napiga kazi.

Kilichobaki ni mwanangu tu kumpata, sababu yule mwanamke nasikia yupo Uganda kwa sasa.
 
Title inasema mwanamke kakuharibia maisha…

Ila ndani ni kama kuna wizi ulishiriki huko ofisni kwenu wakawatimua. Haya maofisi hakuna dhambi mbaya kama ya wizi.

Nyakati ngumu mara zote ndio zinatudhihirishia ni watu gani tumewahold… hata we waweza kuwa mfano mbaya katika nyakati ngumu ya fulani. Kwa kifupi tu, tumuombe Mungu atuepushe na hizo nyakati ngumu.

Kwa huyo dada nae hakufanya vyema kukukimbia. Ona ushajipata now akisikia atabaki na muhaho.
 
Sasa oa mwanamke mwingine usiyejua nasaba yake akuharibie tena maisha. Hivi mnapataga wapi wanawake wajinga hivyo. Msitangulize hisia wakati wa kutafuta mke kama unavyotafuta hawara. Kupata mke ni mchakato unaoanzia kwenu kwanza upate baraka za wazazi, kisha ushirikiane nao pamoja viongozi wa dini yako kuchagua mwanamke anayeendana na wewe.
 
Title inasema mwanamke kakuharibia maisha…

Ila ndani ni kama kuna wizi ulishiriki huko ofisni kwenu wakawatimua. Haya maofisi hakuna dhambi mbaya kama ya wizi.
Nyakati ngumu mara zote ndio zinatudhihirishia ni watu gani tumewahold… hata we waweza kuwa mfano mbaya katka nyakati ngumu ya fulani.
Kwa kifupi tu, tumuombe Mungu atuepushe na hizo nyakati ngumu.

Kwa huyo dada nae hakufanya vyema kukukimbia. Ona ushajipata now akisikia atabaki na muhaho.
Hivi Depal kwanini mnakuwa hivyo

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu mu hali gani? Nashukuru mie mzima wa afya.

Kuna kisa nimekuwa nacho kwa muda mrefu, sikuwahi kushare humu. Niliandika kiufupi tu ila naona ni vizuri nikashare kwa ukubwa ili tupate kujifunza na wengine.
namke nasikia yupo Uganda kwa sasa
Wanawake wa sasa ukipigika ndipo utawajua vzuri.
Story yako inafànana fulani na ya kwangu ila yako ilikuwa ngumu zaidi.
Yule alinibadilikia kiasi ni kama vile sikuwahi kumfahamu kwa miaka yote 8. Nilikonda na kupoteza focus kwa miaka miwili.
Nashukuru kupitia kile niligraduate nikapata phd ya mahusiano na hatukuwa na watoto kila mtu akapita njia yake nikaanza jitafuta tena.
After miaka mitatu nimeanza kujipata anataka rudi maishani mwangu, nilimtimulia mbali.
 
Title inasema mwanamke kakuharibia maisha…

Ila ndani ni kama kuna wizi ulishiriki huko ofisni kwenu wakawatimua. Haya maofisi hakuna dhambi mbaya kama ya wizi.
Nyakati ngumu mara zote ndio zinatudhihirishia ni watu gani tumewahold… hata we waweza kuwa mfano mbaya katka nyakati ngumu ya fulani.
Kwa kifupi tu, tumuombe Mungu atuepushe na hizo nyakati ngumu.

Kwa huyo dada nae hakufanya vyema kukukimbia. Ona ushajipata now akisikia atabaki na muhaho.
Hapana mkuu. Sikushiriki wizi. Wale wenzangu walikuwa ni team yangu kwenye utendaji. Kuna mzigo waliupiga kwenye kitengo, wakanishirikisha kuwa upigwe bei tugawane, nikagoma. Kilichotokea wakaomba nisiwareport. Nikaushe tu sababu taarifa ingefika juu lazima mimi ndio ningekuwa nimewachoma sababu nipo kinyume na mpango wao.

Kilichotokea walipiga deal hilo, sasa kwenye tathmini ya ofisi ilipofanyika ulionekana umefanyika upigaji, na material zilizopigwa zilikuwa kutoka team yetu. Hawakuwa na mjadala, kwakuwa ni team basi tayari kila mmoja ni mhusika. Kiufupi niliwajibishwa na kosa la wengine
 
Back
Top Bottom