Mwanakijiji, huu ni UDINI pia...

Mwanakijiji, huu ni UDINI pia...

Status
Not open for further replies.

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,616
Kwanza kabisa nalaani kwa nguvu yote mauaji ya Padri huko Zanzibar ningependa kuona hatua kali zinachukuliwa kwa wahusika bila huruma yeyote wala mizengwe ya aina yeyote......

Sasa turejee kwenye mada....

Ni kawaida watu wenye UDINI kuwa watu wa kwanza kulalamikia UDINI wa wengine na wao wenyewe kuwa 'vipofu' kabisa na udini wao
hata kama Udini wao upo waziwzi.....

Sasa nafahamu heshima aliyonayo Mzee Mwanakijiji kwa wana JF na wengine kiasi kwamba hata anapokosea huoni watu wakimkosoa kabisa......

Hii thread ya Mwanakijiji akimtaka Kardinali Pengo ajiuzulu au achukue hatua ni thread iliyojaa hisia za UDINI na thread HATARI mno kwa Taifa Na Kwa mtu kama Mwanakijiji kuja na thread hii hapa ni jambo la kushangaza mno.....

Ukiwa MTAIFA basi kila tatizi la nchi unaloliona uta demand action kutoka kwa viongozi wa kitaifa kamwe huwezi demand action kutoka kwa viongozi wa DINI hasa DINI yako......

Kuuwawa kwa Padri Zanzibar hakuhitaji action za Pengo ,Kunahitaji actions za Viongozi wenye UTAIFA Na wanaojali UTAIFA kwanza,Pengo hata awe na busara za aina gani ni kiongozi wa DINI ,na UHALALI wa Pengo unaishia kwa wafuasi wa dini yake tu......hata kama viongozi wa KITAIFA hawafanyi wanayotakiwa kufanya, bado Pengo Hawezi ku Play role ya Kiongozi wa Taifa hasa kwenye vurugu za kidini kama hizi...

Pengo yuko sahihi kuwa kimya na kusubiri,kuliko kukimbilia kutoa kauli zinazo weza leta MAAFA ZAIDI, hasa kama mpaka sasa hatuna uhakika waliomuua huyo Padri wana malengo gani haswaa?

What if malengo yao ilikuwa ni kuwa Provoke WAKATOLIKI ili walipize visasi na nchi ivurugike?

Huwezi kusikia Jenerali Ulimwengu akimuomba Pengo aingilie kati,unajua why? sababu anajua ni makosa kwa watu kukimbilia kwa viongozi wao wa dini kuomba muongozo kwa matatizo ya 'uzembe wa kisiasa na wanasiasa'.....

uhalifu na vurugu zinazojitokeza ni zao la serikali dhaifu,sasa kila mtu akianza kuomba muongozo wa Viongozi wa DINI yake,unafikiri hii nchi itakalika?

Ukosefu wa busara kwa viongozi wa serikali hauwezi kuzibwa na busara za viongozi wa dini, viongozi wa dini watabaki kuwa viongozi wa dini,wakitetea maslahi ya dini zao na wafuasi wao... leo kwa WAKATOLIKI utasema Pengo achukue hatua,kesho akiuwawa msabato?
akiuwawa Imam wa Shia je?je kukitokea mauaji ya Mashia,wakuawa huko Zanzibar labda na waislam wa Sunni? Pengo atakuwa relevant?...

BADO KAMA TAIFA TUNAWEZA KUTAFUTA 'BUSARA YA KUTUPATANISHA' NA KUWASHUGULIKIA 'WAHUNI' WOOTE BILA KILA MTU KUKIMBILIA KWA KIONGOZI WAKE WA DINI, KUKIMBILIA KWA VIONGOZI WA DINI KUOMBA MUONGOZO KWA MATATIZO YA KITAIFA NDIO UDINI WENYEWE.

Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.

Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..

Pengo... utafanya nini....
 
Yes Boss... Lakini after everything hudhani kwamba its time (inaweza isiwe pengo) jamii ya wakristo wakasema jambo?
 
Yes Boss... Lakini after everything hudhani kwamba its time (inaweza isiwe pengo) jamii ya wakristo wakasema jambo?

Chochote wakachosema
bado jukumu la kukamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani lipo kwa serikali....

Pengo sio Nyerere,yes ni sad Padri kauwawa but si kwamba waluiomuua huyo Padri wana
baraka za waislam wote wa TZ....sioni umuhimu wa Kauli za viongozi wa dini kwenye 'POLICE CASE'
 
The Boss usemayo ni kweli lakini angalia upande wa pili wao huwa wanakimbilia wapi.............angalia roles za viongozi wa Kikristo na zile za viongozi wa waislamu, utagundua kwanini Mwanakijiji kasema vile
 
Jenerali Ulimwengu hawezi mwambia Pengo KWA KUWA SI wa dini yake!
 
Ni mtihani mkubwa sana haya mambo yanatokea... Ni mtihani kwa Waislamu na Wakristo pia. I can understand Mwanakijiji ingawa sikubaliani naye; najaribu kufikiria katika nafasi yake ningekuwa na msimamo na mawazo gani... Najikuta siwezi pata jibu sababu circumstances zake na zangu ni tofauti... Na hali pia circumstances za tukio na matukio ni lazima yapeleke wengi huko na kuwafanya wawe wenye hasira, hasa kwa Imani ya Wakristo.

Boss I support you na uliyosema... I can understand the frustration for I am so frustrated right now na sielewi ni nani nimwelekezee. Sad.
 
The Boss usemayo ni kweli lakini angalia upande wa pili wao huwa wanakimbilia wapi.............angalia roles za viongozi wa Kikristo na zile za viongozi wa waislamu, utagundua kwanini Mwanakijiji kasema vile

TWO wrongs do not make it right...

wakuwa held responsible ni serikali.....na sio kila mtu akimbilie kwa viongozi wa dini yake
unapinga nini,na unafanya nini?
 
Chochote wakachosema
bado jukumu la kukamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani lipo kwa serikali....

Pengo sio Nyerere,yes ni sad Padri kauwawa but si kwamba waluiomuua huyo Padri wana
baraka za waislam wote wa TZ....sioni umuhimu wa Kauli za viongozi wa dini kwenye 'POLICE CASE'

The Boss...huoni kwamba viongozi wa ukristo wanatakiwa kusema japo tujihadhari kutokana na trend yaa mauaji yanayoendelea? Wanaweza wasiwe police wa kukamata wahallifu lakini wanaweza japo kutuambie sie wafuasi wao tuwe na tahadhali?
 
Aina hii ya mtizamo ndio imetumika kuwa "tame" christians hapa nchini...unfortunately this loophole imeendelea kutumiwa na the other side ku-provoke christians, na baada ya hapo this kind of argument hutolewa, so hii huendelea katika mzunguko usiokwisha. Pengo anahitajika sasa kutoa bold statement ambayo itaelezea hisia za christians hapa nchini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wao ni binaadamu
wanaweza kuwa 'carried out' na emotions na hasira na uchungu
mwisho wakasema 'kuweni na tahadhari na waislam wote'
we unaonaje hapo?
fair?
 
MODs hebu unganisheni uzi huu na ule wa MMM, mbona duplications!!

THE BOSS: si uchangie palepale, kwani lazima uanzishe uzi mwingine?? Kwanini usimjibu kulekule!!???
 
Chochote wakachosema
bado jukumu la kukamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani lipo kwa serikali....

Pengo sio Nyerere,yes ni sad Padri kauwawa but si kwamba waluiomuua huyo Padri wana
baraka za waislam wote wa TZ....sioni umuhimu wa Kauli za viongozi wa dini kwenye 'POLICE CASE'

Mkuu The boss viongozi wanasema tutawachukulia hatua, kwenye thread yangu nmesema watawala wawajibike, tuna hitaji kupewa taarifa ya kinachoendelea na kama taifa tunahitaji kuona mtu anawajibishwa kwa uzembe huu
 
Aina hii ya mtizamo ndio imetumika kuwa "tame" christians hapa nchini...unfortunately this loophole imeendelea kutumiwa na the other side ku-provoke christians, na baada ya hapo this kind of argument hutolewa, so hii huendelea katika mzunguko usiokwisha. Pengo anahitajika sasa kutoa bold statement ambayo itaelezea hisia za christians hapa nchini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Wewe unaita 'ku tame' christians
wakati hata waislam wanapopigana,mfano kesi za viwanja za BAKWATA'
wenye busara husema haya haya....
watu wajiepushe na kukimbilia viongozi wao wa dini na kuwachukulia wote wasio wa dini zao ni maadui...
police case ibaki police case,wote tushirikiane 'wahalifu' washughulikiwe'
 
Police case ni ngonjera za kupumbaza jamii.
Ina maana huoni yote yafanywayo na Police dhidi ya raia? Tumeyaona ya Iringa na tumeyaona ya Madaktari, bado unashauri watu waende police?
Acha kujaza watu hofu, Udini unazidi kukua na kushika kasi...umesahau kauli ya Wassira huko Mwanza?
Unakataza waumini wasiende kwa viongozi wao wa kidini kuomba miongozo, je ulitaka waende wapi? Kama ni serikali..unaiongelea serikali ipi? Tusikariri wajibu wa serikali bali tutambue uwezo wa serikali iliyopo.
If we are destined to vurugu, then let that one be...si kwa kushambulia walio kinyume na imani yetu, bali kwa kuwatafuta wahuni hawa wachache watumiao mwamvuli wa dini....na ni lazima viongozi watoe kauli mapema sana kuliko kusubiri hisia zigeuke kuwa imani na ukweli vichwani mwa wengi.
 
Kwanza hawa wanasiasa hasa wa CCM ndio wanaootesha hizi mbegu za udini wakitegemea kujiimarisha kisiasa.Unakuta jambo baya limefanywa na mtu au kikundi (liwe la kisiasa au kijamii), Badala ya kulitatua kwanza kama dola, tena kwa busara..wanaanza kuhoji kwamba hawa watakuwa ni CUF au CHADEMA.The way they handle this matter create more problems.

nARUDIA KUSEMA TENA SERIKALI HII YA CCM ndiyo inayotengeneza na kupromoti UDINI, UKANDA, UKABILA.Halafu cha ajabu wanataka viongozi wa dini wawasaidie,wakipita kwenye kampeni wanawatumia pia viongozi wa kimila kwenye kampeni zao.
 
Nalaan sana mauaji ya Zanzibar
katika wiki mmoja tumepoteza viongozi wawili wa kidini

ILA SIKUBALIANA NA hoja ya MWANAKIJIJI kumtaka Mh.Kadinal PENGO atoe kauli kwa sababu zifuatazo
1.Padri hajauwawa na serikali bali na kudhi la watu possibly Waislam wana Uamsho wasiotaka Muungano
2.Kama wauwaji wa Liberatus Barlow walipatikana nadhan hawa wa Padri ni lazima serikali iwanase
3.Pengo bado ni mapema mno kwake kutoa kauli manake akiitoa tu sisi wafuasi tutatekeleza pasipo kusita.

PENGO AKUTANE NA VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALI ikishindikana alete maombi yake kwa Wakristo tutekeleze.
 
Wao ni binaadamu
wanaweza kuwa 'carried out' na emotions na hasira na uchungu
mwisho wakasema 'kuweni na tahadhari na waislam wote'
we unaonaje hapo?
fair?

Boss..tusiwe wanafki kama wanasiasa kwa kujidai hatuoni tatizo ilhali tatizo lipo...japo for a minute hebu vaa viatu vya watoto na wake wa wachungaji walio uawa....
 
The Boss, tatizo ni kwamba hao viongozi wa upande wa pili wanatoa instructions ambazo zimekuwa zikiwagharimu Wakristo. We as Christians we want our leaders to do the same
TWO wrongs do not make it right...

wakuwa held responsible ni serikali.....na sio kila mtu akimbilie kwa viongozi wa dini yake
unapinga nini,na unafanya nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom