Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
Nitaomba radhi kwa kuanzisha thread mpya ili niweze kupata fursa ya kujibu hoja za ndugu yangu Mimi Mwanakijiji au kama anavyojiita sauti ya kijijini inayoelezea iliyoandikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu? K
Napende niwaeleze wale wote walioshabikia historia ya TANU kuwa wamelishwa "tango pori" na mheshimiwa sana Mwanakijiji japo sijaelewa amefanya kwa makusudi au kwa kutokufahamu kwakuwa tunae humu jamvini ni imani yangu atatueleza na kututanabaisha mapenzi yake juu ya vyama alivyovizungumzia, ila ningependa kumshauri awe mzalendo zaidi na apendelee kuwaelimisha watu kwa historia ya ukweli japo kwa kiwango cha asilimia 80 kama si mia kwa mia.
Pengine ni vyema tuangalie mtiririko wa kupigania uhuru wa nchi hii ili tuone mchango wa Mwanakijiji juu ya hoja yake na tupate kumuenzi kwa kutupa elimu na historia adhimu tusioijua:
1929: TAA yaundwa ikiwa na wajumbe wafuatao:
1. Kleist Sykes, 2. Mzee bin Sudi, 3. Ibrahim Hamis, 4. Zibe Kidasi, 5. Ali Said Mpima, 6. Suleiman Majisu, 7. Raikes Kusi, 8. Rawson Watts, 9. Cecil Matola.
1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kujenga mawasiliano na chama cha Kenya African Union (KAU).
1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la TAA; likiwa na wajumbe wafuatao:
1. Abdulwahid Sykes (Secretary)
2. Sheikh Hassan bin Amir
3. Hamza Kibwana Mwapachu.
4. Said Chaurembo
5. Dk. Kyaruzi.
6. John Rupia.
7. Stephen Mhando
1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika Arusha. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, Dossa Aziz na Stephen Mhando.
1952: Abdulwahid alichaguliwa kuwa Rais wa TAA.
1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika.
Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid.
Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano.
1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU.
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Mohammed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate na Mwinjuma Mwinyikambi. Wengine walikuwa Rajab Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidar Mwinyimvua na Idd Faiz Mafongo. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia na Mashado Ramadhani Plantan.
Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa.
1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, ,
Abubakar Ilanga na Saadan Abdu Kandoro. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia.
Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine.
Napenda kumfahamisha ndugu yangu Mwanakijiji kuwa pia ndani ya TAA na TANU kulikuwa na kina Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi, Dr Luciano Tsere, Dome Budohi, Zuberi Mtemvu, Ali Mwinyi Tambwe, Tatu bint Mzee, Mwinyijuma Mwinyikambi, Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo
Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi Titi Mohamed kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25.
Ndugu yangu Mwanakijiji,
Kwa watu makini makala yako ni moja ya utumiaji kalamu kupotosha jamii makala yako imebaka historia ya kweli ya TAA/TANU na sasa CCM kama nilivyoeleza mwanzo pengine mapenzi ya chama kimoja wapo ndio mapenzi hayo yamekusukuma kuinanga historia ya kweli.
Ni matumaini yangu ipo siku utaungana na Joseph Mihagwa utajitolea kuuvunjaa mwiko wa kuuzungumzia muungano
inavyostahili.
Shukrani sana na nakutakia siku njema wewe na jamaa wote wa JF.
Mohammed Shossi.
Kwa kuhitimisha napenda kujibu hoja ya Mwanakijiji pale alipo sema
Namsauri asome maandiko ya Ernesto Cheka ili aweze kuyajibu kwa hoja na kuweza kuwaondoa watu fikra kuwa CDM ni chama cha kikabila kwani watu Kama Cheka wanaweza kuwafanya watu waamini kutokana na mazingira yalivyo ndani ya chama. Hii itaijenga cdm na sio kuona kama ni uasi kuzungumzia yale yote yanayosemwa kwa ubaya kwa chama.
Na haitakuwa mbaya pia maswala kama haya hapa chini yakatolewa ufumbuzi.

Tatizo ni kuwa Shossi hataki kuvuka ambapo mantiki inamtaka avuke. Anauona ukweli lakini hataki kuuitikia japo unapiga kelele uitikwe. Chadema hakijawahi kuwa Chama cha Wachagga - iwe katika uanzilishi wake, uongozi wake, sera zake au hata katika kukubalika kwake. HILO SOTE TUNAJUA. Wanaosema ni cha Kichagga ni kwa sababu ya majina tu ya "Baadhi" ya viongozi wake. Hata tukikubali kwa ajili ya hoja kuwa uamuzi wa kiongozi mmoja ulifanywa kwa sababu ya kabila - kitu ambacho hakuna mtu amewahi kukithibitisha zaidi ya kutuambau "wanajua" haiwezekani hilo lifanye chama kizima kuwa cha kabila la watu hao wawili kwani ukikubali uwezekano huo inabidi ukubali pia kuwa kama kiongozi mmoja wa CCM ambaye ni Mndengereko akimuajiri mndengereko mwenzake basi CCM imekuwa ni ya Wandengereko! Ataliikataa hilo kwa CCM lakini atalikubali kwa Chadema.
Akiwa ni mtu anayependa ukweli ingempasa akubali na kukiri kuwa Chadema siyo chama cha kikabila kwa sababu hakuna ushahidi wowote wa ukabila ambao umewahi kuwekwa wazi au kuoneshwa kuwa unatengenezwa na Katiba, Sera au Viongozi. Kwa sababu kama upo aidha hao waliouona ni watu wazembe na waoga ambao walitakiwa kuripoti kwa Msajili ili uchunguze ufanyike kwani kunavunja Sheria ya Vyama vya Siasa. Kama kuna kiongozi yeyote wa Chadema ambaye amewahi kukataliwa kwa sababu ya kabila lake au dini yake alipaswa kusiimama na kwenda kutoa ushahidi au hata kufungua kesi kwani hili ni suala la haki yake kama raia. Zaidi ya kulalamika pembeni hakuna ushahidi wowote. NONE. Kama viongozi au watu hao wapo ambao wanajua kuwa kuna mambo Chadema inafanya kwa misingi ya ukabila au dini na watu hao wamenyamaza kimya basi ni watu waoga na wasiofaa kupewa hata uenyekiti wa nyumba zao.
So far Shossi amefanya kazi nzuri sana ya kutuonesha kuwa hakuna ukabila ndani ya Chadema na kuwa CCM siyo chama cha Waislamu. Hata hivyo nina uhakika atakubali hilo la pili na kukataa la kwanza.
Namsauri asome maandiko ya Ernesto Cheka ili aweze kuyajibu kwa hoja na kuweza kuwaondoa watu fikra kuwa CDM ni chama cha kikabila kwani watu Kama Cheka wanaweza kuwafanya watu waamini kutokana na mazingira yalivyo ndani ya chama. Hii itaijenga cdm na sio kuona kama ni uasi kuzungumzia yale yote yanayosemwa kwa ubaya kwa chama.
The Moment Of Truth:The Complete Text.(What Every Tanzanian Should Read)
by Ernesto Sheka
Ndoto na chuki zaja hadharani sasa;
Baada ya miaka takribani 26,Julai 1992 mfumo wa vyama vingi ukaanza.The same year Mtei akaanzisha Chadema na mpaka ninapoandika hili,in practical terms yeye ni mwenyekiti wa Chadema,kwake yeye ile ni fimbo maalumu ya kumchapa Mwalimu Nyerere siku akifanikiwa japo kila mara anakosea mahesabu huku jamii ikizidi kuamka na kujua historia ya taifa na kuchambua mambo hatua kwa hatua.Uzee wake umekuwa wa mashaka na wasiwasi.Ni dhahiri kuwa masterplan ya kuanza kwa Chadema ilianza kuandikwa Nairobi na baadaye Washington huku ikiuwaza ubepari na Ikulu kabla hata ya usajili.Lilian Mbowe ni mtoto wa kike wa Edwin Mtei ambaye aliolewa na Mbowe.Ni daktari ambaye kama nilivyosema awali anajishughulisha na kuendesha club ya usiku katikati ya jiji la Dar es salaam mtaa wa Mkwepu.Nyumba zao hutumika kukusanya vijana na wengi wana upofu na historia ya Chadema,wanaogundua huondoka mara moja.(Mtafuteni David Kafulila atawahadithia sehemu hii).
Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
Edwin Mtei namnukuu akisema,"we can't give this position to a man from nowhere" akimaanisha Zitto Kabwe,Zitto alitaka kuondoka ila alibaki kwa sababu zake.Tafakari hiyo kauli ya Mtei.Who's a man from nowhere and who's a man from somewhere??Ni ipi hasa masterplan ya mzee huyu aliyechekeana kinafiki na Nyerere?To revenge and take back his dignity and self interests.Ni ndoto yake ya ujanani na anaomba Watz tumsaidie aitimize.
Imefanikiwa kiasi gani?
Hali ni ngumu,ukabila bado umekuwa tatizo.Kifo cha Wangwe,maneno kuhusu viti maalumu,uwepo wa Deus Mallya aliyevuruga mpango wa kufunika sakata la kula pound za waingereza kama ruzuku kwa chama na baadaye kufoji risiti .(John Mnyika alikuwa kinara wa shughuli hii ya kuchakachua risiti).Wangwe's head had a price but Deus Mallya made a noise and Chadema let him went down and come up alone(sifa kubwa ya majasusi unapoharibu mpango wa kazi na ukapata tatizo).Ninapoandika hili,Deus Mallya ni mpiga picha na designer rasmi wa Chadema huku mifupa na damu ya Chacha Zakayo Wangwe ikilala udongoni kule Tarime.
Na haitakuwa mbaya pia maswala kama haya hapa chini yakatolewa ufumbuzi.
Vijana tunakiamini chama cha demokrasia na maendeleo,kwa namna kinavyosimama na kuibua na kuhoji mambo muhimu sana katika jamii yetu.
Hata wazazi wetu wanaamini chadema ndio kimbilio letu, licha ya wao kutuonya kuhusu kujitokeza mbele sana kwenye harakati za siasa, wakihofia usalama wetu.
Ila sasa viongozi wetu mnapoonekana kuvutana kwa ajiri ya tamaa za madaraka na ruzuku, ni aibu sana na ipo siku vijana wengi watafuatilia kiundani mambo ya chama chetu na ikiwa watabaini ukweli ulio tofauti na hisia zao, basi wataingia msituni kwani hawataamini mabadiliko kupitia chama cha siasa.
Ikiwa CHADEMA hakitabadilika kimtazamo, kisera na ki-organisation, hakuna mafanikio, nawaomba sana Mbowe, Slaa na Zitto kubalini kukaa na kushauriana.
I dnt understant wht the deal with uwenyekiti, tafadhali sana vijana vyuoni sasa wameanza kuhoji undani wa ugomvi wa Mbowe na Zitto kila wanapo onana.
Na ni kwa nini wanaonekana kutosikilizana hata kwa jambo la maana, tunajitahidi kujibu maswali magumu sana kutoka kwa vijana wasiojua CHADEMA, ila tunafanikiwa kuwatuliza na kuwapa moyo, ila wakati mwingine unajibu mtu na unaona haimwingii akilini.
Please msituumize kabisaaa.