Habari ya uongo kuhusu deni la Taifa: Mwananchi walikosea au walidhamiria?

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,318
HABARI YA UONGO KUHUSU DENI LA TAIFA KUONGEZEKA KWA TRILION 12 BADALA YA TRILION 3 NDANI YA MIEZI 3 |¦| Mwananchi Walikosea au Walidhamiria??

Mimi siyo mtaalamu wa masuala ya uandishi wa habari na mawasiliano, ila wataalamu wa masuala ya habari na mawasiliano wana kitu wanachokiita 'yellowish journalism' kwa tafsiri isiyo rasmi, hii ni aina ya uandishi wa habari ambao mwandishi huandika makusudi kwa lengo la kupotosha ukweli (misinformation or hoax). Habari za aina hii zinaweza kusababisha matatizo makubwa, usumbufu na hata kutumbukiza jamii ktk sintofahamu au hata migogoro isiyokoma au vita.

Mathalani, mwaka 1475 ktk mji wa Trentino-Italy, ilizushwa habari ya uongo ya kwamba Wayahudi wamemuua mtoto mwenye umri wa miaka miwili na nusu aitwaye Simonimo. Habari hizi, zilienenzwa kupitia machapisho, nyumba za ibada za Wakristo na vijiwe. Habari hii ya uongo iliyozushwa ilipelekea Wayahudi wote ktk huo mji kukamatwa na kuteswa sana, 15 kati yao walichomwa kama ndafu. Habari zinaeleza kuwa mpaka kufikia hatua ya Papa Sixtus IV kuchukua hatua na kujaribu kuingilia habari hiyo ya uongo ili kuzuia hatari iliyokuwa ikiendelea kutendeka dhidi ya Wayahudi, tayari alikuwa amechelewa maana madhara yake yalikuwa yamekuwa makubwa na wengi wameumizwa vibaya.

Stori za uongo na uzushi za aina hii zilikuwa zikianzishwa na makundi mbalimbali kujaribu kuuaminisha umma kuwa Wayahudi walikuwa wakiwaua wakristo, hususani watoto wa kikristo kwa ajili ya kufanyia matambiko, japo haikuwa kweli, lengo la makundi yaliyokjwa yakieneza uongo huu walitaka kuwachafua wayahudi mbele ya macho ya wakristo na wananchi wengine. Makundi haya yalikuwa yakibuni tuhuma na habari za uongo dhidi ya Wayahudi ili kuwajengea chuki na hata kuwachonganisha na jamii, kwasababu hakukuwepo na aliyejali au kuwahi kuchukua hatua, wayahudi walijikuta wakiteswa na kudhurumiwa mara kwa mara kwasababu ya habari za uongo.

Baada ya uvumbuzi wa magazeti mwaka 1439, usambazaji wa habari kwa njia ya machapisho na majalida ulisambaa na kukua, lakini hakukuwepo na miiko ya uandishi iliyopaswa kufuatwa na kuheshimiwa ktk kuhakikisha kuwa kinachosambazwa kwenye hayo magazeti au machapisho mbalimbali ni habari za kweli na siyo habari za uongo, kupotosha na za kuudanganya umma kwa maslahi ya mtu, au kundi flani la watu kwasababu ya faida kibiashara, au kiitikadi, kisiasa au ajenda za siri za kuipindua serikali nk. Baada ya mwanasayansi wa kale aitwaye Galileo Galilei kushtakiwa, ndipo haja na umuhimu wa kudai habari zilizothibitishwa ulipoanza kupamba moto, hii ni kwasababu habari za uongo zilitumika kuhukumu watu na hata. kupotosha ukweli nk

Pia, katika karne ya 18, wachapishaji wa habari za uongo na upotoshaji walikuwa wakipigwa faini na hata kupigwa marufuku ktk nchi mbalimbali duniani kama vile Netherlands. Mwandishi wa kale wa Netherlands aliyejulikana kwa jina la Gerard Lodewijk van de Macht alifungiwa mara nne na utawala wa ki-dutch, lakini bado alianzisha gazeti jipya kwa mara nne zote alizofungiwa. Marufuku hizo lililenga kupambana na habari za uongo na waandishi wa habari za upotoshaji na waandishi nao waliendelea kuwa wabunifu kila. kukicha ukimgungia gazeti A, anaanzisha gazeti B na kuendelea. Hali iko hivyo hata Tanzania (Mawio na Mwanahalisi)

Katika karne ya sasa ya teknolojia ya mawasiliano, utafiti unaonyesha kuwa habari ya uongo inasambaa zaidi ya habari ya kweli. Ikiwa mamlaka zinazohusika zisipokuwa makini, habari ya uongo inaweza kusababisha taharuki, machafuko, ugomvi, chuki, na hata upotoshaji.

Moja ya Yellowish Journalism kwa hapa kwetu Tanzania ni ile habari iliyowahi kuandikwa na Saed Kubenea kupitia gazeti lake la Mwanahalisi iliyosema kuwa 'Ben Saanane alikuwa amejificha ili kutafuta umaarufu wa kisiasa ndani ya chama' kwasababu Mwanahalisi na Saed Kubenea ni mwandishi aliyekuwa amejizolea umaarufu mkubwa kwa wafuasi wake hao kwa miaka mingi.

Habari hiyo ilizua tafrani na hata kusababisha baadhi ya watu waone kuwa huenda Chadema inajua kinachoendelea kuhusu Ben au huenda Ben anachezea hisia za watu kwa kuhadaa kuwa ametekwa (Japo ukweli ni kwamba mpaka leo Ben Saanane hajulikani alipo, licha ya Saed Kubenea na Mwanahalisi yake kusema amejificha).

Saed Kubenea kama mbunge wa Chadema, andiko lake la kupotosha lilichangia kwa kiasi kikubwa watu kuanza kudhihaki suala la kupotea kwa Ben Saanane, na kusababisha lisichukuliwe kwa uzito uliostahili.

Katika hili la Mwanahalisi na Saed Kubenea, sote tulishuhudia jinsi ambavyo vijana waliokuwa wafuasi wa gazeti hili kwa miaka mingi walivyojitokeza hadharani kulaani vikali kuhusu kile walichokiita UPOTOSHAJI wa makusudi uliofanywa na gazeti hili, hali iliyo wachanganya watu wasijue nani anasema ukweli kati ya wale waliokuwa wakisema Ben ametekwa au Mwanahalisi/Kubenea aliyeendelea kusisitiza kuwa kwa habari zao za uchunguzi Ben Saanane hajatekwa bali amejificha ili kutafuta umaarufu (Jambo ambalo gazeti hili halikuwa na ushahidi nalo, ila huenda walifanya hivyo kwa malengo yao binafsi au kuna jambo walilokuwa wakilifahamu ambalo sisi wengine hatukulijua).

Mbali ya hii habari kuwa-mislead wengi na kuwafanya wasijue waamini lipi, Ikumbukwe kuwa Mwanahalisi na Saed Kubenea hakuwahi kuomba radhi kuhusiana na habari hiyo, wengi walitegemea japo kiongozi wa chama amuonye Kubenea lakini kitu kama hicho hakikutokea, sijui kwanini lakini natumai ipo siku tutajua malengo ya Mwanahalisi yalikuwa ni yapi.

[HASHTAG]#KENYA[/HASHTAG] wamefanya nini??

Mwezi huu tumeshuhudia Rais Uhuru Kenyatta akitia saini ule Muswada wa Sheria za Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni wa 2018 kuwa Sheria, hatua hii itatotoa adhabu kali kwa wote watakaopatikana na makosa ya mtandaoni.

Sheria hiyo mpya inatoa adhabu ya faini ya Ksh 5 milioni (dola 50,000 za Marekani) sawa sawa na Shilingi milioni 114 za Tanzania au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa yeyote atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uongo na uzushi. Pamoja na jumuiya za waandishi wa habari kuandama na kupiga kelele kumtaka Uhuru Kenyatta asiukubali huo mswada kuwa sheria, jibu walilopewa ni kuwa KWANI NYIE HUWA MNAANDIKA HABARI ZA UONGO? Kama mnaandika si muache kuandika habari za uongo na muanze kuandika habari za kweli??

Jibu hili linafikirisha sana, maana kama wewe ni mwandishi unayeheshimu miiko ya kazi yako, na unaifanya kazi yako kwa weledi unaweza vipi kuandika habari ya uongo ktk gazeti au mtandaoni??

[HASHTAG]#Nchini[/HASHTAG] Kwangu Tanzania

Hii habari iliyosambazwa kwa kasi na gazeti la Mwananchi ikisema kuwa deni la taifa limeongezeka kwa trilioni 12 ktk kipindi cha miezi mitatu pekee, ni moja ya habari za uongo na upotoshaji zinazoonyesha ni kwa kiasi gani vyombo vyetu vya habari visivyozingatia weledi ktk ufanyaji kazi wao. Hakuna aliyebisha kuwa deni hfslijaongezeka, ila watanzania walio wengi wanahoji kwanini chombo cha habari kiamue kupotosha bayana bila kujiridhisha kuhusu kiwango cha hilo deni lililoongezeka ktk kipindi cha miezi 3??

Kwamba kuanzia mwandishi wa habari yenyewe mpaka wahariri wote wa gazeti zika hakuna aliyeona au kutilia mashaka upotoshaji huo, wala hata kuhangaika kutafuta ufafanuzi zaidi kutoka mamlaka husika!?? Mwananchi ilidhamiria kuzua taharuki au ilikosea ?

Hii ni habari ya uongo ambayo imewasikitisha wengi sana, watu pekee ambao hawajaguswa na hili ni jukwaa la wahariri(TEF), Umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), Baraza la vyombo vya habari (MCT) maana sijasikia wakikemea kuhusu hili, huenda kwao hawaoni iwapo ni kosa au huenda meno ya mbwa hayaumani. Nilitamani kusikia hata Kidjo Bisimba wa LHRC akikemea maana watanzania wana haki ya kupata habari za kweli na siyo uongo na upotoshaji, au huenda siyo lazima sana, au tutamsikia siku chombo cha habari kikifungiwa kwa kuandika habari za uongo na upotoshaji.

Kuna wakati dhana upotoshaji kuhusu udhaifu wa serikali husababishwa na serikali yenyewe, kwanini nasema hivyo? Serikali husababisha yote hayo kwa kuendelea KUVUMILIA mazoea ktk makosa hatari kama haya ambayo hufanywa na mtu au makundi ya watu flani flani kwa makusudi ila kwa ujanja na weledi wa hali ya juu sana wakiwa na malengo flani flani ya kibinafsi kutengeneza faida, kiitikadi au hata kisiasa.

Kwa sababu ya mazoea, mamlaka zenye wajibu wa kuhakikisha kuwa zinasimamia weledi na nidhamu ktk maeneo mbalimbali hushindwa kuchukua hatua za haraka za muda mfupi au hata mrefu ili kupambana na aina hiyo ya upotoshaji kuhusu serikali au mamlaka za serikali, wakati mwingine kutokana na uzembe wa watendaji, udhaifu wa kimfmo wa mamlaka husika, au hata mianya ktk sheria zinazosimamia masuala ya habari magazeti na mawasiliano. Serikali inapaswa kuangazia hili, kama sheria zilizopo hazitoshelezi mahitaji, kuna haja ya kufanya marekebisho ya sheria ili kuenenda na mahitaji ya sasa, bila hivyo ipo siku nchi itatumbukizwa ktk migogoro na machafuko kutokana na magazeti au vyombo vya habari vinavyotoa habari za uongo na upotoshaji kuendelea kuruhusiwa bila kupigwa marufuku.

Kama chombo cha habari cha ndani kinaweza kuandika habari nyeti na tata kama hii ya deni la taifa kukua kwa Trilion 12 ndani ya miezi mitatu, tusidhani hii ni sifa nzuri ktk weledi wa uandishi wa habari, habari iliyosababisha taharuki kama hii kisha adhabu yake ikawa kuomba radhi usitegemee hiyo radhi itawafikia wote waliopotoshwa na habari hizo za uongo, kama kweli ni za uongo, na tusitegemee waandishi wengine au vyombo vingine vitakuwa makini ikiwa adhabu ya kwanza ni kuomba radhi.

Katika nchi inavyopambana kunyenyuka kiuchumi, nchi ambayo jitihada kama hizi haziwafurahishi mataifa makubwa yanayotamani mataifa yenye rasilimali nyingi kama Tanzania yanaendelea kuwa tegemezi kiuchumi, katika nchi kama Tanzania ambayo inapambana kukua sekta ya viwanda japo inakabiliwa na changamoto nyingi hatutegemei kuwa na magazeti au vyombo vya habari vinavyoweza kuandika habari nyeti 'sensitive' kama hii bila kupata ufafanuzi kutoka BOT kuhusu deni la taifa, hii ni hatari na ninasikitika kuwa adhabu watakayopewa ni kuomba ya radhi bila. kuzingatia usumbufu waliosababisha.

Leo unaweza kuanzisha gazeti, ukalisajiri kwa mujibu wa sheria kisha ukaandika habari yoyote ya uongo na ukazua taharuki, ukapotosha na kudanganya harafu kesho yake ukaomba radhi kwa mujibu wa sheria na ukawa umemaliza.

Baada ya miezi miwili unaandika habari nyingine ya uongo, ukaonywa na mamlaka husika, unaomba radhi hadharani kwa mujibu wa sheria umemaliza, ukiendelea zaidi na zaidi unaweza kufungiwa na gazeti moja au chombo kimoja cha habari kikifungiwa hauzuiliwi kufungua au kuanzisha chombo kingine cha habari au gazeti jipya, ni uamuzi wako tu, kulingana na uwezo wako wa kimtaji.

Je sheria zetu ni imara kiasi gani kupambana na habari za uongo zinazoweza kusababisha taharuki ktk nchi? Je kuna haja ya kutazama upya sheria zetu ktk hili??

Magoiga SN
 
Hata wewe uliyeandika hapa unaeneza habari za uongo. Tanzania haidaiwi popote. Tanzania yenye uchumi wa gesi ishindwe ulipa madeni? Acha uongo na uchochezi
 
Huyo mama Kiiijo binti Simba uliye mtaja ndio BUUURE KABIISA! Habari za UZUSHI dhidi ya Serikali atazivalia njuga kama katoka unyagoni leo!
 
Deni la taifa ni mwiba mkali, nao wanaingia kwenye orodha ya kupiga u.turn kuyakanusha maandishi yao baada ya CAG kufanya hivyo kabla, nafikiri deni hili tuliache likue tu na tusilijadili wala kuliandika popote kwa vile halitunyimi usingizi
 
Regardless ya uongo wa Deni la trilioni 12 kwa miezi mitatu, Kinachohuzunisha zaidi ni wengi wetu kufikiria kuwa deni la Trilioni 3 kwa miezi mitatu ni jambo dogo sana.
 
teheteheee.Hi ndio Tanzania bhana.awamu hii,kila ukweli kwao huwa ni uongo tuu,baaasi.
 
Back
Top Bottom