Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,922
- 6,531
Cha kushangaza ni kwamba mbele kuna nafasi ambayo inaonekana ndiyo mpaka wa kiwanja chake, lakini sasa anaziba barabara kabisa. Swali linajiuliza, kama kweli hiyo ndiyo mipaka ya kiwanja chake, ile nafasi ya mbele aliacha kwa matumizi gani?
Kitendo hiki cha kumwaga mawe kimezuia shughuli za wananchi na matumizi ya barabara hii muhimu. Ni vyema mamlaka husika zifike eneo hilo, zihakiki mipaka halali ya kiwanja na kuchukua hatua stahiki ili barabara irejeshwe katika hali yake na wananchi waendelee kuitumia bila usumbufu.