MwanaHalisi ladai Ben Saanane huonekana kwa jamaa zake

hilo gazeti umelinunua wewe

ukaamua kulitia moto wewe

ukalipiga na picha wewe

haitoshi ukaona wewe

kuwa vema uanzishe na uzi wewe

goli lako ni nini hasa?
 
Sijaelewa mantiki ya hiyo posti yani ningekuwa nagawa maksi basi wewe ungekua umefaulu kufeli kwa alama miamoja
 
MSAADA NDUGU ZANGUNI :

Tamko la Serikali kuhusu kuyafanya masomo ya SAYANSI kuwa ya LAZIMA kwa Shule za Sekondari (forms 1 - 4) linapatikana katika Waraka upi wa Serikali?

Nitangulize shukrani.
 
MSAADA NDUGU ZANGUNI :

Tamko la Serikali kuhusu kuyafanya masomo ya SAYANSI kuwa ya LAZIMA kwa Shule za Sekondari (forms 1 - 4) linapatikana katika Waraka upi wa Serikali?

Nitangulize shukrani.
Mkuu Mutarwe, kwanza karibu jf.

Pili humu jf kuna majukwaa mbali mbali, ukitaka kuzungumzia issue yoyote unakwenda jukwaa husika utazikuta topic zake. Ukizikosa unanzisha thread kuhusu swali lako.

Mode:Baadhi ya wageni wanahitaji ka orientation japo kadogo.

P.
 
SAKATA la kupotea kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa, Ben Focus Saanane, litatimiza nusu mwaka wiki ijayo, Mei 18, mwaka huu, huku mchakato wa kumtafuta ukiwa umepitia hatua takribani nane bila mafanikio.

Saanane ambaye alikuwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, alitoweka Novemba 18 mwaka jana hadi sasa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka mamlaka za kiserikali kuhusu mwanasiasa huyo kijana.

Pamoja na kuendesha harakati za kisiasa Saanane pia alikuwa katibu wa taasisi inayoitwa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Nchini (UTG) ambayo imesajiliwa rasmi hapa nchini.

Hatua saba kubwa zilizokwishafanyika bila mafanikio ni kupekuwa kumbukumbu zake Idara ya Uhmiaji (kama yupo nje ya nchi), kukagua hospitali mbalimbali, kukagua mahabusu na magereza, vyumba vya kuhifadhia maiti kwa nyakati tofauti.

Hatua nyingine ni kutoa shinikizo kwa Chadema na serikali kuhusu kutafutwa kwa mwanasiasa huyo, kujaribu bila mafanikio kukagua miili iliyookotwa mto Ruvu na kuzikwa kinyemela na kuanzisha kampeni maalumu ya kuhamasisha mwanasiasa huyo apatikane akiwa hai.

Mwishoni mwa wiki Raia Mwema lilizungumza na ndugu, marafiki na baadhi ya viongozi wa Chadena kuhusu kupotea kwa Ben Saanane, na wameelezea masikitiko yao kuhusu kile walichodai ni uzembe wa vyombo dola kushughulikia suala hilo.

Mmoja wa viongozi wa UTG, Godlisten Malisa aliliambia Raia Mwema kuwa walitoa taarifa ya kupotea kwa katibu wao Ben Saanane makao makuu ya Jeshi la Polisi na katika kituo cha Tabata, Desemba 5, 2016 na kupewa RB namba TBT/RB/8150/2016.

"Jumatatu hiyo hiyo ya tarehe 5 Desemba mwaka 2016 UTG tulianza rasmi kumtafuta Ben maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo katika hospitali za Amana, Temeke, Mwananyamala na hospitali ya Taifa Muhimbili lakini kote tuliambulia patupu," alieleza Malisa na kuongeza;

"Kote huko tulipewa ushirikiano wa kutosha na tulikagua vyumba vya wagonjwa mahututi, na orodha ya wagonjwa waliolazwa hospitalini humo wasiotambulika (unknown cases) na katika vyumba vya kuhifadhia maiti lakini hatukumpata."

Alieleza zaidi kuwa kati ya Desemba 6 na 7 mwaka 2016, UTG walipita mahabusu katika vituo vyote vikubwa vya polisi jijini Dar es Salaam na magereza yanayotunza mahabusu ya Keko na Segerea lakini Ben Saanane hakuwemo katika orodha ya mahabusu waliowahi kufikishwa katika magereza hayo.

UTG walifuatilia taarifa za Ben pia katika Idara ya Uhamiaji ili kujua kama Ben amesafiri nje ya nchi, ambapo Idara hiyo ilitoa taarifa kuwa Ben hajasafiri nje ya nchi kwa kipindi cha mwezi Novemba na Desemba kama ilivyodhaniwa awali.

Kiongozi huyo wa UTG alieleza zaidi kuwa Desemba 8 mwaka huu wa 2016 walisafiri kwenda Bagamoyo kujiridhisha kama miili iliyookotwa huko mto Ruvu inahusiana na Ben kwa namna moja au nyingine, lakini walipofika walikuta miili yote imekwishazikwa bila kuacha kielelezo chochote cha utambuzi.

"UTG tulitoa saa 72 kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na taasisi za kiserikali kuchukuwa hatua juu ya sakata la Ben na miili iliyozikwa Bagamoyo na Desemba 14, Chadema iliitikia wito wetu ambapo Mnadhimu Mkuu wa Chama, Tundu Lissu, alifanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu suala hilo." aliongeza Malisa.

Alisema Desemba 13 (ndani ya saa 72 za UTG) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kuwabaini waliohusika na mauwaji ya watu saba ambao miili yao iliokotwa pembezoni mwa mto Ruvu wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ili hatua kali kwa zichukuliwe kwa waliohusika na mauwaji hayo.

Kwa mujibu wa Malisa, UTG pia wameanzisha kampeni mpya ya "Bring Back Ben Alive" kama moja ya njia ya kuhamasisha juhudi za kumtafuta Ben kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Kwa upande wake ndugu wa Ben Saanane aliyejitambulisha kwa jina la Erasto, akizungumzia sakata hilo alidai kuwa kampuni ya simu ambayo Ben alikuwa akitumia huduma zake, iliwasilisha taarifa ya mawasiliano ya Ben kwa Jeshi la Polisi, Desemba 14, mwaka 2016.

"Taarifa ya mawasiliano ya simu ya Ben ilikuwa na upungufu mwingi hasa taarifa ya mawasiliano ya mwisho. Mawasiliano yaliyowasilishwa Jeshi la Polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao (cyber crime) yanaonesha kuwa Ben aliwasiliana mara ya mwisho kupitia simu yake tarehe 16/11/2016, lakini Ben aliondoka nyumbani kwake tarehe 18/11/2016 tunatilia shaka kwamba huenda mawasiliano ya Ben ya siku mbili za mwisho (tarehe 17 na 18) yamefichwa kwa sababu maalumu," alidai.

Mshauri wa kisheria wa UTG, Bob Wangwe, alisema wamewasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ambayo kikatiba ina mamlaka ya kusikiliza mashauri au malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu kwa mujibu wa ibara ya 130 na 131 ya Katiba ya Jamuhuri wa Tanzania.

Tume hiyo ina mamlaka ya kumwita na kumhoji mtu yeyote katika Jamuhuri ya Muungano isipokuwa Rais wa Tanzania, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar.

"Kwa mamlaka yake tume inaweza kuwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi na kuwahoji juu ya matukio ya kuogofya yanayoendelea nchini ya watu kupotea na wengine kuripotiwa kuteswa au miili yao kuokotwa wakiwa wamekufa," alifafanua Wangwe.

Alisema, kupitia UTG, wanaiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imuagize Mkemia Mkuu wa Serikali (GC) kwa kushirikiana na mamlaka nyingine wafukue miili ya watu saba waliozikwa kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo ili ifanyiwe vipimo vya vinasaba (DNA test).

Wangwe alisema pia wamefanya mazungumzo na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kukiomba kupeleka malalamiko rasmi Umoja wa Mataifa (UN) juu ya matukio ya Watanzania kutoweka katika mazingira tata, akiwemo Ben Saanane.

"Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba tayari LHRC wamekwishaandika barua hiyo Umoja wa Mataifa kuwaomba kuleta wataalamu watakaokuja kuchunguza matukio haya ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa," alisema Wangwe.

Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema chama hicho kimechukuwa hatua mbalimbali ikiwemo kuhakikisha mawaziri wote vivuli bungeni wanagusia suala la Ben Saanane katika hotuba zao wanazowasilisha bungeni.

"Ni Tanzania pekee duniani ambapo mtu anaweza 'akayeyuka hewani' na vyombo vya dola vikashindwa kumpata na kutoa maelezo yanayoweza kuridhisha umma," alidai Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.

Hivi karibuni Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliishauri serikali kuomba wataalamu wa uchunguzi kutoka Uingereza (Scotland Yard) kuja kuchunguza suala la kupotea kwa Ben Saanane.

Hata hivyo serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Majaliwa ilipinga mpango huo kwa madai kuwa vyombo vyetu vya usalama havijashindwa kufanya kazi hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Imekuwa ni kawaida ya chadema kuungana na mabeberu na kuanza kuombea mabaya nchi yetu. Pamoja na maombezi yao hayo bado laana ipo upande wa chadema tangu kutoka rais Magufuli aingie madarakani miaka minne iliyopita.

Kila wakiombea uchumi ushuke ndiyo kwanza unapanda.

Kila wakiombea tushitakiwe MIGA ndiyo kwanza Barrick wanakuja kusaini mikataba mipya yenye manufaa kwa watanzania wote.

Kila wakisingizia serikali ya Magufuli ina fanya mauaji ndiyo kwanza Saed Kubenea anawaumbua kwenye magazeti yake kwamba Ben Saanane anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa mitaa ya UFIPA.
IMG_20200202_065946.jpeg
Screenshot_20200201-212750.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imekuwa ni kawaida ya chadema kuungana na mabeberu na kuanza kuombea mabaya nchi yetu. Pamoja na maombezi yao hayo bado laana ipo upande wa chadema tangu kutoka rais Magufuli aingie madarakani miaka minne iliyopita.

Kila wakiombea uchumi ushuke ndiyo kwanza unapanda.

Kila wakiombea tushitakiwe MIGA ndiyo kwanza Barrick wanakuja kusaini mikataba mipya yenye manufaa kwa watanzania wote.

Kila wakisingizia serikali ya Magufuli ina fanya mauaji ndiyo kwanza Saed Kubenea anawaumbua kwenye magazeti yake kwamba Ben Saanane anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa mitaa ya UFIPA.View attachment 1344165View attachment 1344166

Sent using Jamii Forums mobile app

What the fvck is this?

Vichaa wengi sana!
 
Back
Top Bottom