Wenyeviti wa TANU Mwanza na Kijijini Nyamazugo Geita

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
WENYEVITI CHAMA CHA TANU MWANZA NA KIJIJINI NYAMAZUGO GEITA NA HISTORIA YA KADI YA TANU

Chairman wa TANU wa kwanza Mwanza nakumbuka jina lake Hussein Jumbe.

Kijijini Nyamazugo Geita kadi za TANU zilikuwa zikipatikana kwa Mzee wa Kimanyema jina lake Saadallah.

Hii ilikuwa katika miaka ya 1956-1960.

Taarifa kutoka kwa Mohamed Sleyim.

Nimemuomba tupate historia za wazalendo hawa na picha zao ikiwezekana:

"Mohamed Said sidhani ila nitajitahidi kuwatafuta waliokuwa majirani wa marehemu Mzee Saadallah."

Tuwe na subra.

Naweka hapo chini historia ya Kadi ya TANU:

HISTORIA YA KADI YA TANU 1954

Ndugu yangu mmoja kanirushia kadi ya TANU nami kwa kuonyesha shukurani yangu kwake namuwekea hapo chini historia ya kadi ya TANU kama nilivyoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes:

''Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake.

Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika.

Mfano wa kadi ya TANU ulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion.

Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.

Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA) alichapisha kadi nyingine 2000.

Ally Sykes alikuwa Secretary wa TAGSA.

Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa.

Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo.

Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na John Rupia kadi nambari 7.

Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Faizi Mafungo kadi nambari 24; Iddi Tosiri kadi nambari 25.''

Picha ya Ally Sykes na Julius Nyerere miaka ya mwanzo ya kuunda TANU.

1694535240848.png

1694535300261.png
 
Historia nzuri
Lakini haijalisaidia Taifa hili.
Taifa limekuwa la wapigaji uzalendo hakuna.
Wazalendo hao wakifufuka leo hawatoamini kama kweli watoto wameharibu urithi kiasi hichi.


Kila mtu anataka kujaza kibunda
Viongozi wapo kimasilahi zaidi
Wanainchi wengi( watawaliwa) wanaishi maisha ya dhikiiiii na mateso

Nisawa na mzazi anapambania familia yake kuacha urithi ili watoto waishi vizuri.

Matokeo yake Baba kufariki watoto wanagombania mali wanazigawana, wanauza ovyo. Ndivyo Taifa letu lilivyo.

Bora ukose nguo utapata mtu wakukuonea huruma atakupatia uvae kuliko kukosa akiri.
Viongozi wa Taifa hili hawana akiri kabisa( ni tusi kwa mtazamo wako).

Madini, gase, rasilimali watu, aridhi, vyanzo vya maji, misitu, wanyama poli...

NANI ANAJALI KWENYE TAIFA HILI?
 
Historia nzuri
Lakini haijalisaidia Taifa hili.
Taifa limekuwa la wapigaji uzalendo hakuna.
Wazalendo hao wakifufuka leo hawatoamini kama kweli watoto wameharibu urithi kiasi hichi.


Kila mtu anataka kujaza kibunda
Viongozi wapo kimasilahi zaidi
Wanainchi wengi( watawaliwa) wanaishi maisha ya dhikiiiii na mateso

Nisawa na mzazi anapambania familia yake kuacha urithi ili watoto waishi vizuri.

Matokeo yake Baba kufariki watoto wanagombania mali wanazigawana, wanauza ovyo. Ndivyo Taifa letu lilivyo.

Bora ukose nguo utapata mtu wakukuonea huruma atakupatia uvae kuliko kukosa akiri.
Viongozi wa Taifa hili hawana akiri kabisa( ni tusi kwa mtazamo wako).

Madini, gase, rasilimali watu, aridhi, vyanzo vya maji, misitu, wanyama poli...

NANI ANAJALI KWENYE TAIFA HILI?
Von...
Sisi ambao wazee wetu ndiyo walioasisi harakati za kudai uhuru tumeshukuru kwa kuweza kuirejesha historia hii ikawa leo tunaisoma hapa.

Hayo ya rasilimali ni mengine.
 
Mnasoma halafu?
Mbuli...
Halafu yake ndiyo sasa.
Wewe umeijua.

Hivi punde nimemuandikia mtu maneno hayo hapo chini:

"Kitabu cha Abdul Sykes kiliwashtua watu wengi kupita kiasi.

Kwanza kubwa ni kuhusu chanzo cha harakati za Waafrika kujikusanya kuunda umoja wao.

Kitabu kinamnukuu Kleist Sykes akieleza kuwa fikra ile aliipata kutoka kwa Dr. Kwegyir Aggrey walipokutana Dar es Salaam mwaka wa 1924.

Kleist akawataja waasisi wote kwa majina yao.

Hakuna mwandishi yeyote kabla yangu aliyeanza kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa namna nilivyoandika mimi.

Kubwa hayo niliyoandika si yangu yalikuwa yanatoka kwa wenyewe Sykes waliounda vyama hivyo.

Suala lililowatatiza wasomaji ni Julius Nyerere anaingiaje katika historia ya TANU?

Kwa miaka yote ikiaminika kuwa chama cha TANU kiliundwa na Nyerere kutoka TAA mwaka wa 1954.

Bahati mbaya sana Nyerere hakueleza vipi aliingia katika uongozi wa TAA Dar-es-Salaam mwaka wa 1953.

Kleist kaeleza kwa nini waasisi wa African Association 1929 wengi walikuwa Waislam.

Akaendelea kueleza kwa nini licha ya kuwa na African Association waliona waunde Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933.

Wanapofika kwenye historia ya TAA hapo ndipo wasomaji wanakutana na watoto wa Kleist: Abdulwahid, Ally na Abbas katika uongozi wa chama.

Nyerere haonekani.

Jambo hili liliwakasirisha wengi lakini liliwafurahisha wengi pia.

Kama wasemavyo Waingereza: "The rest is history."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom