Wazalendo Watatu Waliosajili TANU na Mmoja Aliyewaingiza Wanachama wa Kwanza TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
WAZALENDO WATATU WALIOKABIDHIWA USAJILI WA CHAMA CHA TANU NA MMOJA ALIYEWAINGIZA WANACHAMA WA KWANZA TANU

Nilialikwa Ikwiriri Rufiji kwenye Bibi Titi Festival.

Siku ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kufunga tamasha niliombwa nimzungumze Bibi Titi kwa dakika tano.

Nilifungua mazungumzo yangu kwa kueleza kuwa wanachama wa kwanza wa TANU walitoka Rufiji na nikaeleza kisa cha usajili wa TANU kazi ambayo walikabidhiwa wazalendo watatu: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Abdulwahid Kleist Sykes na Ally Kleist Sykes ndugu wawili.

Msajili Mzungu alikataa kusajili TANU kwa kisingizio kuwa Julius Nyerere aliyekwenda kufanya usajili hana orodha ya wanachama wala hana kadi za chama.

Nyerere akaenda nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist Sykes) ambako Abdul na Ally walikuwa wakimsubiri.

Alipotoa taarifa hii Abdul Sykes akaagiza atafutwe Mzee Said Chamwenyewe na alipofika Abdul Sykes alimkabidhi register book na kadi za TANU akamuomba aende Rufiji akaandikishe wanachama wa TANU.

Nakuwekeeani picha adimu za walazendo hawa niliowataja Ikwiriri na hapa katika makala haya:

Kulia waliokaa wa kwanza ni Said Chamwenyewe, Zuberi Mtemvu, Saleh Muhsin hawa walitoka TANU 1958 wakaunda chama cha Congress na mwaka wa 1964 walikivunja chama chao wakarejea TANU.

Aliyewapokea siku hii ya kurudi TANU alikuwa Bibi Titi Mohamed na picha iko hapo chini akimkaribisha Mtemvu.

Picha ya tatu: Kulia ni Lawi Nangwanda Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz Ukumbi wa Arnautoglo kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1956; Picha ya nne ni Ally Sykes na Julius Nyerere 1958.

1702011750640.png

1702011795188.png

1702011818245.png

1702011838887.png
 
Asante sana kwa hii.
P
 
Back
Top Bottom