sheikh yasin
Member
- Aug 6, 2015
- 61
- 50
Wakuu,
Kuna huyu mama wa makamo ana 51 kwa sasa, kuna kazi ya matibabu nilimfanyia, huwa anasumbuliwa sana na mgongo, na mimi ni Herbalist, nina kijifrem changu Mwanza ambapo nafanya shughuli hizi.
Sasa huyu mama baada ya kufahamiana kwa muda tukajikuta tumekuwa wapenzi na baadae akaniomba nihamie kwake tuweze kuishi pamoja, kwamba yeye kwa makamo yale hawezi kuhamia kwangu, nikakubali nikahamia kwake, yupo vizuri sana kwa kweli, anaishi na watoto wake hapo, mmoja wa kiume 21 na mwingine 19 wa kike, kuna aliyeolewa yupo kwake.
Sasa huyu wa kiume yaani hanipendi kama nini sijui, hanisalimii wakati namzidi mbali nina 34, nikitoka na gari la mama yake ananitazama kama mtu ameona mavi. Ni mwanachuo, akiwa anamuomba mama yake pesa akinyimwa anakosa adabu kabisa na kumjibu kwamba mbona huyo mtu wako unampa hela.
Wakati yule binti mwingine wala hana neno na mimi, ananiamkia na kuniheshimu na huwa tunatoka nae outing mara kadhaa na mama yake.
Huyu kijana amekuwa akinizungumza vibaya hata kwa ndugu wengine wanaokuja nyumbani, imekua ni kero sana.
Naomba mawazo yenu

Nimeleta uzi Jana wa Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje? kuomba ushauri kuhusu huyu kijana ambae naishi na mama yake nyumba moja, na tunaishi na huyu kijana pia mwenye miaka 21, mimi Nina 34 na mpenzi wangu ana 51.
Lakini kinyume na matarajio yangu nimetukanwa sana kwenye uzi huo kwamba nimefuata pesa kwa mama huyo, kwamba mimi ni marioo.
Nimesikitishwa sana hivyo naomba kusahihisha.
(1) Wakati wanafungua chuo huyu kijana aliombwa na mama yake akakae hostel ili tupate nafasi ya kupumua mle ndani lakini akakataa, lengo la kukataa ni kutaka kutuvurugia mapenzi yetu, na ameapa atayavuruga tu kwa namna yoyote ile.
(2) Huyu kijana ana baba yake aliyemkimbia mama yake na kwenda kuoa mwanamke mwingine, sasa mama yake nae akiwa na mpenzi kuna ubaya?
Na kwanini basi asiende kuishi kwa baba yake Dar?
Hadi ang'ang'anie hapa na kutuletea fujo?
Isitoshe mimi ini mkubwa kwake 34 kwa 21 ni tofauti kubwa sana ya umri, mimi sio age mate wake, mnaobeza tofauti hiyo mnanishangaza sana.
(3) Ingekuwa tunazungumzia mwanaume ana miaka 80 na binti miaka 18 msingeona ajabu, tena akina dada wangekuwa wanashabikia kabisa, lakini inapotokea mwanamke ndie mkubwa inakua ajabu!
Sielewi kwanini mnakua hivyo.
Huyu mwanamke wangu anajiweza kimaisha na ameamua kunisaidia mimi kimaisha kama mpenzi wake ambae nilikuwa najikongoja kimaisha, kuna ubaya? Mbona mwanaume tajiri anapomsaidia binti maskini maisha hamsemi?
Ikiwa kinyume chake ndio mnasema? Wakati kuna thawabu nyingi sana mwanamke akifanya hivyo. Nimemvumilia sana huyu kijana na nimefika mwisho, hawezi kunitangaza mimi mtaa mzima na kunidhalilisha kwa ndugu na jamaa, mbona alipotaka kufukuzwa na mama yake mimi niliingilia kati?
Mimi pia ni mafia, nafanya utu tu, sasa utu huo nauvua ngoja tuone sasa na nyinyi wanaume wenzangu humu ndani inakuwaje mnashindwa kuniunga mkono na kunipa support kwa jambo hili?
Mnaungana na watoto wa kike kunishambulia badala ya kunishauri njia nzuri ya kutatua hili tatizo. Mimi na mpenzi wangu tulitaka kufunga ndoa siku nyingi ili tuweze kuishi kwa amani na upendo lakini kutokana na huyu kijana mama yake anaahirisha kila Mara, anajaribu kunivurugia.
Ngoja tutaona, nimechoka sasa.