B40
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 820
- 537
Wakuu wenzangu poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa letu.
Naomba nijitambulishe, mimi ni mwalimu wa shule za English medium, yaani shule za mchepuo wa lugha ya kiingereza.
Huwa nafundisha madarasa ya mtihani, wale darasa la saba na darasa la nne. Tatizo limeanzia baada ya mwalimu mwenzetu mmoja anayefundisha darasa la tatu kwenda masomoni, sasa nikiwa kama mwalimu wa taaluma niliamua kugawa vipindi vya mwalimu huyu kwa wengine na mimi nikachukua somo la sayansi.
Sasa Leo nikiwa katika kipindi nafundisha na kuandika notisi,kuna kitu cha ajabu kilitokea, mtoto mmoja wa kike aliita sir, nikageuka kumsikiliza akasema"mwalimu Neema kasema eti huyu mwalimu ilibidi awe msichana"(mimi)
Wakuu mwili ulikufa ganzi, nikaishiwa pozi, ilibidi nipotezee ili kuwatuliza wanafunzi maana niliona walidhani labda nitahamaki, kisha nikawaelekeza wale watoto wawili wake ofisini baada ya kipindi.
Walipofika nikataka kiini cha Neema kusema vile akasema akaniangalia nilivyo eti nimefanana na dada yake Dah! Nilikasirika sana ila Neema akajitetea kuwa hata rafiki yake aliemtaja yeye naye husema hivyo hivyo.
Niliwaonya wale wanafunzi kwa kuwapa counselling tu, sikuwaadhibu
Je, wakuu ingekuwa ni wewe ungechukua hatua gani, ili kama nimekosea niboreshe.