Historia ya Kadi ya TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
HISTORIA YA KADI YA TANU 1954
Ally Sykes ndiye aliyechora na kusanifu kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Alifanya kazi hii kwa kuangalia na kunakili kadi yake ya Tanganyika Legion.

Ally Sykes akachagua rangi, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika.

Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie.

Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) ambako alikuwa Katibu alichapisha kadi nyingine 2000.

Kadi nambari 1 Ally Sykes alimwandikia Rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake.

Ilipendekezwa kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama.

Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo.

Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid, akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Denis Phombeah (Kutoka Nyasaland) kadi nambari 5; Dome Okochi (Kutoka Kenya) alipata kadi nambari 6 na John Rupia kadi nambari 7.

Picha: Picha ya tatu ni ya Kadi ya Lawi Nanngwanda Sijaona iliyotolewa Newala mwaka wa 1955.

1702006746398.png

1702006793000.png

1702006816392.png

1702006853573.png
 
Duh kwa hiyo nyerere kadi yake ya TANU siyo namba moja

Ova
 
Back
Top Bottom