Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje?

Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje?

Basi bora ampige na kitu kizito kuliko kuendelea kufedheheka hivyo!

Kweli ampige tu maana hamna namna msela mwenyewe anajifanya king'ang'a kafa kaoza ***** kama nakaona kamejifunga taulo kanatoka chumbani kanapita kwenda kuoga.....aisee kijana anaachaje kukakata mtama kaangukie mdomo kaangushe meno ya sebleni
 
Huyu mpenzi wangu hataki niondoke, nilileta ombi hilo baada ya ugomvi mkubwa ndani kati ya kijana na mama yake, lakini hata hivyo mama alikua tayari kumfikuza huyo kijana home, nikaingilia kati na kumuomba asifanye hivyo

Nashindwa kuelewa tatizo la huyu kijana ni nini hasa?

Si uondoke tu

Unavyozidi kukaa kuna ndugu wa baba yao watakumaliza.

Kinachokukalisha hapo ni nini? Rudi kwako na acha kutumia mali za baba yao.
 
Nimeleta uzi Jana wa Mwanae hanitaki kabisa, nifanyeje? kuomba ushauri kuhusu huyu kijana ambae naishi na mama yake nyumba moja, na tunaishi na huyu kijana pia mwenye miaka 21, mimi Nina 34 na mpenzi wangu ana 51.

Lakini kinyume na matarajio yangu nimetukanwa sana kwenye uzi huo kwamba nimefuata pesa kwa mama huyo, kwamba mimi ni marioo.
Nimesikitishwa sana hivyo naomba kusahihisha.

(1) Wakati wanafungua chuo huyu kijana aliombwa na mama yake akakae hostel ili tupate nafasi ya kupumua mle ndani lakini akakataa, lengo la kukataa ni kutaka kutuvurugia mapenzi yetu, na ameapa atayavuruga tu kwa namna yoyote ile.

(2) Huyu kijana ana baba yake aliemkimbia mama yake na kwenda kuoa mwanamke mwingine, sasa mama yake nae akiwa na mpenzi kuna ubaya?

Na kwanini basi asiende kuishi kwa baba yake DSM?
Hadi anganganie hapa na kutuletea fujo!
Isitoshe mim ini mkubwa kwake 34 kwa 21 ni tofauti kubwa sana ya umri, mimi sio age mate wake, mnaobeza tofauti hiyo mnanishangaza sana.

(3) Ingekua tunazungumzia mwanaume ana hata 80 yrs na binti 18 yrs msingeona ajabu, tena akina dada wangekua wanashabikia kabisa, lakini inapotokea mwanamke ndie mkubwa inakua ajabu
Sielewi kwanini mnakua hivyo.

Huyu mwanamke wangu anajiweza kimaisha na ameamua kunisaidia mimi kimaisha kama mpenzi wake ambae nilikua najikongoja kimaisha, kuna ubaya?Mbona mwanaume tajiri anapomsaidia binti maskini maisha hamsemi?

Ikiwa kinyume chake ndio mnasema? Wakati kuna thawabu nyingi sana mwanamke akifanya hivyo.Nimemvumilia sana huyu kijana na nimefika mwisho, hawezi kunitangaza mimi mtaa mzima na kunidhalilisha kwa ndugu na jamaa, mbona alipotaka kufukuzwa na mama yake mimi niliingilia kati?

Mimi pia ni mafia, nafanya utu tu, sasa utu huo nauvua ngoja tuone sasa na nyinyi wanaume wenzangu humu ndani inakuaje mnashindwa kuniunga mkono na kunipa support kwa jambo hili?

Mnaungana na watoto wa kike kunishambulia badala ya kunishauri njia nzuri ya kutatua hili tatizo.Mimi na mpenzi wangu tulitaka kufunga ndoa siku nyingi ili tuweze kuishi kwa amani na upendo lakini kutokana na huyu kijana mama yake anaahirisha kila Mara, anajaribu kunivurugia.

Ngoja tutaona, nimechoka sasa.
 
Hii kanuni ya umri wa miaka fulani kuwa na fulani inatoka wapi? Nani kaianzisha? Huyu bwana anakuwa anatenda dhambi kwa kufanya hivyo kama wamefuata njia sahihi. Kaeleza akitoka na gari ya huyo mwanamke, amesema yeye hana? Kwanini tunakimbilia kuwaza mali tu, je na sisi tulifuata mali? Ni kweli haiwezekani watu hao wakapendana?
Jamani tuamini, kila mtu anaweza akachagua anachotaka. Angekuwa mwanaume amevuta binti wa umri huo tusingeonana kelele. Kwanini kanuni ya kimila tuilazimishe kwa kila mtu?

Naona kama kuna ka ukweli ndani yake.
 
Huyu jamaa ni king'ang'anizi kama Hashim Rungwe na apigwe tuu uploadfromtaptalk1448008207539.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom