Mwanafunzi wangu amenidhalilisha

Mwanafunzi wangu amenidhalilisha

MTU UNA HIPS KAMA BASHITE AFU UNAVAA MODO DARASANI UNATEGEMEA NN???
 
Wakuu wenzangu poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa letu.

Naomba nijitambulishe, mimi ni mwalimu wa shule za English medium, yaani shule za mchepuo wa lugha ya kiingereza.

Huwa nafundisha madarasa ya mtihani, wale darasa la saba na darasa la nne. Tatizo limeanzia baada ya mwalimu mwenzetu mmoja anayefundisha darasa la tatu kwenda masomoni, sasa nikiwa kama mwalimu wa taaluma niliamua kugawa vipindi vya mwalimu huyu kwa wengine na mimi nikachukua somo la sayansi.

Sasa Leo nikiwa katika kipindi nafundisha na kuandika notisi,kuna kitu cha ajabu kilitokea, mtoto mmoja wa kike aliita sir, nikageuka kumsikiliza akasema"mwalimu Neema kasema eti huyu mwalimu ilibidi awe msichana"(mimi)

Wakuu mwili ulikufa ganzi, nikaishiwa pozi, ilibidi nipotezee ili kuwatuliza wanafunzi maana niliona walidhani labda nitahamaki, kisha nikawaelekeza wale watoto wawili wake ofisini baada ya kipindi.

Walipofika nikataka kiini cha Neema kusema vile akasema akaniangalia nilivyo eti nimefanana na dada yake Dah! Nilikasirika sana ila Neema akajitetea kuwa hata rafiki yake aliemtaja yeye naye husema hivyo hivyo.

Niliwaonya wale wanafunzi kwa kuwapa counselling tu, sikuwaadhibu

Je, wakuu ingekuwa ni wewe ungechukua hatua gani, ili kama nimekosea niboreshe.
kweli wanaume tunazidi kupungua................
 
  • Thanks
Reactions: B40
Teacher ungetuonesha pc yako ingekuwa poa kweli
Ili kuepusha dhana baina ya ww na your students wako
 
Vitu kama unavipotezea...sio utangaze hadharani mkuu watu watakufikilia vibaya shauri yako
 
je unazingatia haiba ya mwalimu anayotakiwa kuwa nayo? maana nyie walimu wa siku hiz hatari tupu..mnavaa surual za kubana na mashati yaani kiufupi wengi wenu hamna maadili.
 
Kwenye maisha kuna vitu unaweza kuchagua kua navyo na vingine huna uwezo wa kuchagua kua navyo au kuto kua navyo; kimoja wapo ni mwonekano wako wa sura hilo hupangi wewe; yawezekana wewe unafanana na mama yako na sio baba yako, that much is out of your capacity, you cant change it ni suala la Mungu na wala sio wazazi wako wala wewe, ni issue ya uumbaji wa Mungu mwenyewe. So yawezekana kweli umefanana na dada yao huwezi jua. Nakupongeza sana kwa jinsi ulivyo wa treat hao watoto cause ungewapiga ukweli ni kwamba wala wasingeelewa kosa lao ni lipi, wao wanaona umefanana na dada yao and that is not one of their mistake. Kweli wewe ni mwalimu na mimi nakupongeza. Nimeandika haya nikiwa sijasoma comment ya mtu hata mmoja kwenye uzi wako so sielewi stands za wenzangu concerning this, to me I give you 5
 
  • Thanks
Reactions: B40
fuga ndefu, acha kuonyesha onyesha simu kwa wanafunzi na hasa kujipigapiga selfie huku wakiona-inasemekana wanaume wanaopeda kujipiga/au kupigwa picha wana genes za kike
 
  • Thanks
Reactions: B40
Back
Top Bottom