Mwanahalisi leo latoboa ile ya ndani kabisa ya EPA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanahalisi leo latoboa ile ya ndani kabisa ya EPA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 1, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana-JF,

  Gazeti la Mwanahalisi la leo ni moto wa kuotea mbali. Ndani ya stori yao kuu ya leo kuna habari kuhusu yale aliyoyatamka Marando katika Viwanja vya Jangwani siku ya Jumamosi hadi TBC wakamkata. Leo gazeti hilo limeweka bayana kwamba Marando alikuwa anauhakika asilimia 100 kilw alichokisema -- jinsi CCM ilivyofanya hujuma kubwa ya kihistoria kwa Watanzania pale viongozi wake wakuu walipokula njama kuibia BoT mabilioni kupitia akaunti ya EPA.

  Mwanahalisi limeweka bayana, tena kwa undani kabisha na kwa ushahidi usiopingika kwamba aliyosenma Marando hayakuwa matusi au kejeli yoyote, bali ni ukweli kabisa kwamba CVCM ilituma watu kuchota mahela hayo kwa ajili ya kufanyia kampeni zilizoimwingiza JK mwaka 2005.

  Wana-JF ntajaribu kupata soft copy na kuiweka hapa muda si mrefu, ikishindikana nitajaribu kui-key story na hasa zile ibara husika. It's damaging to CCM. It really is!!!!!!
   
 2. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Tuwekee haraka ili tuikomeshe hiyo TBC inadhani kukata matangazo ndiyo kuzuia watu wasipate habari?
   
 3. M

  Msharika JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ZAK Usilale, Leta habari za huo wizi wa CCM hapa, Tendwa kawaambia lazima majimbo 100 yaondoke, tukaze buti nuru hipo karibu.
  Alunta contiinue. Nimekubonyezea thanks
   
 4. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mhmm! Nami nimelipata ngoja kwanza nisome hapa......
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi mkijua zaidi inawasaidia nini zaidi? ni kitu gai mkisikia kitawashtusha?
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280

  mada zako unazoletaga hapa we unazani huwa zinatusaidia nini?
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kimsingi hakuna jipya, kama ni Ufisadi ni ule ule ila ni vizuri mafisadi wakaelewa fika kuwa uovu wao wananchi tunaujuwa.
  Sasa mambo ni hadharani.
   
 8. R

  Ramos JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji, unadhan kila mtu anajua vyote unavyofahamu wewe? Kama ingekuwa hivyo nisingetegemea hawa wahusika wa wizi wakaendelea kushabikiwa na maelfu ya waTz...
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwani nafikiria zinawasaidia?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  thats exactly my point.. ndio maana sikuhizi kwa kweli sihangaiki kufichua ufisadi zaidi kwa sababu tumeshapigwa ganzi.. sasa hivi ni kujipanga kuushughulikia tu.. Tangu Loliondo hadi leo bado tupo hapo hapo.. kashfa kashfa kashfa..
   
 11. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Lete habari hiyo ndugu.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Sep 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi unafikiri kweli wale maelfu waliojazana Jangwani kwenye mkutano wa CCM hawajui ufisadi unaofanyika nchini? Really..?
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona mwanahalisi wanachojaribu ni kutia msisitizo ili ata wale ambao walikuwa kizani waweze ona nuru
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  tupate habari kamili
   
 15. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  MM wacha yazidi kusemwa maovu yao ili kuwakumbusha watanzania ni nani hasa hao wajao kuomba kura zao! tunacho taka ni kama ilivyokuwa operation sangara kuwafumbua zaidi macho waTz ili October wapige kura za hasira dhidi ya CCM!
   
 16. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Chadema chukueni hili jimbo. Ni muda wa kushauri kamati kuu ifanye juhudi hapa kunyakua na si kulalamika humu daily. Huyu jamaa hana shule kama mgombea mwenza wenu.

  Barua ya siasa: Njombe Kaskazini tuiadibishe CCM
  Barua ya siasa: Njombe Kaskazini tuiadibishe CCM

  SISI ni Watanzania wapigakura, wakazi wa jimbo la Njombe Kaskazini. Tunaandika kutoa maoni yetu huku mioyo yetu ikiwa ni mizito kwa uchungu usiomithilika. Kwanza tunaeleza kusikitishwa na namna zoezi zima la kura ya maoni kumsaka mgombea wa nafasi ya Ubunge toka ndani ya CCM lilivyoendeshwa jimboni kwetu.

  Kulikuwa na wagombea 11, akiwamo mbunge aliyemaliza muda wake, Jackson Makweta. Hatuna maneno na wagombea wengine kumi ila mmoja wao tu.

  Mgombea huyo pa,oja na kuwa na wadhifa mkubwa ndani ya CCM ngazi ya mkoa, hakuwa na sifa za kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge. Ni mgombea mwenye kasoro na upungugu mwingi kiasi ambacho angalazimisha vikao vya uteuzi ndani ya CCM kuliengua jina lake bila hata ya kuwa na majadiliano marefu.

  Moja ya kasoro kubwa alizonazo ni elimu. Ana elimu ndogo ya darasa la pili. Kwa kiwango hicho cha elimu hawezi kuwa na upeo mpana wa kupambanua mambo, hasa aktika karne hii ya 21 ambayo ni ya sayansi na teknolojia.

  Tanzania imeingia kwenye Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, mbunge mwenye elimu ndogo ya darasa la pili ataweza kweli kupambana na changamoto zilizoko kwenye jumuiya hiyo?
  Kwa kutambia kwamba hana sifa, uwezo wala vigezo vya kuwa mbunge, aliamua kufanya kampeni zake kwa kutumia jina la Raos Jakaya Kikwete.

  Katika kampeni zake, kwenye kura za maoni, alidai kwamba ametumwa na Rais kuja kugombea ubunge Njombe Kaskazini kwa lengo mahsusi la kumng'oa mbunge aliyemaliza muda wake, Jackson Makwetta.

  Ili kuipa nguvu hoja ya kwamba alitumwa na rais kugombea ubunge njombe Kaskazini, alidai yeye ndiye aliyemshauri rais kuunda mkoa mpya wa Njombe na wilaya mpya ya Wanging'ombe. Alidai bila ya ushawishi na ukaribu wake kwa Rais, Mkoa na Wilaya mpya vingekuwa ndoto.
  Hatuamini kama rais anaweza kumshawishi na kumuunga mkono kugombea ubunge mtu mwenye elimu duni ya darasa la pili. Kampeni za mgombea huyo ‘ngumbaro' kujinadi kuwa alitumwa na rais zilimbeba kwa kiwango kikubwa.

  Sisi wapigakura wenye uelewa tunaona kuwa CCM imeamua kutudhalilisha wazi wazi kwa kutuletea mgombea ubunge mwenye elimu duni.
  Hii ni fedheha, tena ni aibu kubwa.

  Tunadhani na kuamini udodoki aliokuwa akiuzungumzia hayati Baba wa Taifa Mwalimu nNyerere, ndani ya CCM umeshawadia. Hivyo sasa ni vyema sisi wananchi wa Njombe Kaskazini tukaiadibisha CCM kwa kutuchagulia mgombea wao.
  Tunasema jimbo la Njombe Kaskazini lipo wazi, tunawakaribisha wagombea kutoka vyama vingine.
  Tukithubutu kumchagua mgombea huyu wa CCM, tutachekwa leo hadi milele. Wali na pilau ni vya kupita, mbunge mbovu huacha makovu ya kudumu.
  Ni sisi wapigakura,
  Njombe Kaskazini.
   
 17. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Chadema chukueni hili jimbo. Ni muda wa kushauri kamati kuu ifanye juhudi hapa kunyakua na si kulalamika humu daily. Huyu jamaa hana shule kama mgombea mwenza wenu.

  Barua ya siasa: Njombe Kaskazini tuiadibishe CCM
  Barua ya siasa: Njombe Kaskazini tuiadibishe CCM

  SISI ni Watanzania wapigakura, wakazi wa jimbo la Njombe Kaskazini. Tunaandika kutoa maoni yetu huku mioyo yetu ikiwa ni mizito kwa uchungu usiomithilika. Kwanza tunaeleza kusikitishwa na namna zoezi zima la kura ya maoni kumsaka mgombea wa nafasi ya Ubunge toka ndani ya CCM lilivyoendeshwa jimboni kwetu.

  Kulikuwa na wagombea 11, akiwamo mbunge aliyemaliza muda wake, Jackson Makweta. Hatuna maneno na wagombea wengine kumi ila mmoja wao tu.

  Mgombea huyo pa,oja na kuwa na wadhifa mkubwa ndani ya CCM ngazi ya mkoa, hakuwa na sifa za kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge. Ni mgombea mwenye kasoro na upungugu mwingi kiasi ambacho angalazimisha vikao vya uteuzi ndani ya CCM kuliengua jina lake bila hata ya kuwa na majadiliano marefu.

  Moja ya kasoro kubwa alizonazo ni elimu. Ana elimu ndogo ya darasa la pili. Kwa kiwango hicho cha elimu hawezi kuwa na upeo mpana wa kupambanua mambo, hasa aktika karne hii ya 21 ambayo ni ya sayansi na teknolojia.

  Tanzania imeingia kwenye Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, mbunge mwenye elimu ndogo ya darasa la pili ataweza kweli kupambana na changamoto zilizoko kwenye jumuiya hiyo?
  Kwa kutambia kwamba hana sifa, uwezo wala vigezo vya kuwa mbunge, aliamua kufanya kampeni zake kwa kutumia jina la Raos Jakaya Kikwete.

  Katika kampeni zake, kwenye kura za maoni, alidai kwamba ametumwa na Rais kuja kugombea ubunge Njombe Kaskazini kwa lengo mahsusi la kumng’oa mbunge aliyemaliza muda wake, Jackson Makwetta.

  Ili kuipa nguvu hoja ya kwamba alitumwa na rais kugombea ubunge njombe Kaskazini, alidai yeye ndiye aliyemshauri rais kuunda mkoa mpya wa Njombe na wilaya mpya ya Wanging’ombe. Alidai bila ya ushawishi na ukaribu wake kwa Rais, Mkoa na Wilaya mpya vingekuwa ndoto.
  Hatuamini kama rais anaweza kumshawishi na kumuunga mkono kugombea ubunge mtu mwenye elimu duni ya darasa la pili. Kampeni za mgombea huyo ‘ngumbaro’ kujinadi kuwa alitumwa na rais zilimbeba kwa kiwango kikubwa.

  Sisi wapigakura wenye uelewa tunaona kuwa CCM imeamua kutudhalilisha wazi wazi kwa kutuletea mgombea ubunge mwenye elimu duni.
  Hii ni fedheha, tena ni aibu kubwa.

  Tunadhani na kuamini udodoki aliokuwa akiuzungumzia hayati Baba wa Taifa Mwalimu nNyerere, ndani ya CCM umeshawadia. Hivyo sasa ni vyema sisi wananchi wa Njombe Kaskazini tukaiadibisha CCM kwa kutuchagulia mgombea wao.
  Tunasema jimbo la Njombe Kaskazini lipo wazi, tunawakaribisha wagombea kutoka vyama vingine.
  Tukithubutu kumchagua mgombea huyu wa CCM, tutachekwa leo hadi milele. Wali na pilau ni vya kupita, mbunge mbovu huacha makovu ya kudumu.
  Ni sisi wapigakura,
  Njombe Kaskazini.
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau, nimerjaribu hapa kwa haraka kuweka kile nilichoahidi, lakini hii siyo full stori. Full stori pia imegusia masuala ua Bulyanhulu kwa undani zaidi.

  Kombora lililorushwa na muasisi wa mageuzi nchini, wakili wa Mahakama Kuu, Mabere Marando limetia kiwewe Rais Jakaya Kiwete na baadhi ya wasaidizi wake, Mwanahalisi imeelezwa.

  Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, tangu Marando atupe kombora kwa viongozi wastaafu na waliopo madarakani, kumekuwa na mkanganyiko ndani ya chama hicho.

  Kundi moja la vciongozi limekuwa likitaka Marando ajibiwe, huku kundi lingine likitaka kunyamaza, likihofia "kuyakuza na kuyaeneza nchi nzima."

  Marando akihutubia maelfu wa wananchi katika viwanja vya Jangwani jijini Dare s Salaam Jumamosi ilyopita alisema wahusika wakuu wa ufisadi katika akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), bado hawajakamatwa.

  Aliwataja ambao hawajakamatwa kuwa ni rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na mfanyabiashara Rostam Aziz.

  Alisema serikali iliyopo madarakani haiwezi kumaliza ufisadi kwa kutoa kafara baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi na kuacha vigogo waliohusika kuendelea kupata.

  Kati ya July 2005 na Januari 2006 zaidi ya Sh 133 bilioni zilikwapuliwa……………
  ………………………………………………….

  Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu za Chadema, Marando alisema watuhumiwa wenyewe wa ufisadi hawajakamatwa.

  Alisema ufisadi unaodaiwa kufanywa na mkurugenzi wa utumishi wa BoT, Amatus Liyumba au fedha za umma zinazodaiwa kuchotwa na mfanyabiasdhara Rajabu Maranda, ni sehemu ndogo sana ya fedha zilizoibwa.

  Kwa sauti ya mpasuko kwa wasikilizaji waliokaa kwa shauku ya kupokea ujumbe, Marando alisema ufisadi hauwezi kumalizwa na CCM kwa kuwa nyingi ya fedha hizo zilitumiwa na chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2005.

  Marando alikiri kuwa anatetea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika akaunti ya EPA na kwamba hiyo ni haki yao kikatiba na kisheria. Alidai kuwa anasema anayoyasema kwa vile anafahamu kilichotendeka………
  …………………………………………………………………………….
  ……………………………………………………………….

  Akiitikia kauli za wananchi za Sema! Sema!, Marando alisema, "Nasema haya kwa sababu nafahamu hawawezi kunifanya chochote.. wakithubutu nitawaumbua mahakamani."

  Wakati Marando alianza kuranda rejea tuhuma hizo, ghafla kituo cha televisheni cha TBC1 kilikatisha matangazo yake, jambo ambalo lilizusha tafrani kubwa kwa washabiki na wanachama wa chama hicho kutishia kuchoma moto gari la matangazo la shirika hilo.

  Aliyeiokoa TBC "kutoangamizwa" ni mkuu wa wilaya ya Ilala, Leonidas Gama ambaye taarifa zinasema aliwaeleza viongozi wa juu serikalini hatari iliyopo iwapo hatua za harakahazitachukuliwa kurejesha matangazo hayo.

  Gama alichukuwa uamuzi huo baada ya mwenyekiti wa taifa wa Chadema Freeman Mbowe kuomba msaada wa ulinzi kutokana na kuwapo tishio la kutaka kushambulia wafanyakazi wa TBC na kuchoma moto vifaa vyao yakiwamo magari.

  Mkuu wa wilaya huyo alikuwa miongoni mwa wageni kutoka serikalini walioalikwa kuhudhuria mkutanoi wa Chadema…………….

  Siku moja baada ya ya Marando kutuhumu viongozi wa CCM kuchota fedha za umma kupitia akaunti ya EPA, Meneja wa Kampeni wa chama hicho, Abdulrahman Kinana aliitisha mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam kujibu madai ya Marando. ………

  Kinana alisema, "CCM imesikitishwa na kauli (za Marando), hasa ikizingatiwa kuwa aliyetoa tuhuma hizo ni mwanasheria." Akashauri viongozi wakuu wa Chadema kuacha kutoa kile alichoita "uzushi na kebehi.."

  Baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wamedai katika hati zao za kiapo kwamba baadhi ya fedha walizochukuwa walizikabidhi kwa Salome Mbatia, ambaye wakati huo alikuwa mweka hazina wa chama hhicho. Ni marehemu.

  Kwa mfano, mmoja wa watuhumiwa wa EPA, Jeetu Patel, katika kesi iliyopo mahakamani, ameeleza katika kiapo chake kwamba karibu asilimia 60 ya fedha alizopewa alizikabidhi kwa baadhi ya viongozi wakuu akiwemo (Salome) Mbatia.

  Anasema fedha nyingine zilitumika kuingiza magari aina ya Hindra ambayo yalitumiwa na CCM katika kampeni zake mwaka 2005.

  Taarifa za kuaminika zinasema watuhumiwa wengi wana nyaraka ambazo pale zitakapowasilishwa mahakamani, zitabadili mkondo wa tuhuma………………..


  My Take (kwenye red):

  Taarifa ambazo ninazo ni kwamba Marando ndiye chanzo cha habari zote hizi katika Mwanahalisi, na pia kwamba mwanasheria huyo machachari ataingia kwa undani zaidi kuhusu suala hilo la uchotaji wa EPA katika mikutano ijayo ya kampeni za Chadema.
  Mfano, Jeeti Patel hakurudisha hela yoyote ya EPA aliyolipwa na ndiyo maana alitinga mahakamani. Katika kiapo chake alidai vipi arudishe iwapo hela nyingi walichukuwa wao CCM na kwamba wao walitumiwa kama conveyor belts.
   
 19. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Yapo mengi ya design ya Njombe Kaskazini!! Hayo mengine kama si elimu basi ni mvundo mwingineo. Hapo ndipo pazuri kwa wapinzani. Kwa kweli inaleta karaha kisiasa.
   
 20. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  You have a point, lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa desperate, ni muhimu pia kuendelea kuipiga ngoma hiyo bila kuchoka ili jamaa wasipate usingizi wa amani kabisa; wajue kuwa kweli mambo yameharibika; the topic just won't go away by mere wishing. Na uzuri wake wanazidi kuharibu kwa kuwanyanyasa wananchi kwa kauli mbovu za jeuri kama "hatuna hela hizo hata wakigoma kwa miaka minane ...; kama ni kura zao potelea mbali sizihitaji". Hawa watu waajabu sana. Wanaahidi meli; hospitali za rufaa; viwanja vya kimataifa; ... kama vile tunaishi nchi nyingine au uwezo wetu wa kufikiri ulikufa siku nyingi! Lazima waendelee kukumbushwa hujuma kuu walizolitendea taifa hili ambazo mfumo wake bado wanaendelea kuulea. They shouldn't be allowed sweet dreams but unending nightmares until they either repent or get thrown off the stage.
   
Loading...