CCM, gazeti la Uhuru na nia ya kuleta machafuko nchini

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Wana jf; wanaoweza kupata gazeti la uhuru leo wasome, walinganishe na kilichosomwa jana kwa waandishi wa habari, ili tujue hili gazeti linalomilikiwa na chama tawala, ukiachilia mbali maadili ya uandishi lakini yaliyoandikwa yapo katika tamko la CHADEMA? Kwanini unaandika kisichokuwepo ukisingizia kuwa ndicho walichosema? Kama inawezekana mwandishi wa habari wa gazeti hilo hakwenda kwenye press amepewa story na mtu pembeni, mhariri huwezi kuomba kopi ya tamko ili uhariri habari yako itoke? Tunachafua nchi kwa manufaa ya nani? Tunaielekeza nchi wapi? Kwa leo siulizi mengi wasomaji wanajua.

Watu wote mnaoitakia mema nchi yetu Tanzania, someni gazeti la Uhuru 19/12/2012, mlinganishe Kilichoandikwa ukurasa wa mwanzo wa gazeti hilo, na someni pia Taarifa ya CHADEMA kuhusu maamuzi ya Mkutano Mkuu iliyotolewa kwa vyombo vya habari ili muangalie kama:
• Chadema wametangaza machafuko,
• Wamedai nchi haitatawalika,
• Ukata waisambaratisha M4C
• Kama hayo hayapo katika Tamko la CHADEMA- Uhuru wameyachukua
wapi?
• Wametabiri vipi machafuko hayo ambayo hayajatangazwa na
wanaowasingizia?
• Kati ya Tamko la CHADEMA na Gazeti hilo linalomilikiwa na CCM
nani ni mchochezi? Anayekusudia kuleta machafuko?

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA MKUTANO WA
KAMATI KUU YA CHADEMA ULIOFANYIKA TAREHE 15 NA 16
DISEMBA 2012

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imefanya mkutano wake wa kawaida wa siku mbili tarehe 15 mpaka 16 Desemba, 2012 Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa Kamati Kuu ulijadili ajenda mbalimbali ikiwemo yatokanayo na mikutano miwili ya Kamati Kuu iliyopita, taarifa ya hali ya siasa,mapendekezo ya mwenendo wa Operesheni za vuguvugu la Mabadiliko (M4C) na taarifa kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba na kufanya maamuzi mbalimbali.

CHADEMA, inachukua fursa hii kueleza baadhi ya masuala yaliyojiri na maamuzi yaliyofikiwa kama ifuatavyo:

Mosi, Kamati kuu imetaarifiwa kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Rais Jakaya Kikwete juu ya hoja ya kuundwa kwa Tume ya Kimahakama/kijaji kuchunguza mauaji na haja ya Rais ya kuchukua hatua. Kamati Kuu imeazimia kwamba Rais akumbushwe mwezi Desemba 2012 kujibu barua kama alivyoahidi na mwendelezo wa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) mapema 2013 utumike kuishinikiza serikali iwapo hatua Stahiki zitakuwa hazijachukuliwa.

Pili, Kamati Kuu imetaarifiwa juu ya kucheleweshwa kwa chaguzi za marudio za Udiwani, mitaa, vijiji na vitongoji katika maeneo mbalimbali nchini na kuazimia kwamba uongozi wa CHADEMA katika maeneo husika uunganishe umma kufanya shinikizo la kisiasa kwa mamlaka zinazohusika kutangaza nafasi kuwa wazi na vyombo vinavyosimamia chaguzi katika ngazi hizo ili haki za kikatiba na kisheria za wananchi kupata uwakilishi ziweze kupatikana kwa wakati.

Tatu, Kamati Kuu imezingatia hatua ya serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukwepa wajibu wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura toka Mwaka 2010, hali yenye kuathiri haki za wananchi kupiga kura na matokeo ya chaguzi za marudio zinazofanyika na kuazimia kwamba kambi rasmi ya Upizani inayoongozwa na CHADEMA ichukue hatua za kibunge kuhakikisha kwamba daftari linaboreshwa mwaka 2013 ikizingatiwa kuwa daftari hilo litatumika kwenye kura za maoni za katiba mpya

Nne, Kamati Kuu imepokea taarifa ya awali kuhusu mchakato wa katiba mpya na kubaini upungufu katika mchakato unaoendelea hali ambayo inaweza kukwamisha upatikananaji wa katiba mpya na bora mwaka 2014 kama ilivyotangazwa na serikali na Tume husika. Kamati kuu imeazimia kwamba kamati ndogo ya Kamati Kuu ikutane kwa haraka na kufanya tathimini zaidi na kutoa taarifa kwa umma. Aidha kamati kuu hiyo iwasilishe mapendekezo kwa tume ya mabadiliko ya katiba juu ya maoni ya CHADEMA ya kuzingatiwa katika katiba mpya na mapendekezo kwa serikali juu ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba awamu ya pili nay a tatu kwa pamoja ili nchi ipate katiba mpya na bora yney muafaka wa kitaifa.

Tano Kamati Kuu imeazimia kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, itumie njia mbalimbali za kibunge kupitia hoja binafsi au Miswada binafsi kuwailisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya katiba mpito kuhakikisha tume huru ya uchguzi na marekebisho ya sheria zinazosimamia uchguzi yanafanyika kabla ya katiba mpya kwa kuzingatia kuwa kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba kura ya maoni ya katiba mpya itasimamiwa na tume ya sasa kwa mfumo wa kikatiba na kisheria usio huru.

Sita, Kamati Kuu imepokea ikiwa ni sehemu ya hali ya siasa imetaarifiwa kuhusu hoja binafsi zilizowasilishwa na wabunge wa CHADEMA, Halima Mdee, (ugawaji kiholela wa ardhi) na Zitto Kabwe (kuhusu fedha zilizofichwa nje ya nchi) na maazimio yaliyopitishwa na Bunge kuhusu hoja hizo. Aidha Kamati kuu imetaarifiwa kuhusu kusudio lililotolewa na Tundu Lissu kuhusu hoja ya utezui wenye kasoro wa baadhi ya majaji. Kamati Kuu imeazimisa kwamba Kambi Rasmi ya Upinzani inyoongozwa na CHADEMA ifuatilie kwakaribu serilai kuhusu hoja hizo na kupendekeza hatua za ziada za CHADEMA kuwaunganisha wananchi iwapo hakutakuwa na uwajibikaji unaohitajika.

Saba; Kamati Kuu ikiwa ni matokeo yatokanayo na vikao vilivyotangulia imepokea taarifa ya kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma mbalimbali wilayani karatu zenye athari kwa utendaji wa chama mathalani tofauti baina ya viongozi, ugawaji wa ardhi ya shule ya sekondari welwel, uchimbaji wa visima katika kijiji cha Ayalabe na malalamiko kuhusu uendeshaji wa Mamlaka ya Maji Karatu (KAVIWASU). Kamati Kuu imepokea mapendekezo ya kamati hiyo pamoja na maoni ya sekretarieti ya Chama na kuamua kuisimamisha
kamati nzima ua utendajiwa Chama Wilayani Karatu na kuweka wilaya hiyo chini ya Uangalizi wa Kamati Kuu ya chama Taifa mpaka hapo hatua za ziada zitakapochukuliwa.

Kamati Kuu imebaini pia kuwa masuala ua ugawaji wa maeneo ya ardhi ya shule ya Welwel yalianza kufanywa na Mkuu wa Wilaya na viongozozi wengine wa CCM na pia zipo taarifa potofu zinazotolewa kuhusu masuala hayo. Hivyo, kamati Kuu imeunda jopo la wanasheria likiongozwa na Mabere Marando na prof. Abdalla Safari kufanya mapitio ya ripoti hizo, vielelezo vya ziada na kutoa mapendekezo ya hatua zaidi katika Mkutano ujao wa Kamati Kuu. Aidha, wakati hatua hizo zikiendelea kuchukuliwa, CHADEMA taifa kitafanya mikutano na wananchi Karatu kuwajulisha hatua zilizoanza kuchukuliwa.

Nane; Kamati Kuu imepokea taarifa ya awali kuhusu yaliyojiri Jiji la Mwanza baada ya hatua ya Kamati Kuu kuafukuza madiwani wawili kwa kwenda kinyume na katiba na maadili ya Chama, pamoja na mambo mengine Kamati kuu ilitaarifiwa kuhusu uchaguzi wa Umeya katika Halmashauri ya Ilemela uliofnyika kinyume na sheria za Serikali za Mitaa na Kanuni za Halmasharui sanjari na hatua ya kufukuzwa kwa madiwani wengine wa CHADEMA na Meya huyo kinyume cha Sheria na Kanuni Kati kuu ilitaarifiwa hatua za kisheria zinazoendelea kuchukuliwa na kuazimia hatua hizo ziendelee. Aidha pamoja na hatua za kisheria kuendelea, kamati Kuu imeazimia kwamba hatua za kisiasa za kutaka uwajibikaji kwenye Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuunganisha nguvu ya Umma ili haki itendeke ziendelee kwenye masuala mengine ya ziada na taarifa iwasilishwe kwenye kamati kuu ijayo kwa ajili ya hatua zaidi.

Tisa; Kamati Kuu imetambua kupitia Taarifa ya hali ya siasa kwamba CCM na serikali kupitia maazimio ya Mikutano, ziara na kauli mbalimbali imeendelea kuahidi kutekekeleza sera za CHADEMA kuhusu elimu, gharama za vifaa vya Ujenzi, katiba mpya na nyinginezo ambazo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 walizipinga. Kamati kuu imezingatia kwamba hatua hiyo ni uthibitishao wa ziada wa CHADEMA kuwa na sera na propaganda za CCM dhidi ya sera hizo kushindwa. Hata hivyo CHADEMA inatambua kwamba CCM haina uwezo na uwajibikaji wa kuzitekekeleza sera hizo kwa ufanisi kama ambavyo CHADEMA ingekuwa katika uongozi wanchi; hivyo Kamati Kuu inaendelea kuhimiza wananchi kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa kupitia Chaguzi za Mwaka 2014 na 2015. CHADEMA itaendelea kufanya mapitio na sera zake nyingine zaidi ili kuziboresha na kuziendeza kupitia operesheni na vuguvugu la mabadiliko.

Kumi, Kamati Kuu imepokea mapendekezo ya mwendelezo wa Operesheni na M4C na kuazimia kwamba Sekretarieti ifanye tathimini zaidi kuboresha mpango/mfumo/muundo wa utekelezaji na kutangaza ratiba kwa umma mapema mwaka 2013 ikiwa ni sehemu ya kufanikisha mikakati ya CHADEMA na kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Chama na taifa kwa ujumla.

Kamati Kuu imepitia maamuzi na Maazimio mengine ya ziada kuhusu hali ya siasa ambayo umma utaendelea kujulishwa hatua kwa hatua na kuzingatia katiba, kanuni, maadili na itifaki ya Chama.

Wenu katika Demokrasia na Maendeleo
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Taifa.
 

Attachments

  • UCHOCHEZI.pdf
    70.2 KB · Views: 165
Hapa umetupa mtihani mkuu, maana kuna wengine humu hawana uwezo wa kulipata hilo gazeti. Na zaidi sana hata tungeweza kulipata, mimi binafsi sipo tayari kutoa hela yangu kuichangia CCM kupitia hilo gazeti lao. Ungekuwa umetusaidia sana, kama ungeandika hicho kilichoandikwa ndani ya gazeti la uhuru.
 
nyie wana jf vipi.Mnahangaika na gazeti ambalo halifai hata kufungia mandazi? kuna baba yangu mmoja ambaye ni mjumbe wa nyumba kumi(CCM) wa kujiteua tena mkulima wa jembe la mkono na kilimo cha kujikimu anaenda kiM4C. nakusanya nguvu niende nikasilimishe ukoo mzima kutoka CCM kwenda CDM as soon as posible.
 
Haa! hilo Gazeti sijalisoma miaka mingi wala sishangai kusikia wameandika mambo ya kijinga maana akili zao zimeishia hapo.
 
Labda hawana cha kuandika.:sick:
kuna badiko moja hapa janvini linasema tanzania imeorodheshwa kwenye nchi za kuchunguzwa na ICC, hao uhuru waangalie katika ilie list ya Kenya inajumuisha na mwandishi mmoja kanjanja kama wao
 
Picha hii ni kwa hisani ya mjengwa blog.

DSC00060.JPG
 
Huyo mhariri wa Uhuru anajitakia matatizo kama yaliyomkuta yule mtangazaji wa radio wa Kenya - Joshua Sang! Ana kesi sasa hivi ICC.
 
Usijisumbue na gazeti hilo ndugu yangu halifai hata kwa kufungia vitumbua, just ignore it lina propaganda za kijinga na kishamba inaonekana waandishi wake hawajabobea kwenye taaluma ya uandishi, mi siku zote bora nitupie jicho kwenye gazeti pendwa kuliko Uhuru.
 
Picha hii ni kwa hisani ya mjengwa blog.

DSC00060.JPG

Wikolo asante sana kwa kutusaidia kupata nakala ya gazeti hili ili kupanua wigo wa mjadala. Nadhani Mwandishi wa uhuru na Mhariri wake wanaweza hata kwa kubold kwenye tamko Kauli zao walinukuu wapi point zao na katika aya zipi za tamko walilosema kuna machafuko na nchi haitatawalika.............CCM namba One hata kwa uongo jamani
 
Kweli kaka gazeti la uhuru ni feki na waandishi wake sidhani kama wameiva sawasawa au labda propaganda zinawasumbua
Usijisumbue na gazeti hilo ndugu yangu halifai hata kwa kufungia vitumbua, just ignore it lina propaganda za kijinga na kishamba inaonekana waandishi wake hawajabobea kwenye taaluma ya uandishi, mi siku zote bora nitupie jicho kwenye gazeti pendwa kuliko Uhuru.
 
Wajameni mimi binafsi nakumbuka nilinunua gazeti hili na kulisoma ilikuwa mwaka 1984 mwezi April

Ilikuwa ni kwa ajili ya kufuatilia taarifa za kifo cha Waziri Mkuu, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Tokea hapo walaahhhhhhhhh sina muda sina muda kabisa na sina pesa ya kuchezea


MIZAMBWA
NABII MTARAJWA!!!
 
Back
Top Bottom