Mmoja wa wanahabari maarufu na muendeshaji wa kipindi maarufu cha mboni show kinachooneshwa na kituo cha television cha East Africa TV, mjasiriamali na icon maalum ya wanawake wenye uthubutu katika nchi ya tanzania na Africa kwa ujumla Mboni Masimba ametangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mboni amefikia uamuzi huo baada ya kutathimin hali ya siasa hapa nchini na kuona kuwa chama pekee chenye msimamo na sura ya utaifa ni CCM na kwamba vyama vingine vinaendeshwa kibabaishaji na upendeleo wa waziwazi. "Unajua mimi nimekaa muda mrefu bila kujiunga na chama chochote cha siasa nikiwa nafanya tathmin juu ya hali ya siasa na hivyo baada ya kujiridhisha kuwa Chama Makini ni CCM ndipo nimeamua sasa kujiunga nacho." Alisema Mboni.
Tukio la kumkaribisha Mwanamke huyo ambae ni muwakilishi wa wanawake wajasiriamali, wanahabari na wenye uthubuti nchini litafanyika hivi karibuni baada ya mapumziko ya sikukuu za christmass na Mwaka mpya.
Mapokezi hayo yatakayoambatana na ghafla fupi yatafanyika jijini Dar es salaam katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Lumumba ambapo katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. NAPE NNAUYE ataongoza mapokezi hayo ya kada huyo mpya wa Chama Cha Mapinduzi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.