Mwanakijiji na Uislamu wa TAA/TANU mpaka CCM

Hajasema waislamu watupu bana weee aah! Amewataja wakristo pia tena miongoni mwa hao uliowataja. Kweli hukuona au hukuelewa? ALichokieleza tena kwa kukirudia mara kwa mara kimantiki ni waislamu walikua na influence kubwa sana,tena walishika nafasi nyingi zile muhimu katika vyama hivyo na harakati zake; na nazungumzia nafasi muhimu! (usije tu mathalani ukamtaja mshindo, kwa vile alikua anashika bango la PPT-MAENDELEO basi awemo kwenye historia ya orodha ya waasisi wake).

Mantiki yake pia inaeleza bayana: kuwepo kwao hao waisalamu tena kwa influence kubwa,hakuvifanyi vyama hivyo kuwa vya kiislamu,la hasha! Hawakuvianzisha kwa sababu ya uislamu wao,wala kwa maslahi ya UISLAMU bali ukombozi wa TANGANYIKA,period!

Tukiachana na MKJJ, my take sasa: Hao waislamu waasisi wa TAA,TANU,ASP na CCM,ndio walikua waislamu wa kweli ambao tunapaswa kuwaenzi. Kama Abdulwahid Sykes anaweza kumpisha Julius aongoze harakati na asimwite kafiri,huyo ni mfano wa kuigwa na waislamu wengine. Lakini nina wasiwasi kama wewe ndugu unaweza kufanya hivyo kama ungekua na nafasi hiyo. Hebu nitoe wasiwasi tafadhali!
hapo kwenye red , watu kama hawa sijui kama tunao kwenye nchi yetu kwa sasa hivi, na kama wapo ni mmoja kati ya mia moja.
 
Hajasema waislamu watupu bana weee aah! Amewataja wakristo pia tena miongoni mwa hao uliowataja. Kweli hukuona au hukuelewa? ALichokieleza tena kwa kukirudia mara kwa mara kimantiki ni waislamu walikua na influence kubwa sana,tena walishika nafasi nyingi zile muhimu katika vyama hivyo na harakati zake; na nazungumzia nafasi muhimu! (usije tu mathalani ukamtaja mshindo, kwa vile alikua anashika bango la PPT-MAENDELEO basi awemo kwenye historia ya orodha ya waasisi wake).

Mantiki yake pia inaeleza bayana: kuwepo kwao hao waisalamu tena kwa influence kubwa,hakuvifanyi vyama hivyo kuwa vya kiislamu,la hasha! Hawakuvianzisha kwa sababu ya uislamu wao,wala kwa maslahi ya UISLAMU bali ukombozi wa TANGANYIKA,period!

Tukiachana na MKJJ, my take sasa: Hao waislamu waasisi wa TAA,TANU,ASP na CCM,ndio walikua waislamu wa kweli ambao tunapaswa kuwaenzi. Kama Abdulwahid Sykes anaweza kumpisha Julius aongoze harakati na asimwite kafiri,huyo ni mfano wa kuigwa na waislamu wengine. Lakini nina wasiwasi kama wewe ndugu unaweza kufanya hivyo kama ungekua na nafasi hiyo. Hebu nitoe wasiwasi tafadhali!

Amewataja lakini kwa uchache na mwisho akawatoa kwenye hesabu hebu msome hapa.........
M. M. Mwanakijiji​

Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga.

Utaona kwa makusudi ameamua kuwataja wachache ili aweze ku align na CDM hapo ndipo mwerevu anagundua kwa haraka sana mantiki ya makala yake! na nimeshasema Mwanakijiji ni kama alietengeneza igizo kwahiyo kwenye hilo igizo alitaka kumpamba stering na amlinde asife! Ndio maana akawatoa wakristo wazalendo wapigania uhuru.
 
Nitarudia mara mia lakini sitafahamu kwanini amewatoa wapigania uhuru wakristo kwenye historia!

What Mwanakijiiji is doing is basically a continuation of un-finished business, he wont win it and you all know that Isalm is strong faith, it has very strong foundation and it can not easily be shaken.
 
Acha kuendekeza udini wewe.
Hizo ulizoweka rangi ya kibuluu ziko ngapi na hizo zenye rangi nyeusi ziko ngapi.
Tupatie idadi kamili ya kila upande.
Kwani hata hiyo cdm mnayodai (na wewe ukiwamo) kuwa ni ya wakristu ni kwa sababu zipi...pengine ni kuwa idadi ya wakristu ni kubwa kuliko ile ya waislam; inawezekana ni kweli. Lakini swali la kujiuliza hapa ni "Je hakuna waislamu ndani ya chadema?" Jibu ni kuwa wapo, tena wengi kwa idadi na ni waislamu safi kabisa wanaofuata maadili ya dini yao (sina haja ya kuwataja kwa majina kwani hata wewe unawafahamu).
Iweje ninyi muendelee kueneza propaganda kuwa chadema ni chama cha wakristu.

Wewe ni mpotoshaji:
Mbali ya comment zako nyingi za upotoshaji, ulishawahi kuja na comment zako hapa kuwa Osama hajauwawa,. Anyway yalikuwa maoni yako na hapakuwa na haja ya kukulazimisha kile ambacho dunia nzima imekiamini kutokana na kuwepo ushahidi lukuki. Tayari Al-Qaeda wameshakiri kuwa "boss wao" kauawa na NAVY SEALS TEAM SIX, na kwa kukuthibitishia hilo tayari wameshaeleza nia yao ya kulipa kisasi kutokana na kuuwawa kwa "boss wao huyo". Huoni hii kwako ni AIBU KUBWA?
 
Penye red, kwanza mimi sikujua kama Mohammed Shossi ni Muislam, pili nazidi kuamini kwamba Waislam wanatumia mda mwingi kupigania uislam

Ndugu yangu ndio unaamka nini? Ulishasikia sera zao fuatilia kwa karibu kama hujakimbia upoteze na mguu wako, hawaeleweki wanachokipigania ni dini au ni siasa au ni maisha magumu. Wanagazeti lao linaitwa mzalendo net, hapo nyuma lilinitia kichefuchefu sana. Lakini ninashukuru mungu wanaohangaika na huu usumbufu wa kutusumbua hapa TZ ni wachache wengine maisha yanawachapa kama sisi.:mod:

MUNGU IBARIKI TANZANIA SOPRA TUTTO Dr wangu SLAA.:A S-rose:AMEN.
 
Ndugu,ndio maana nakusihi usome tena ile makala. Aliweka wazi kabisa kuwa hakuwataja baadhi ya wakristo kwa makusudi kabisa ili "hoja inoge"...nimemnukuu hapo. Vivyo hivyo hakuwataja baadhi ya wanachadema waasisi waislamu na wale wasio wachaga kama Bob Makani. Mie nilimwelewa kwamba lengo lake lilikua kwa wasomaji werevu kama mimi na wewe tuweze kuwapambanua na kuwabeza wale wanaotaka kutukoroga na udini na ukabila kwa logic rahisi sana:
Wanaotutajia ukristo na uchaga wa CDM(ambao hawatutakii mema kama taifa) kwa sababu tu waasisi wake ni wachaga na ni wakristo - na si sababu nyingine- ; kwanini wasituambie kwamba CCM iliyotokana na TANU na ASP ni ya kiislamu kwa sababu hiyohiyo?
Unaweza kuniambia kwanini hakutaja majina ya wakristo wote kwenye makala yake? in fact mie wengine nimewaacha kama oscar kambona! amewaacha kwa makusudi amewaacha kwa kuwa anataka picha la filamu aliyoitengeneza iishe anavyotaka yaani steringi sijui kama ni CDM au CCM asife!
 
Hapo kwenye red mkuu sikubaliani na wewe mwenye kujua na aliesoma kama wewe hawezi kusema eti TAA/TANU mpaka CCM ni chama cha waislamu ikiwa kulikuwa na wakristo kindakindaki kama madaktari watano – Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere, patrick kunambi, gerimano pacha, japhet kirilo na l.m. Makaranga.bila kuwashau joseph kimalando na john rupia.

Kwahiyo kimantiki Mwanakijiji analo alilokusudia na si jingine ila kuipembejea CDM na kuutukanisha Uislam! Kama alikuwa na haja na hoja ya kuisafisha TAA/TANU na CCM na waenyeji wa Dar es Salaam ambao ni Wazaramo ila aliona kuwa kina Sykes hawakuwa Wazaramo ametumia ufundi kuisuka hoja yake ili afanikishe malengo yake! Narudia hakututendea haki Waislam mimi nikiwa mmoja wao kwa kuufananisha Uislam na Uchagga ambao ndani ya huo Uchagga kuna waislam pia!

Shukran sana kwakuwa wewe mwenzetu umeenda sana shule na uimekusaidia sana nadhani utakuwa unaelewa mantiki ya mada yangu.

Mohammed Shoshi: Kwanza nikushukuru sana kwa majibu yako yanayojaribu kumwelimisha mtu. naomba nieleweke vyema hapa ndugu yangu Mohammed, nachojaribu kueleza ni kwamba kwa mtanzania wa kawaida kabisa huenda hata mimi nakwenda mbali kidogo kama Nyerere alivyosema, tunapoanza kuhoji, huyu ni mchaga, huyu ni mmakonde, itakwenda mbali zaidi. Kwa picha ya mazingira ya hoja aliyoibua kiongozi wa CCM kudai CDM ni ya Wachaga, next time itakuwa ya wakristo (hayo tumeyasikia kwa masikio yetu toka kwa viongozi wa dini zetu wenyewe, kupitia vyombo vya habari na wakati mwingine kwenye mahubiri, refernce tunazo). Nilivyomuelwa mimi na hata baadhi ya watu wemgine walioijadiri hoja si kwa mtazamo hasi, watakuwa wamepata ujumbe ule ule......MMK amebeba mawazo ya watanzania wengi tu nikiwemo mimi personally, kama kiongozi anaweza kusema leo hii chama fulani ni cha watu wa kabila fulani, kesho itakuwa wa imani fulani, the same itakuwa kwa upande pinzani......tusiyaangalie mambo haya kwa itikadi za kichama, au imani zetu, tuangalie hoja iliyojegwa msingi wake ni nini...hayo ndiyo mawazo yangu
MASAHIHISHO: Samahani sana kwa kuni-quote vibaya ndugu yangu Mohammed na nina shukuru sana kwa uungwana wako pia katika kujibu hili, lakini niliposema kuna watu shule huenda haikuwasaidia sana kuna watu niliolenga kulingana na posts zao. Wamekuwa hawajengi hoja badala yake ni matusi, kuropoka na kukurupuka tu, sasa hii haimsaidii sana achilia mbali sisi wanajukwaa mwezao. Tunahitaji watu wanaoweza kujenga hoja zenye mantiki na zenye kuleta tija. Nijuavyo mimi si lazima kila post mtu uchangie, kuisoma tu inatosha kujifunza kitu au kuelewa na hata kama haikufai basi ni vyema kuipuuza.
Asante sana Ndugu yangu Mohammed.
 
1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la TAA; likiwa na wajumbe wafuatao:

1. Abdulwahid Sykes (Secretary)
2. Sheikh Hassan bin Amir
3. Hamza Kibwana Mwapachu.
4. Said Chaurembo
5. Dk. Kyaruzi.
6. John Rupia.
7. Stephen Mhando

Wangapi wanajua historia ya madaktari watano – Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere na mchango wao katika kusukuma mbele harakati za TAA kati ya 1948 – 1950?

Shukrani sana na nakutakia siku njema wewe na jamaa wote wa JF.

Mohammed Shossi.

Kwa kuanza tuu naomba ninukuu kipande kwenye hoja ya Mwanakijiji "Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga."

Kwa hiyo kwa kipande hiko tuu nataka napenda kuthibitisha kuwa ww ume-duplicate bila kuelewa... Pia natoa heko kwa JF mod walichofanya.. Kimsingi ungekuwa Tarime ungepopolewa si kwa chuki bali kwa utovu wa kuelewa... Nadhani utagundua maana ya neno "falacy". Mwanakijiji anajaribu kuthibitisha kuwa wanaosema ya CHADEMA kisiwaume ikisemwa CCM basi.. Hakuna udini wala ukabila
 
Hajasema waislamu watupu bana weee aah! Amewataja wakristo pia tena miongoni mwa hao uliowataja. Kweli hukuona au hukuelewa? ALichokieleza tena kwa kukirudia mara kwa mara kimantiki ni waislamu walikua na influence kubwa sana,tena walishika nafasi nyingi zile muhimu katika vyama hivyo na harakati zake; na nazungumzia nafasi muhimu! (usije tu mathalani ukamtaja mshindo, kwa vile alikua anashika bango la PPT-MAENDELEO basi awemo kwenye historia ya orodha ya waasisi wake).

Mantiki yake pia inaeleza bayana: kuwepo kwao hao waisalamu tena kwa influence kubwa,hakuvifanyi vyama hivyo kuwa vya kiislamu,la hasha! Hawakuvianzisha kwa sababu ya uislamu wao,wala kwa maslahi ya UISLAMU bali ukombozi wa TANGANYIKA,period!

Tukiachana na MKJJ, my take sasa: Hao waislamu waasisi wa TAA,TANU,ASP na CCM,ndio walikua waislamu wa kweli ambao tunapaswa kuwaenzi. Kama Abdulwahid Sykes anaweza kumpisha Julius aongoze harakati na asimwite kafiri,huyo ni mfano wa kuigwa na waislamu wengine. Lakini nina wasiwasi kama wewe ndugu unaweza kufanya hivyo kama ungekua na nafasi hiyo. Hebu nitoe wasiwasi tafadhali!

Hapo kwenye red inafaa iingwe na CDM na wanacdm kwa kuacha kumsakama Zitto kwa kuwa anautaka uenyekiti ila swali je Mbowe anaweza kuwa kama Abdulwahid Sykes kumpisha Zitto kama Sykes alivyompisha Nyerere nadhani jibu mnalo na mtakumbuka yaliyotokea kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa CDM alipokuwa aking'atuka Bob Makani.
 
Nitarudia mara mia lakini sitafahamu kwanini amewatoa wapigania uhuru wakristo kwenye historia!

niliposoma lile bandiko nilijua tu lazima kuna watu amabao watalikurupukia lile bandiko kama wewe unavyofanya sasa hivi, kwanza nijibu hili swali.
kwa nini mwanakijiji aliihusisha ccm na uislam kwenye lile bandiko lake?niambie chanzo cha yeye kufanya vile na kama hujui basi hii mada ya mwanakijiji umekurupuka kuijibu.
unayayaongea yote ni kweli kabisa sikatai , na hata mwanakijiji hawezi kukubishia lakini tafuta chanzo kwanza kwamba kwa nini mwanakiji alitumia ihii style ya uandishi?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Humu ndani ya Jf, kuna wanachama ambao ni viongozi wa Chadema, na hizi tuhuma za kukisema chadema kuwa ni chama cha wakristo na wachaga wanaziona.

Sijui wao kama viongozi wanalichukuliaje ili suwala, naona wapo kimya sana. Je hawaoni kuwa ni hatari kwa chama chao. Hao wasio wakristo wanayasoma haya, na wakitoka nje ya hapa wanawaeleza ndugu, jamaa na marafiki zao kile kinacho endelea humu.

Je hii si hatari kwa mustakabari mzima wa chama chao?
 
Hapo kwenye red inafaa iingwe na CDM na wanacdm kwa kuacha kumsakama Zitto kwa kuwa anautaka uenyekiti ila swali je Mbowe anaweza kuwa kama Abdulwahid Sykes kumpisha Zitto kama Sykes alivyompisha Nyerere nadhani jibu mnalo na mtakumbuka yaliyotokea kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa CDM alipokuwa aking'atuka Bob Makani.

Nyerere alikuwa genious na alikuwa na ushawishi mkubwa kuliko huyo Sykes. Zitto hawezi kumwingia Mbowe hata nusu asilimia.
Yote kwa yote, mazingira wakati wa kupigania uhuru ni tofauti kabisa na mazingira tuliyonayo leo. Sumbua kichwa hicho, acha siasa za masjid.
 
Humu ndani ya Jf, kuna wanachama ambao ni viongozi wa Chadema, na hizi tuhuma za kukisema chadema kuwa ni chama cha wakristo na wachaga wanaziona.

Sijui wao kama viongozi wanalichukuliaje ili suwala, naona wapo kimya sana. Je hawaoni kuwa ni hatari kwa chama chao. Hao wasio wakristo wanayasoma haya, na wakitoka nje ya hapa wanawaeleza ndugu, jamaa na marafiki zao kile kinacho endelea humu.

Je hii si hatari kwa mustakabari mzima wa chama chao?

Vipi CCM na Uislam hulioni hilo ama wao viongozi wa Magamba hawalioni hili? Changanya na zakwako bro!
 
Kwa kuanza tuu naomba ninukuu kipande kwenye hoja ya Mwanakijiji "Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga."

Kwa hiyo kwa kipande hiko tuu nataka napenda kuthibitisha kuwa ww ume-duplicate bila kuelewa... Pia natoa heko kwa JF mod walichofanya.. Kimsingi ungekuwa Tarime ungepopolewa si kwa chuki bali kwa utovu wa kuelewa... Nadhani utagundua maana ya neno "falacy". Mwanakijiji anajaribu kuthibitisha kuwa wanaosema ya CHADEMA kisiwaume ikisemwa CCM basi.. Hakuna udini wala ukabila

Kwanini awatoe hao kwenye nyekundu tu na asiwataje wengine waliobakia ilhali tunawajua wa majina na idadi yao? hebu jiulize halafu utajua alichokikusudia ili makala yake inoge!
 
Amewataja lakini kwa uchache na mwisho akawatoa kwenye hesabu hebu msome hapa.........

Utaona kwa makusudi ameamua kuwataja wachache ili aweze ku align na CDM hapo ndipo mwerevu anagundua kwa haraka sana mantiki ya makala yake! na nimeshasema Mwanakijiji ni kama alietengeneza igizo kwahiyo kwenye hilo igizo alitaka kumpamba stering na amlinde asife! Ndio maana akawatoa wakristo wazalendo wapigania uhuru.

Shossi mbona unaleta ubishi katika hoja iliyonyooka??
Umeshauriwa kurudia kumsoma mwanakiji lakini hutaki kwa kuwa hutaki tu kwa makusudi umeamua kubadilisha hoja ya mwanakiji kutoka kwenye jukwaa la kisiasa unasema unatetea uislamu kwakuwa mwanakijiji kawakosea sana waislamu kwa kuulinganisha na uchaga!!

Sasa nakuomba usome kipande hiki kidogo tu na wewe mwenyewe umeki-quote lakini sijui hukielewi ama unafanya kusudi, hapa ninanukuu;

"Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga."

Kama ukujiruhusu akili yako kufanya tafakuri kwa uhuru kabisa na kwa kuwa naamini una elimu ya kutosha, sidhani kama una hoja ya kumshutumu mwanakiji, badala yake ulitakiwa kumpongeza na kuanza kumhoji nape na ccm kwa kujaribu kupandikiza uchochezi na ubaguzi miongoni mwa watanzania. Kama huwezi kuona kwamba chadema inaungwa mkono na watanzania wa makabila mbalimbali; kuanzia Kilimanjaro hadi Ruvuma, kuanzia Dsm hadi Kigoma, kuanzia Mara hadi Mbeya, basi utabaki kujifungia kwenye kioski cha udini na kujitolea kuwa mtetezi wa uislamu kila jina hilo linapotajwa.

Kama huwezi kuelewa kwamba mwanakijiji amelinganisha dhana ya ukabila inayotajwa na ccm dhidi ya chadema, kitu ambacho sio kweli na akafanya ulinganifu huo huo kwa ccm kuwa ya waislamu tena akiweka alama ya kuuliza, basi una tatizo kubwa sana la uelewa. Nadhani ni vizuri kujadili hoja kwa hoja badala ya jazba na hamaki.
 
hivi wakati waislam wanwapinga wazungu hadi leo tunayaona haya. lkn wakiristo ni ndugu zao wazungu hadi leo tunaona. inakuwaje wakiristo wapambane na ndugu zao wazungu?

Tatizo lenu mna roho mbaya, kwahiyo unataka tuendeleze chuki za enzi za ukoloni?, hivi unajua waarabu walichowafanya babu zetu enzi za utumwa je unataka tuwachukie waarabu kwa hilo mpaka leo? Hasa ukichukulia waarabu wengi ni "Waislam safi"
 
Ok mkuu, labda kwa maswali tutaelewana:

  1. Kati ya wakristo na waislamu,ni wepi hasa walikua vinara waanzilishi wa TAA hadi TANU hadi CCM? Kama ni waislamu,basi umwelewe sasa MKJJ. Kama ni idadi sawa,basi nithibitishie. Na Kama ni wakristo,je nikisema kuwa ndio maana "waliwaweka pembeni waislamu baada ya uhuru" kama wanazuoni wengi wa kiislamu wanavyosema,nitakua nasema urongo?
  2. Kama MKJJ akiwarudisha wakristo "wazalendo" wote kwenye orodha yake,halafu akawarudisha na waasisi wote wa CDM wasio wakristo na wasio wachaga,je utaamini kwamba CDM si cha kikristo na si cha kichaga kama ilivyo CCM?
Pamoja mkuu!

Back
Top Bottom