Nimeipata nyingine hii kutoka Mwanahalisi la leo Ukurasa wa 11 -- makala iliyoandikwa na Saed Kubenea inayozungumzia matamshi ya Kinana. Hii inazidi ku-prove alichokisema Marandi Jumamosi ni kweli kabisa na kwamba safari hii CCM wameminywa sehemu mbaya sana. Paragraphs husika:
………."hata ndani ya Kamati ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi iliyoundwa na chama chake kutafuta suluhu ya migogoro ndani ya Bunge na katika Chama, suala la CCM kujinufaisha na fedha za EPA liliibuka.
Mjadala ulipopamba moto, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (utawala Bora), Sophia Simba alijitokeza na kukaripia wanaotuhumu. Akiongea kwa sauti iliyojaa mipasho, waziri Simba alimtuhumu Anne Kilango Malecela kuwa ni miongoni walionufaika na fedha za EPA.
Alisema Kilango alinufaika na fedha hizo kupitia kwa mfanyabiashara Jeetu Patel aliyekuwa anafadhili kampeni za mume wake, John Samuel Malecela. Kauli ya Simba ilitokana na hoja kadhaa zilizokuwa zinajengwa na baadhi ya Wabunge akiwamo Kilango, kwamba serikali imeshindwa kushughulikia ufisadi wa EPA kwa sababu baadhi ya fedha zilizoibwa zilinufaisha chama hicho.
Wabunge hao waliokuwa wamepachikwa jina la "Makamanda wa Ufisadi" walilenga mabilioni ya fedha yaliyokwapuliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited. Kampuni ya Kagoda ilichota zaidi ya Sh 40 bilioni kupitia BoT.
(Sophia Simba) alisema. "Mimi ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri. Hata Takukukuru iko chini yangu. Idara ya usalama wa taifa iko pale kwangu. Mlango wangu uko karibu na lango la rais. Nafahamu kilichotendeka."
Aliongeza, "Nafahamu kwamba baadhi ya fedha za EPA ambazo leo Kilango anatuhumu zimetunufaisha baadhi yetu, zilinufaisha hata kampeni ya mumewe."
Hakuna hata mahali popote ambapo CCM ilikana madai ya Simba.
Pamoja na kwamba Kinana alikuwa mjumbe katika kamati ya Mwinyi, na kwamba yeye na katibu mkuu wake, Yusuph Makamba walihudhuria mkutano uliomtuhumu Kilango, lakini hawakujitokeza kukana kauli ya Simba.
Hii ni kwa sababu, Kinana alijua kuwa yeye na Simba katika kujua siri za sereikali, wako tofauti. Mwenzake ni waziri anayehitajika kila wakati katika kazi za kuendesha serikali, yeye (Kinana) huwa anatafutwa wakati wa kampeni tu.
Aidha, Kinana anajua kuwa tofauti na waziri Simba anayehudhuria vikao vya baraza la mawaziri, anayeshiriki mipango ya uendeshaji wa serikali, yeye (Kinana) hulazimika kusubiri ripoti ifikishwe kwenye vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC). Isipotolewa basi!
Pili, tofauti na Sophia Simba, Kinana hana ubavu wa kusoma mafaili ya watuhumiwa wa ufisadi wanaochunguzwa na Takukuru. Hivyo basi, hawezi kujua nani ameiba nini, wapi na kwa kushirikiana na nani?
Hawezi kujua kwa ufasaha kwamba Jeetu Patel alisema nini katika kiapo chake mbele ya Kamati ya Rais ambayo mtendaji mkuu wa Takukuru, Edward Hoseah alikuwa mjumbe.
Hafahamu kwa undani kwa nini Jeetu amegoma kurejesha fedha zilizokwapuliwa na nini ameegemea………………………..