Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje?

Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje?

Nimeleta uzi Jana wa Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje? kuomba ushauri kuhusu huyu kijana ambae naishi na mama yake nyumba moja, na tunaishi na huyu kijana pia mwenye miaka 21, mimi Nina 34 na mpenzi wangu ana 51.

Lakini kinyume na matarajio yangu nimetukanwa sana kwenye uzi huo kwamba nimefuata pesa kwa mama huyo, kwamba mimi ni marioo.
Nimesikitishwa sana hivyo naomba kusahihisha.

(1) Wakati wanafungua chuo huyu kijana aliombwa na mama yake akakae hostel ili tupate nafasi ya kupumua mle ndani lakini akakataa, lengo la kukataa ni kutaka kutuvurugia mapenzi yetu, na ameapa atayavuruga tu kwa namna yoyote ile.

(2) Huyu kijana ana baba yake aliemkimbia mama yake na kwenda kuoa mwanamke mwingine, sasa mama yake nae akiwa na mpenzi kuna ubaya?

Na kwanini basi asiende kuishi kwa baba yake DSM?
Hadi anganganie hapa na kutuletea fujo!
Isitoshe mim ini mkubwa kwake 34 kwa 21 ni tofauti kubwa sana ya umri, mimi sio age mate wake, mnaobeza tofauti hiyo mnanishangaza sana.

(3) Ingekua tunazungumzia mwanaume ana hata 80 yrs na binti 18 yrs msingeona ajabu, tena akina dada wangekua wanashabikia kabisa, lakini inapotokea mwanamke ndie mkubwa inakua ajabu
Sielewi kwanini mnakua hivyo.

Huyu mwanamke wangu anajiweza kimaisha na ameamua kunisaidia mimi kimaisha kama mpenzi wake ambae nilikua najikongoja kimaisha, kuna ubaya?Mbona mwanaume tajiri anapomsaidia binti maskini maisha hamsemi?

Ikiwa kinyume chake ndio mnasema? Wakati kuna thawabu nyingi sana mwanamke akifanya hivyo.Nimemvumilia sana huyu kijana na nimefika mwisho, hawezi kunitangaza mimi mtaa mzima na kunidhalilisha kwa ndugu na jamaa, mbona alipotaka kufukuzwa na mama yake mimi niliingilia kati?

Mimi pia ni mafia, nafanya utu tu, sasa utu huo nauvua ngoja tuone sasa na nyinyi wanaume wenzangu humu ndani inakuaje mnashindwa kuniunga mkono na kunipa support kwa jambo hili?

Mnaungana na watoto wa kike kunishambulia badala ya kunishauri njia nzuri ya kutatua hili tatizo.Mimi na mpenzi wangu tulitaka kufunga ndoa siku nyingi ili tuweze kuishi kwa amani na upendo lakini kutokana na huyu kijana mama yake anaahirisha kila Mara, anajaribu kunivurugia.

Ngoja tutaona, nimechoka sasa.

huna hata aibu mwanaume mzima unatumia jasho la mwanamke,huna lolote wala hauna mapenzi ya kweli na huyo mama hapo ulipo unakimchepuko chako huko kinachokuliwaza,unasubiria mama wa watu afe ili wewe ndio urithi mali zake,na kwa taarifa yako tofauti ni kubwa sana kwa mwanamke wa 18 kuwa na babu wa 80 kuliko wewe mwanaume wa 34 kuwa na mama wa 50,sie wanawake tunahuruma na roho ya kusaidia na kumpenda mtu kiukweli ila nyie wanaume hamjaumbwa ivyo,ndio maana sie wanawake tukimfumania mume wetu tunasamehe ila nyie hamsamei,so wala usitudanganye hapa tuku support ujinga ni kweli umefata hela za huyo mama na mali zake,umefata mtelezoo
 
mkuu huna point ya msingi...kifupi tafuta mwanamke wa umri wako ambaye utaweza kumuoa huyo kijana ana haki ya kulaani kwa kuwa njaa yako ndo yakupeleka kwake, una dhulumu urithi wa hao watoto, huyo mama akifa we ndo usimame kama mrithi wa mali huo ni uendawazimu mkuu...... kama la msingi msiwe mnatupotezea mda kuweka nyuzi za kijinga wadhani nasi ni wajinga na waroho wa mali kama ulivyo wewe....kuwa basi hata na aibu

like, like. like, like, like,....umeongea point mkuu
 
Lady Jaydee hakukosea.
Kuna wanaume kama mabinti .
Kwa umri wako hupaswi uendelee kutetea huo ujinga.
Njaa itakufikisha usikotegemea
 
Unataka mtoto aende kwa baba ake! Wewe huna baba nawe ukaenda kwa baba ako?
 
Eti Mafia mimi Mafia ninaowajua kina Gambino, Al Capone, Luciano wote wana pesa na hawategemei umariyoo... Kwa ajili ya kuishi ungekuwa Mafia ungekuwa tayari una mijengo yako kadhaa plus businesses and cars kibao ungekuwa mafia usingetegemea msingi kiuno wewe sikuoni kama ni Mafia ila nakuona kama mganga NJAA ambaye umeona huyo Mama ndio pa kutokea
 
Leo umeniangusha, umekua mgumu sana kuelewa, yani umri wao, mapenzi yao, kama sheikh anahongwa, kama ni marioo hayo ni makubaliano yao hayahusu hata kidogo..... Tatizo ni huyu jamaa kuhamia pale home hebu assume ni wewe unaishi kwenu na mama halafu mama analeta kibuzi maringo humo ndani kiishi hivi utajisikiaje?
 
Last edited by a moderator:
huna hata aibu mwanaume mzima unatumia jasho la mwanamke,huna lolote wala hauna mapenzi ya kweli na huyo mama hapo ulipo unakimchepuko chako huko kinachokuliwaza,unasubiria mama wa watu afe ili wewe ndio urithi mali zake,na kwa taarifa yako tofauti ni kubwa sana kwa mwanamke wa 18 kuwa na babu wa 80 kuliko wewe mwanaume wa 34 kuwa na mama wa 50,sie wanawake tunahuruma na roho ya kusaidia na kumpenda mtu kiukweli ila nyie wanaume hamjaumbwa ivyo,ndio maana sie wanawake tukimfumania mume wetu tunasamehe ila nyie hamsamei,so wala usitudanganye hapa tuku support ujinga ni kweli umefata hela za huyo mama na mali zake,umefata mtelezoo

Angekuwa kaoa labda kidogo ingeleta mantiki..ila uzini na mama yangu na tena kwenye nyumba yetu AF unataka heshima yangu,labda kama unipumbaze kwa miti shamba ulionayoo.
 
Binafsi nimegoma kukuelewa. Unatia aibu. Badala upambane kivyako, unataka umtenganganisha mama na mtoto wake? shindwa mbwelu wewe. Eti na mimi ni mafia mafi what? Mafia your ass.
 
Nimeleta uzi Jana wa Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje? kuomba ushauri kuhusu huyu kijana ambae naishi na mama yake nyumba moja, na tunaishi na huyu kijana pia mwenye miaka 21, mimi Nina 34 na mpenzi wangu ana 51.

Lakini kinyume na matarajio yangu nimetukanwa sana kwenye uzi huo kwamba nimefuata pesa kwa mama huyo, kwamba mimi ni marioo.
Nimesikitishwa sana hivyo naomba kusahihisha.

(1) Wakati wanafungua chuo huyu kijana aliombwa na mama yake akakae hostel ili tupate nafasi ya kupumua mle ndani lakini akakataa, lengo la kukataa ni kutaka kutuvurugia mapenzi yetu, na ameapa atayavuruga tu kwa namna yoyote ile.

(2) Huyu kijana ana baba yake aliemkimbia mama yake na kwenda kuoa mwanamke mwingine, sasa mama yake nae akiwa na mpenzi kuna ubaya?

Na kwanini basi asiende kuishi kwa baba yake DSM?
Hadi anganganie hapa na kutuletea fujo!
Isitoshe mim ini mkubwa kwake 34 kwa 21 ni tofauti kubwa sana ya umri, mimi sio age mate wake, mnaobeza tofauti hiyo mnanishangaza sana.

(3) Ingekua tunazungumzia mwanaume ana hata 80 yrs na binti 18 yrs msingeona ajabu, tena akina dada wangekua wanashabikia kabisa, lakini inapotokea mwanamke ndie mkubwa inakua ajabu
Sielewi kwanini mnakua hivyo.

Huyu mwanamke wangu anajiweza kimaisha na ameamua kunisaidia mimi kimaisha kama mpenzi wake ambae nilikua najikongoja kimaisha, kuna ubaya?Mbona mwanaume tajiri anapomsaidia binti maskini maisha hamsemi?

Ikiwa kinyume chake ndio mnasema? Wakati kuna thawabu nyingi sana mwanamke akifanya hivyo.Nimemvumilia sana huyu kijana na nimefika mwisho, hawezi kunitangaza mimi mtaa mzima na kunidhalilisha kwa ndugu na jamaa, mbona alipotaka kufukuzwa na mama yake mimi niliingilia kati?

Mimi pia ni mafia, nafanya utu tu, sasa utu huo nauvua ngoja tuone sasa na nyinyi wanaume wenzangu humu ndani inakuaje mnashindwa kuniunga mkono na kunipa support kwa jambo hili?

Mnaungana na watoto wa kike kunishambulia badala ya kunishauri njia nzuri ya kutatua hili tatizo.Mimi na mpenzi wangu tulitaka kufunga ndoa siku nyingi ili tuweze kuishi kwa amani na upendo lakini kutokana na huyu kijana mama yake anaahirisha kila Mara, anajaribu kunivurugia.

Ngoja tutaona, nimechoka sasa.

Bila shaka huu ni utani wala humaanishi kwamba utaka kufunga ndoa na kikongwe. Lengo la mapenzi yenu ni yapi?
 
Ha ha ha ha eti mpate nafasi ya kupumua ndani, kapumulie kwenye frame yako huko
Kama huyu jamaa si mgonjwa wa akili basi hii ni chai...! Jamaa ana kera sana linasema wazi kabisa linahitaji nafasi kwenye nyumba ya mwanaume mwenzie....! Huyu ni janga zaidi ya VVU
 
Ha ha ha ha yani nmecheka sana tena baada ya huu mrejesho wenye mkwara
 
Wewe Ni sheikh gani mpumbavu kiasi hivyo???????????? Unafaa kutafunwa kalio lako kabisa
 
Back
Top Bottom